JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
Wazazi wangu ni waislamu swala 5, nilipokuwa narudi likizo nilipoteza kabisa imani na Mungu nilikuwa nafikiri kama wewe.Okay nmekupata, ila kwa umri wa wazazi sitajaribu kuwaelewesha..maana ni umri unaoaminika wa kumrudia muumba.
Kwahyo haitakuwa na maana wataona kama najaribu kuwapotosha niwanyime raha za mbinguni.
How did you solve your case?
Hatukuelewana sana waliniponiona muda wa kuswali umefika mimi niko ‘busy’ na mambo mengine, walinisihi sana mpaka wakawa wananikasirikia.
Kuona hali imekuwa mbaya kwa utaratibu nikaanza ku ‘question’ imani yao kwa maswali ‘rational’ nao wakawa wakali, lakini kwa taratibu nikawa nawaelewesha kidogokidogo ila kuna siku niliwaambia kuwa “mimi nahisi nimechanganyikiwa na hizi imani, (nikatolea mfano mgawanyiko wa madhehebu uliokuwepo)” kisha nikawaomba wanipe muda niendelee kujitafuta zaidi maana niko njia panda.
Alhamdulillah wakanielewa, wakasema wataniombea dua niijue imani ya kweli😂
Nami nikashukuru basi tukaishi kwa amani, ila niliporudi likizo tena tuliendelea kujadili dini walini ‘challenge’ walipopata nafasi nami nilifanya hivyo.
Mpaka sasa ninaamini Mungu yupo, na ni jukumu langu kumuabudu. Japo ni ‘work in progress’