Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Okay nmekupata, ila kwa umri wa wazazi sitajaribu kuwaelewesha..maana ni umri unaoaminika wa kumrudia muumba.
Kwahyo haitakuwa na maana wataona kama najaribu kuwapotosha niwanyime raha za mbinguni.

How did you solve your case?
Wazazi wangu ni waislamu swala 5, nilipokuwa narudi likizo nilipoteza kabisa imani na Mungu nilikuwa nafikiri kama wewe.

Hatukuelewana sana waliniponiona muda wa kuswali umefika mimi niko ‘busy’ na mambo mengine, walinisihi sana mpaka wakawa wananikasirikia.

Kuona hali imekuwa mbaya kwa utaratibu nikaanza ku ‘question’ imani yao kwa maswali ‘rational’ nao wakawa wakali, lakini kwa taratibu nikawa nawaelewesha kidogokidogo ila kuna siku niliwaambia kuwa “mimi nahisi nimechanganyikiwa na hizi imani, (nikatolea mfano mgawanyiko wa madhehebu uliokuwepo)” kisha nikawaomba wanipe muda niendelee kujitafuta zaidi maana niko njia panda.

Alhamdulillah wakanielewa, wakasema wataniombea dua niijue imani ya kweli😂

Nami nikashukuru basi tukaishi kwa amani, ila niliporudi likizo tena tuliendelea kujadili dini walini ‘challenge’ walipopata nafasi nami nilifanya hivyo.

Mpaka sasa ninaamini Mungu yupo, na ni jukumu langu kumuabudu. Japo ni ‘work in progress’
 
Kwa hiyo akiwa Muislamu halafu mzazi anamlazimisha kula kitimoto inabidi ale tu kumridhisha??
Hayo mengine utajua wewe na Mungu wako ila as long as upo kwa wazazi tii kile unachoambiwa hata kama utafanya kumridhisha tu ila mtii mzazi ndo Mungu wa duniani.
 
Wazazi wangu ni waislamu swala 5, nilipokuwa narudi likizo nilipoteza kabisa imani na Mungu nilikuwa nafikiri kama wewe.

Hatukuelewana sana waliniponiona muda wa kuswali umefika mimi niko ‘busy’ na mambo mengine, walinisihi sana mpaka wakawa wananikasirikia.

Kuona hali imekuwa mbaya kwa utaratibu nikaanza ku ‘question’ imani yao kwa maswali ‘rational’ nao wakawa wakali, lakini kwa taratibu nikawa nawaelewesha kidogokidogo ila kuna siku niliwaambia kuwa “mimi nahisi nimechanganyikiwa na hizi imani, (nikatolea mfano mgawanyiko wa madhehebu uliokuwepo)” kisha nikawaomba wanipe muda niendelee kujitafuta zaidi maana niko njia panda.

Alhamdulillah wakanielewa, wakasema wataniombea dua niijue imani ya kweli[emoji23]

Nami nikashukuru basi tukaishi kwa amani, ila niliporudi likizo tena tuliendelea kujadili dini walini ‘challenge’ walipopata nafasi nami nilifanya hivyo.

Mpaka sasa ninaamini Mungu yupo, na ni jukumu langu kumuabudu. Japo ni ‘work in progress’
Una bahati wazazi wako waelewa.
Mimi kama wangekuwa waelewa wangekuwa washaelewa.
ila sasa kwakuwa wameshupaza shingo, wacha nifanye wanachokitaka
 
Ndio maana nikamuambia mwenzako kuwa kama anaupeo mdogo WA MAMBO aache kujadili mambo makubwa.

Na Wewe upo kundi Hilo Hilo.

Kama hujui tofauti ya mambo haya jua unaakili mgando.
1. Dini Vs Imani
2. Elimu Vs Akili
3. Urembo Vs Uzuri
4. Mapenzi Vs Upendo

Mfano yeye amesoma mpaka Degree hivyo anaelimulakini Hana Akili

Yeye kuambiwa aende Kanisani haimaanishi awe na Imani na Dini au Kanisa Hilo.
Hapo ni suala la mamlaka na taratibu za familia.
Vipi kama mamlaka na taratibu za familia zinamtaka awe anapeleka sadaka au kushiriki ibada/matambiko katika makaburi ya familia??
 
.

Alafu kitu kingine usichokijua ni kuwa Kitendo cha kufuata sheria za Iran au Saudia ukiwa katika nchi hizo unakuwa muislam indirect way. Licha ya kuwa huendi msikitini. Kwa sababu dini nikufuata sheria na taratibu zilizoanishwa katika vitabu.
Mkuu, kwa sisi Waislam hatuna Waislam walio katika ‘indirect way’ ni aidha Muislam, Ahlul Kitab (mkristo, Myahudi) au Mpagani na Mshirikina.
 
Shule sio suala la imani, pia inategemea na umri wake, anaweza na anataka kufanya nini.
Kuna watu wengi sana hawajaenda shule na wana maisha mazuri sana kuliko hata wengi walio na PhD.
Siongelei mambo ya PHD Wala mambo ya masters. Nachojaribu kukizungumzia hapa ni swala la nidhamu na kuheshimu mzazi anasema nin na nin anataka ufanye ukiwa chini yake.
Ww hadi umefika hapo nyumbani kwenu umekuta kuna sheria na ulikua wazifuata lkn ulivoondoka nyumbani kwenu ukaanza maisha yako kama ww uliweka sheria zako kweny himaya yako.

Na ww kama mzazi uliweka sheria pia kwa watoto wako tofauti na hivo kinyume na hivo nyumba bila ya sheria ni uhuni.

Au nazungumza na mtu ambae bado anaish kwao pia?!
 
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.
 
Mimi niliishi nyumbani mpaka umri wa miaka 25 nipo home sikubaliani na din nilichofanya nikuwaonyesha wazazi utapel wa dini sasa wapo free.
 
Sijui hata altare inaelekea wapi kwanza nikiingia sala zote ni mpya kwangu wamemodify kila kitu, ukiingia kanisani unaonekana mshamba nyimbo wanazoimba wanakwaya hujui hata moja unaishia kua mpiga makofi tu na msikilizaji mwanzo mpaka mwisho, unakua km mhudhuliaji si mshiriki wa misa, km kwenye hukumu kuna swali la nilihudhulia misa/ibada ngapi duniani basi Mimi mtanikuta motoni
 
Nmesoma Sirat Rasul Allah ya Ibn Ishaq
Sunan Nassai
Al Tabari
Sahih Muslim
Muqqadimah
Ar-raheeq Al-Makhtum nk. Nk.
Baada ya kusoma wewe mwenyewe kitabu cha Seerah cha Imaam Muhammad ibn Is-haq, Sunan an-Nasaai cha Imam Abu Abdur Rahmaan Ahmad ibn Shu'ayb ibn 'Ali ibn Sinan an-Nasai, at-Tabari (Jami' al Bayan 'an Ta-wil al-Qur'an au Tarikh al Umam wal Muluk au kitabu gani?) vya Imaam Muhammad ibn Jarir at-Tabari, Sahih Muslim cha Imam Muslim ibn Hajjaj, Muqaddimah (Cha Ibn Khaldun?), ar-Raheequl Makhtum (the Sealed Nectar) cha Shaykh Safi ur Rahmaan Mubaarakpuri, nk nk... umefahamu chochote katika 'Aqidah ya Ahlus Sunnah na misingi ya Uislam, pamoja na misingi ya kielimu ee "Shaykha"?
 
Back
Top Bottom