Dp800
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 1,793
- 3,709
Kwamba ninyi ubongo wenu ndio umefunguka? Naamini hujijui wewe ni naniHuwezi kuelewa, ni mpaka ufungue ubongo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwamba ninyi ubongo wenu ndio umefunguka? Naamini hujijui wewe ni naniHuwezi kuelewa, ni mpaka ufungue ubongo.
Unashangaa utadhani hauishi Tanzania. Em angalia hata majirani zako hapo usiende mbali.Dah Miaka 24 unakaa kwenu??
🤣🤣🤣🤣🤣🙆🙆🙆🙆🙆Hapana mkuu, ukiona mwanamke ana uwezo wa ku reason maswala ya kiimani huyo ni level nyingine. Nadhani jf nzima hawazidi 10.
Tenga hata dakika 5 za kutafakari utalewaKwamba ninyi ubongo wenu ndio umefunguka? Naamini hujijui wewe ni nani
30+🤣🤣🤣🤣🤣🙆🙆🙆🙆🙆
Una miaka mingapi?!
Ukienda Rumi ishi kama Warumi, siku ukiwa na kwako basi ishi kwa kanuni zako.Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.
Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.
Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.
Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.
Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"
Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"
Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"
Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"
Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"
Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.
Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.
Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"
Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.
Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.
Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana
Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"
Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.
Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?
Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Tenga hata dakika 5 za kutafakari utalewa
Kwamba ninyi hamuamini katika Mungu sasa nitenge muda kwa ajili ya huko kutokuamini kwenu?Tenga hata dakika 5 za kutafakari utalewa
Kabisa na ukitaka kujua upumbavu na udumavu wa akili wa mtu mweusi ,we soma hizi comments humu .Hizi dini ndio zimewafanya waafrika muwe hapa mlipo.. hongera mtu mweupe kwa ujinga aliotuleta
Nyie ndio mnaosapoti mpaka FGM
Ndio, kwa majina naitwa whiteskunkKwamba ninyi hamuamini katika Mungu sasa nitenge muda kwa ajili ya huko kutokuamini kwenu?
Nimekuuliza unanijua wewe ni nani?
Mkuu asante kwa ushauri. Nimesoma vitabu vingi sana vya dini ambavyo najua hata wengi wanaoniattack hapa hawajawahi hata kuvisikia.Pamoja na kwamba siungi mkono kutokusali; ila kwa ulivyo andika tu, you are so bright na unahitaji kuelekezwa kwa hoja za nguvu na sio kwa mazoea. Nakushauri pamoja na kutowiwa kwenda kanisani nakushauri Usome; kama ulisha soma Biblia jaribu kusoma Vitabu vya Dini tofauti.
Hii inaweza kukusaidia kwani bottom line; Mungu yupo, siku ya mwisho ipo, ambapo watu watahukumiwa kutoa haki kwa walioikosa hapa duniani ILA namna gani ya kumjua Mungu sahihi wa kumfuata ndio kazi hapo......SOMA!
Mtoto ako akikwambia baba me sitak kwenda shule kwa sabb yote ni ukoloni na yametengezwa/yameletwa na binadamu utachukua uamuzi gani?
Kapange ili ujipangie cha kufanya, unachopinga hapa wala hakina msingi. Dini ni majina tu ya kutofautisha kati ya zote zilizopo ila Imani ndiyo yampasa mtu kuwa nayo na kuendana na kile ambacho muumba katuhusia.Sawa sasa kwanini haniachi?
Mtu mzima aliyezidi 18 ni wa kulazimisha dini kweli?
Hapo tu ukute una degree ya saut😤
Okay, nmekuelewa. So kwasababu hana uelewa wacha niendelee kumfurahisha tu katika huo uelewa wake.