Mzazi mwenzangu anadai ananipenda lakini nimegundua ana mwanaume mwingine

Mzazi mwenzangu anadai ananipenda lakini nimegundua ana mwanaume mwingine

Bàada ya kusoma maelezo yako nikushauri tafuta pesa kwanza halafu utafute mwanamke mwingine
Nikwambie kitu mkuu?

Sijui utakuwa na umri gani!

Mtu akikuomba ushauri uhusuo mahusiano, jikite kuongelea ama kushauri juu ya mada ile ile na namna ya kurekebisha dosari katika mahusiano hayo pekee.

Hayo mengine sijui ya kutafuta pesa na kujijenga ni mada tofauti na iliyoletwa jukwaani.

Halafu, watu wengi hupenda aridhi ipasuke iwameze ama kutamani kuficha sura zao kwa aibu itokanayo na ushauri mbovu wautoao wa kuvunja mahusiano ya wengine na baadaye kupuuzwa na mahusiano hayo kuendelezwa kibabe na wahusika!
 
Kimbia haraka Sana hapo si salama Tena kwako Mana hata Kama anakupenda anaweza kukusababishia magonjwa ya ngono(au ukimwi) hivyo chukua hatua mapema huyo ashakua mgawaji wa hiyo chakula yako chukua hatua mapema ibaki malezi ya mtoto tu
 
We jamaa humhurumii Yule mtoto Hawa wanaotelekeza vizazi vyao ndo wanao tuletea tabu na shida mitaani .AKALEEE MTOTO WAKE
ukwl namuwaza mtoto nakosa jibu sipend nitengane kwa ajil ya mtoto but inaumiza sana reality
 
Huyo mwalimu wa nursery anakupenda ila analipiwa kodi na kusaidiwa matumizi mengine na mwanaume aliyelazimisha kuja kuleta fujo. Anayependwa ni wewe na hili si kosa la kumuacha. Kwa vile yeye ana ajira na wewe huna basi ukikaa Tabora ukajitolea kule hupotezi mkataba, ila sio uhamie kwake
 
Nikwambie kitu mkuu?

Sijui utakuwa na umri gani!

Mtu akikuomba ushauri uhusuo mahusiano, jikite kuongelea ama kushauri juu ya mada ile ile na namna ya kurekebisha dosari katika mahusiano hayo pekee.

Hayo mengine sijui ya kutafuta pesa na kujijenga ni mada tofauti na iliyoletwa jukwaani.

Halafu, watu wengi hupenda aridhi ipasuke iwameze ama kutamani kuficha sura zao kwa aibu itokanayo na ushauri mbovu wautoao wa kuvunja mahusiano ya wengine na baadaye kupuuzwa na mahusiano hayo kuendelezwa kibabe na wahusika!
nashukuru ndugu kwa ushauri wako bora
 
Mkuu sielewi wapi nimetoka nje ya mada, mtoa mada kasema yupo musoma anajitolea hajaajiriwa sasa unazani kwanini kaandika hayo? Pili kwanini unaangalia alipoangukia na si alipojikwaa?

Hapo mzozo ni kipato tu ndio umesababisha dada kujiongeza, mapenzi yanaumiza mno na dada tayari ni muumizaji yanini kuendelea nae? Mwache jamaa akatafute pesa kwanza wewe huoni matangazo yote ya wadada humu kutafuta wachumba wanataka mtu anayeingiza kipato?
 
Pole sana ndugu,hapo tatizo ni umbali uliopo baina yenu,alishindwa kujizuia kihisia hatimaye akaanzisha uhusiano mpya usiokuwa rasmi hapo nadhani lengo lake lilikuwa ni kukidhi haja na matakwa ya mwili,hana nia nae na ndio tafsiri ya kutoa machozi kwako kujutia alichokifanya,mwamba shikilia tu.
 
Kumbe mko kwenye mahusiano tu na hujafunga ndoa naye?
Bado huyo siyo mkeo!
 
Ushafanywa jogoo la kuazima na si ajabu hata mtoto anaweza akawa kifaranga cha kuazima...

Tembea mbele haraka mno...dharau gani hizo za kufuli kushea funguo!!!
 
Hebu tupe namba ya mzazi mwenzako tumkanye asiwe na mahusiano na mwanamme mwingine
 
Habarini ndugu zangu polen na majukumu ya kila siku, nimekuja mbele yenu kama kijana mwenye shida ya kiushauri na mawazo ili nipanue akili na niwe na uwezo mkubwa wa kuchukus maamuzi sahihi kutokana na mawazo yenu na mawazo yangu kwa pamoja.

Mimi ni kijana na nipo kakika mahusiano ya na mwanamke kwa muda mrefu ambaye tumefanikiwa kuwa na mtoto mmoja ila katika mahusiano yetu hayo tumetenganishwa na umbali kias wa kila mmoja yupo katika mkoa tofaut na mwenzake mimi nipo musoma yeye yupo tabora kutokana na majukumu ya kutafuta riziki za kila siku kwa faida yetu sote.

Mzazi mwenzangu huyo ni mwalimu wa nursery school na anafundisha katika shule fulan iliyopo Tabora nimekuwa nikimuamini kwa muda na hasa baada ya kuzaa mwaka juiz niliamini kuwa sasa malengo na mawazo yetu yapo sawia katika kuendeleza familia na kwa malezi bora ya mtoto lakini cha kushangaza hivi karibun nilienda kumtembelea Tabora na nilimtaarifu kuwa nakuja na ninafikia kwake ila nitakaa siku mbili mpaka tatu alafu narudi kazini kwangu ambapo najitolea bado sijaajiriwa.

Ukweli nilipofika Tabora nilifikia kwake na nikalala siku ya kwanza lakiin ilipofika siku ya pili nimetoka zangu mizunguko jioni nikawa nimeketi naye mpaka mida ya sa mbili kasoro lilitokea tukio la kustaakabisha kiasi, kumbe mwenzangu anamwamaume mwingine ambaye anakujaga kulala mpaka pale na siku hiyo muda wa uck alimwambia anakuja kulala pale, mwenzangu akashindwa kuniambia ikabid akamwambie mama mwenye nyumba wake aje aniambie kuwa huyu mwezako ana mtu wake amemwambia anakuja japo kuwa anasema awali alimwambia kuwa mimi nina mtoto na nina mwanaume wangu lakini yulu mwanaume alikubali hivyo hivyo.

Cha ajabu siku hiyo alipoambiwa mimi nimekuja alisema anakuja hivyo hivyo na ataleta fujo ikanibidi mwenyebnyumba aniombe niondoke na mzazi mwenzangu tukalale pengine asije akaja akatukuta ikaleta fujo na aibu. Pia nami nikafanya kama nlivyoambiwa na nilipofika gesti na mzazi mwenzangu nikaongea nae mambo mengi na nikamuuliza kati ya mimi na yeye unampenda nani akasema wewe hapo.

Swali linakuja kama unanipenda mim unawezaje kumleta mwanaume mwenzangu unapolala kama hauna malengo nae akasema nisamehe tu huku akilia.

Ndugu zangu nimekuja mbele yenu ila muweze kunisaidia ushauri kutokana na uzoefu wenu katika mambo ya mahusiano.
Kila siku ni visa vya mapenzi. Narudia, hakuna mshauri wa mapenzi ya wawili zaidi ya wao wenyewe kuamua la kufanya.
 
Masikini pole, yani nawe ukaambiwa umpishe kidume mwenzio aje alale nawewe ukapisha?!!!.....
Huyu mwanamke akikuacha atajuta milele
 
Hii hali kweli unataka ushauri!!!! Katika 10 bora ya vilaza na wewe upo
 
Back
Top Bottom