Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahyo mama/Baba akiamua sasa nikafanyiwe tohara ni sawa kwakuwa ni mamlaka na sina uhuru wa kuchagua???Siku ukiishi kwako ndio tutajadili kisomi.
Kwa sasa humu watu wote mpaka wajinga wanashangaa mtu mwenye Degree kuwa na upeo mdogo kiasi hiki.
Huo usomi unaojifanya nao utumie kujitegemea uondoke hapo nyumbani. Au ukishindwa utumie kuelewa kuwa hapo kwenu ni mamlaka kamili inayojiendesha Kwa taratibu na sheria za familia kulingana na utashi wa mama au Baba WA hiyo nyumba
Kwahyo kigezo cha kumpa mtu uhuru wa maamuzi kwakuwa amekua ni kipi? (Kama sio umri)Kua na Age 18+ au 18- Sio kigezo cha kua na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.. Kuna wengine wana30+ lakini bado ni wa hovyo tu... Kua uyaone!!
NB: Kua makini sana na Unayosikia, Unayotizama na Unayosoma..
Umesoma vitabu gani? Vitaje nataka nisome.Mkuu asante kwa ushauri. Nimesoma vitabu vingi sana vya dini ambavyo najua hata wengi wanaoniattack hapa hawajawahi hata kuvisikia.
Wewe unaamini nikivisoma hivyo vitabu lazima nitaamini Mungu, je una uhakika? Okay tuseme unao uhakika.
Je ni sahihi kumlazimisha mtu kusoma hivyo vitabu hata kama hapendi?
Kuna quote nimesahau nani alisema "Religion can make even a proffesor act foolish"Kabisa na ukitaka kujua upumbavu na udumavu wa akili wa mtu mweusi ,we soma hizi comments humu .
Masharti mengine yote sawa. ila hili naona linahusiana na imani. Sasa mtu umlazimishe kuamini kitu fulani ni haki?Ukitaka uhuru basi jitegemer uwe na kwako, mimi hapa nina miaka karibia 10 silijui kanisa na hakuna mtu ananiuliza.
Ukikaa kwa watu fuata masharti.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahyo mama/Baba akiamua sasa nikafanyiwe tohara ni sawa kwakuwa ni mamlaka na sina uhuru wa kuchagua???
Wala sishangai wengi unaowaita 'wasomi' na wasio wasomi wakinishangaa....sijaandika kwaajili yao. sijaandika hii kwaajili ya average minds Nimeandika kwaajili ya wale wachache watakaonielewa. (Above average)View attachment 2439026
Zingatia hii graph
Unasema sio shurti halafu unasema tema Lazima nitii...hiyo si ndo maana ya shurti?Swala sio shurti ila kwa kuwa upo kwenye mamlaka yake lazima utii ila ukiwa nje ya kwakwe uko free kufanya unavyojisikiw yeye anaweza kukushauri tu.
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Masharti mengine yote sawa. ila hili naona linahusiana na imani. Sasa mtu umlazimishe kuamini kitu fulani ni haki?
Yesu alishikisha watu mapanga akawalazimisha kuamini dini yake?
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.
Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.
Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.
Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.
Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"
Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"
Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"
Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"
Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"
Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.
Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.
Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"
Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.
Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.
Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana
Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"
Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.
Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?
Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Tunaishi chini ya paa la serikali inayotuongoza...Je ni haki serikali kutulazimisa wananchi wote kuwa waislam?Unaishi chini ya paa lake, ama fuata mwongozo wake au kajitegemee hatokusumbua.
Yeye ukiishi chini yake anaona ni wajibu wake kukuongoza
Wewe ni so short sighted Sina Cha kukusaidia. Have a touble day.Doh! Wewe ni so closeminded mpaka sina la kukujibu. Have a nice day
Okay ntajaribu.Umezidi ujuaji...punguza ujuaji ...lol
Unasema sio shurti halafu unasema tema Lazima nitii...hiyo si ndo maana ya shurti?
Wewe kwa imani yako unaamini katika kulazimishana dini?
Yani mpaka umefikia hatua ya kusema kuwa mwanao akiacha dini sio mwanao bali ni maradhi.Kuna kuzaa na kutoa maradhi mwilini (alisikika mlevi mmoja akisema)
Ungekuwa mtu mzima ungekuwa na kwako.Sawa sasa kwanini haniachi?
Mtu mzima aliyezidi 18 ni wa kulazimisha dini kweli?