Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Taboo lazima ihusiane na Dini,
Taboo inahusiana na miungu na ukishasema miungu moja Kwa moja unataja Dini.
Taboo ni miiko. Na miiko inahusianishwa na Imani Fulani Kwa miungu.

Embu nitajie Taboo yoyote unayoijua ambayo haiendani na Dini?
Vinginevyo hujui maana ya DINI
T
Nani alikudanganya Taboo lazima ihusiane na dini au miungu?? Hivi hizo definitoons unatolea dictionary gani?
Au wewe unaongelea taboo za kidini?
Kuna taboo nje ya dini.

Yani Taboo ni greater than dini itself.
Hata mkikubaliana wewe na washikaji zako ni marufuku mtu wenu kuwa shabiki wa yanga..hiyo inakuwa taboo kwenu.

Mfano wa taboo moja nimekupa hapo ya kukataza wanawake kula map*mbu ya ngombe/mbuzi hiyo inahusiana na dini gani??

Taboo nyingine rahisi hapa bongo ni kama taboo hairuhusiwi mwanamke kumtongoza mwanaume, ataonekana malaya.

Lakini haihusiani na dini, wala dini hazijakataza.
 
Dini hailazimishwi co ww simamia msimamo wako tu na ukiona imekuwa shida San tafuta mishe ambayo utakuwa unaenda had jumapili ili kuepusha mzozo na asilimia kubwà kanisan hawaruhusu simu co utajipa tabu ww simama na msimamo wako na ukienda kanisani kisa mtu hiyo dhambi tiyar fanya kile moyo wako unatak
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Malizana na wazazi wako huko huko, ikiwa hutaki kuamini waeleze hivyo, ikiwa unataka kuamini amini basi.
 
Nani alikudanganya Taboo lazima ihusiane na dini au miungu?? Hivi hizo definitoons unatolea dictionary gani?
Au wewe unaongelea taboo za kidini?
Kuna taboo nje ya dini.

Yani Taboo ni greater than dini itself.
Hata mkikubaliana wewe na washikaji zako ni marufuku mtu wenu kuwa shabiki wa yanga..hiyo inakuwa taboo kwenu.

Mfano wa taboo moja nimekupa hapo ya kukataza wanawake kula map*mbu ya ngombe/mbuzi hiyo inahusiana na dini gani??

Taboo nyingine rahisi hapa bongo ni kama taboo hairuhusiwi mwanamke kumtongoza mwanaume, ataonekana malaya.

Lakini haihusiani na dini, wala dini hazijakataza.

Kwa sehemu uko sahihi lakini Kwa sehemu pia haupo sahihi
Taboo mara nyingi ni kitu kilichokatazwa kidini na pia kijamii. Ni negative norms zilizokatazwa
Dini ni sehemu ya Social aspect.

Mimi kukubaliana na Wewe Jambo haiitwi Taboo,
 
Usahihi ni upi?
Wewe umepotoka kwa kutoamini katika MUNGU WA KWELI.

Mama yako naye amepotoka kwa kukulazimisha wewe kuabudu udanganyifu aliorithi kutoka kwa wazazi wake. Ni udanganyifu sababu kila kanisa linalo abudu siku ya Jumapili siyo kanisa la KWELI la MUNGU.

Hata kama mama yako angekuwa anaabudu katika kanisa la KWELI la MUNGU, bado hatakiwi kukulazimisha kuifwata njia yake.
MUNGU wa KWELI halazimishi watu kumwabudu, bali wamwabuduo humwabudu kwa hiari yao wenyewe, tena katika roho na KWELI.

Hivyo, utaona ni jinsi gani nyote wawili, wewe na mama yako mmepotoka.
 
Ukitaka kujua watanzania wengi ni wajinga soma hizi comment
 
Taboo lazima ihusiane na Dini,
Taboo inahusiana na miungu na ukishasema miungu moja Kwa moja unataja Dini.
Taboo ni miiko. Na miiko inahusianishwa na Imani Fulani Kwa miungu.

Embu nitajie Taboo yoyote unayoijua ambayo haiendani na Dini?
Vinginevyo hujui maana ya DINI
T
Dini ni zao la kutokuepo sheria za kumuongoza binadamu tangu bronze age, iron age,, so mbadala wa sheria kama za zama zetu, mababu walibuni miiko nA ndo ikazaa imani na kuabudu miungu
 
Okay sijajua uislam mkuu...it seems uislam ni very complicated subject..binadamu wa kawaida hawezi kuelewa kirahisi.

And if that's so, then kwann mungu aliucomplicate ili wachache waelewe?

Btw, huna jipya la kuniambia kuhusi uislam.

Ongezea tena fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakuwahi kukujua, hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
Woe unto each sinful liar,
Who heareth the revelations of Allah recited unto him, and then continueth in pride as though he heard them not. Give him tidings of a painful doom.
45:7-8
 
Dini ni zao la kutokuepo sheria za kumuongoza binadamu tangu bronze age, iron age,, so mbadala wa sheria kama za zama zetu, mababu walibuni miiko nA ndo ikazaa imani na kuabudu miungu

Unaweza kuwa Sawa.

Kwenye Norms kuna Aina kuu NNE.
1. Folkways
2. mores
3. Taboos
4. Laws
 
Kwenye biblie kuna amri ya kuheshimu wazazi na pia kuna maelekezo kwa mzazi kulea watoto wake katika Imani so mzazi wako yuko sahihi kuna siku utakuja kumshukuru ila kwa sasa endelea kushupaza shingo mpaka ikatike.
 
Kwa sehemu uko sahihi lakini Kwa sehemu pia haupo sahihi
Taboo mara nyingi ni kitu kilichokatazwa kidini na pia kijamii. Ni negative norms zilizokatazwa
Dini ni sehemu ya Social aspect.

Mimi kukubaliana na Wewe Jambo haiitwi Taboo,
Mkuu utamaduni ni somo paaana sana lenye aspects nyingi sana kama language,arts, rituals, norms, beleifs, customs, taboos, ethics nk. Nk.
Hapo religion ni aspect mojawapo tu ya utamaduni.
Tena ni aspect ndogo sana maana inafall ndani ya aspect ya beleifs, na imani zipo nyingi za kidini na zisizo za kidini.

Mfano hata hapa bongo kuna viimani vingi mfano jicho likicheza kuna mgeni au jambo fulani litatokea, mvua na jua kuna simba anazaa, ukioga baharini unaondoa gundu, watu wafupi wote ni wabishi nk. Nk.
ila sio imani za kidini.

So dini ni kakipengele kadogo sana kwenye swala la utamaduni.
Ambako ndani yake kuna taboos zake.

Lakini Taboos nje ya dini zipo nyingi kuliko hata hizo za ndani ya dini.
Mfano ni taboo kwa wamasai kula samaki, jamii nyingi ni taboo kula mbwa, ni taboo kubusu wazazi mdomoni, ni taboo kukiss hadharani nk. Nk.
Vyote hivi havihusiani na dini.

Kukubaliana na mtu sio taboo...ila pale mtakapo kubaliana kukataa kitu fulani na ikawa ndani ya utamaduni wenu wa maisha ya kawaida kuwa hairuhusiwi kufanya jambo fulani kwenye jamii basi hiyo by definition ni taboo.

Hata wewe nyumbani kwako ukisema hairuhusiwi mtu wa hapo kuvaa nguo nyeusi, itakuwa taboo ya nyumbani kwako.
 
Kwenye biblie kuna amri ya kuheshimu wazazi na pia kuna maelekezo kwa mzazi kulea watoto wake katika Imani so mzazi wako yuko sahihi kuna siku utakuja kumshukuru ila kwa sasa endelea kushupaza shingo mpaka ikatike.
Sasa mimi kumbuka siamini hiyo bible
 
Woe unto each sinful liar,
Who heareth the revelations of Allah recited unto him, and then continueth in pride as though he heard them not. Give him tidings of a painful doom.
45:7-8
Ongezea fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
 
Back
Top Bottom