Mzazi mwenzangu anadai ananipenda lakini nimegundua ana mwanaume mwingine

Bàada ya kusoma maelezo yako nikushauri tafuta pesa kwanza halafu utafute mwanamke mwingine
Nikwambie kitu mkuu?

Sijui utakuwa na umri gani!

Mtu akikuomba ushauri uhusuo mahusiano, jikite kuongelea ama kushauri juu ya mada ile ile na namna ya kurekebisha dosari katika mahusiano hayo pekee.

Hayo mengine sijui ya kutafuta pesa na kujijenga ni mada tofauti na iliyoletwa jukwaani.

Halafu, watu wengi hupenda aridhi ipasuke iwameze ama kutamani kuficha sura zao kwa aibu itokanayo na ushauri mbovu wautoao wa kuvunja mahusiano ya wengine na baadaye kupuuzwa na mahusiano hayo kuendelezwa kibabe na wahusika!
 
Kimbia haraka Sana hapo si salama Tena kwako Mana hata Kama anakupenda anaweza kukusababishia magonjwa ya ngono(au ukimwi) hivyo chukua hatua mapema huyo ashakua mgawaji wa hiyo chakula yako chukua hatua mapema ibaki malezi ya mtoto tu
 
We jamaa humhurumii Yule mtoto Hawa wanaotelekeza vizazi vyao ndo wanao tuletea tabu na shida mitaani .AKALEEE MTOTO WAKE
ukwl namuwaza mtoto nakosa jibu sipend nitengane kwa ajil ya mtoto but inaumiza sana reality
 
We jamaa humhurumii Yule mtoto Hawa wanaotelekeza vizazi vyao ndo wanao tuletea tabu na shida mitaani .AKALEEE MTOTO WAKE
ukwl namuwaza mtoto nakosa jibu sipend nitengane kwa ajil ya mtoto but inaumiza sana reality
 
Huyo mwalimu wa nursery anakupenda ila analipiwa kodi na kusaidiwa matumizi mengine na mwanaume aliyelazimisha kuja kuleta fujo. Anayependwa ni wewe na hili si kosa la kumuacha. Kwa vile yeye ana ajira na wewe huna basi ukikaa Tabora ukajitolea kule hupotezi mkataba, ila sio uhamie kwake
 
nashukuru ndugu kwa ushauri wako bora
 
Mkuu sielewi wapi nimetoka nje ya mada, mtoa mada kasema yupo musoma anajitolea hajaajiriwa sasa unazani kwanini kaandika hayo? Pili kwanini unaangalia alipoangukia na si alipojikwaa?

Hapo mzozo ni kipato tu ndio umesababisha dada kujiongeza, mapenzi yanaumiza mno na dada tayari ni muumizaji yanini kuendelea nae? Mwache jamaa akatafute pesa kwanza wewe huoni matangazo yote ya wadada humu kutafuta wachumba wanataka mtu anayeingiza kipato?
 
Pole sana ndugu,hapo tatizo ni umbali uliopo baina yenu,alishindwa kujizuia kihisia hatimaye akaanzisha uhusiano mpya usiokuwa rasmi hapo nadhani lengo lake lilikuwa ni kukidhi haja na matakwa ya mwili,hana nia nae na ndio tafsiri ya kutoa machozi kwako kujutia alichokifanya,mwamba shikilia tu.
 
Kumbe mko kwenye mahusiano tu na hujafunga ndoa naye?
Bado huyo siyo mkeo!
 
Ushafanywa jogoo la kuazima na si ajabu hata mtoto anaweza akawa kifaranga cha kuazima...

Tembea mbele haraka mno...dharau gani hizo za kufuli kushea funguo!!!
 
Hebu tupe namba ya mzazi mwenzako tumkanye asiwe na mahusiano na mwanamme mwingine
 
Kila siku ni visa vya mapenzi. Narudia, hakuna mshauri wa mapenzi ya wawili zaidi ya wao wenyewe kuamua la kufanya.
 
Masikini pole, yani nawe ukaambiwa umpishe kidume mwenzio aje alale nawewe ukapisha?!!!.....
Huyu mwanamke akikuacha atajuta milele
 
Hii hali kweli unataka ushauri!!!! Katika 10 bora ya vilaza na wewe upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…