Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Kwahiyo wauza chipsi na bodaboda unawaona kama ni vijana wasio na future? Masikini, waliokosa options?

Waajiriwa mna akili za namna gani ninyi watu?
Kuna degree ya kuchoma chips? Ulisoma miaka 7 ukaongeza 4 ukaongeza 2 ukaongeza tena 3/4 alafu unakuja kua mchoma Chips, wewe bichwa lako limejaa uvundo au si ungeacha kitambo uchome chips tu km uliona kuchoma chips ndio kazi unayoitaka ulienda Chuo kufanya nini?
 
Mkuu,kwa nini wafanye hizo kazi za boda boda au kuchoma chips?
-Muuza chips,mwenye kijiwe safi na kilichopo mazingira mazuri anaingiza sh ngapi?

-Muajiliwa,tuseme wa laki 5 kwa mwezi,na muuza chips anayelaza elfu 15 kwa siku,yupi bora?
Siku zote hizi kazi mnazoziona hazina maana,zimewaweka wengi mjini.

Unashauri waziache wakae makwao?
 
Mada hiz zinavuruga sana mwishoni mana hazijengi. Tatizo lililopo kwenye ajira hata kama Leo watu wote watapelekwa veta. Few years later ngoma itakaza.

Na tatizo hili Lina Kona nyingi sana kuziangalia. Mana hata Leo hii ukikutana na injinia kama comics pale Golden tulip au Amaria maana ni ileile.

Watu kufanya kazi ambazo hawajasomea... Hii inapelekea Kule wanakuwa casual na wanalipwa kidogo kuliko kiwango.
Ama kweli this argument is null.
 
Mkuu,kwa nini wafanye hizo kazi za boda boda au kuchoma chips?
-Muuza chips,mwenye kijiwe safi na kilichopo mazingira mazuri anaihiza sh ngapi?

-Muajiliwa,tuseme wa laki 5 kwa mwezi,na muuza chips anayelaza elfu 15 kwa siku,yupi bora?
Siku zote hizi kazi mnazoziona hazina maana,zimewaweka wengi mjini.

Unashauri waziache wakae makwao?
Hamjamuelewa mtoa mada nyie.
 
Inahuzunisha sana kuona kazi wafanyazo watoto waliosomeshwa kwa gharama wakiwa bodaboda na wachoma chips.

Mzazi kugharamia masomo ya mwanao ili aje kuwa mpambaniaji wa kazi hizo na za namna hiyo au kutokuja kuwa na future yoyote mtaani inaleta huzuni kwa mtoto mwenyewe hata kwa mzazi pia.

Wanasiasa hawafanyi ujinga huu kamwe wao na kizazi chao wanaandaliana future bora watoto wao. Hakuna mwanasiasa hata mmoja ataruhusu mwanae awe boda boda au mchoma chipsi wala kutanga tanga mtaani hovyo bila future yoyote ile.

Mzazi jukumu lako lisiishie kuzaa na kupeleka mtoto shule pekee bali muandalie na future bora mtoto wako.

[IMG alt="lukesam"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/275/275627.jpg?1500562796[/IMG]

lukesam

JF-Expert Member​

  • "Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.
Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".
Itakuwa wanawapeleka kusomea ujinga.

Ingieni madrassa mtie akili.
 
Maisha ni neno pana Sana swala la kusoma ni Jambo lingine na kufanikiwa katka maisha ni Jambo jingine .........bado maisha ya walio wengi wetu si madhuri tupambne tu MUNGU atafanya wepesi
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ambaye aliweza kuumba ulimwengu ambao kukata tamaa hakuwezekani, halafu akaumba ulimwengu ambao kukata tamaa kunawezekana, hiyo ni contradiction.

Unaelewa hilo?

Unaelewa kwamba unapoandika "chanzo cha binadamu wa kwanza kuwepo na hii dunia kuwepo ni kitu kikichoumbwa na Mungu" hii ni kauli ya kiimani ambayo hujaithibitisha?

Unazunguka pale pale tu.

Ni kama vike, wewe unadai baba yako mzazi ni James Bond 007.

Mimi nakwambia James Bond 007 si baba yako, ni muhusika wa hadithi ya kutungwa, hayupo. Kama unabisha, thibitisha kuwa James Bond 007 yupo kweli na ni baba yako mzazi.

Unanijibu James Bond 007 yupo kweli, kwa sababu chanzo chako ni huyo baba yako mzazi James Bond 007.

Nilitegemea labda ungenipa ushahidi, uthibitisho.

Hujatoa ushahidi wala uthibitisho kuwa Mungu yupo na ndiye chanzo cha ulimwengu, umekuja na kauli ya kiimani tu.
Dah!
 
Kuna degree ya kuchoma chips? Ulisoma miaka 7 ukaongeza 4 ukaongeza 2 ukaongeza tena 3/4 alafu unakuja kua mchoma Chips, wewe bichwa lako limejaa uvundo au si ungeacha kitambo uchome chips tu km uliona kuchoma chips ndio kazi unayoitaka ulienda Chuo kufanya nini?
Ama kweli bongo nyoso, kwahiyo ulisoma kupata maarifa kutatua changamoto huko ulipo au ulisoma ili ukale kiyoyozi maghorofa ya posta??

Sio kila degree ni kwa ajili ya kuajiriwa kijana, au umetoka chuo mwezi wa 7 mwaka huu??

Kuna watu wengi washachoma vyeti, hawana time na kuajiriwa tena, wamejiajiri na wanapiga pesa kuliko hata hao waajiriwa.

Na kama akili za wasomi wetu ndo hizi zinategemea kuajiriwa tu tutafika kwelii??
 
Sio mfumo wa dunia, sema ni mifumo mibovu ya Afrika na nchi nyinginezo za third world.

First world countries ukisoma na ku pass vizuri huwezi kukosa kazi uishie eti kufanya manual Works

Ni Africa, middle east countries na latin countries tu, Nchi za third world countries ndio kuna wasomi wanao kosa kazi.
Hahahahhahah.... hunidanganyi. Nazijua hizo nchi vizuri sana.
Tena Tz inaafadhali kushinda nchi nyingi duniani kwa kuwa hatujakumbatia sana ubepari usio na mipaka.

Unajua hali ilivyo Europe na North America? Do you know why they feel trapped? Do you know why they're almost suffocating? Kwanini wanalalamika the rich get richer and the poor get poorer?

Nchi pekee iliyosalimika na hili janga la neo-liberalism ni China kwa sababu wanaviwanda. Na wasipokuwa makini litawapata.

Hizo sera mbovu unazodai za third world countries ziliwekwa na nani? Sio USA na goons wake? Are you one of those goons?
 
Inahuzunisha sana kuona kazi wafanyazo watoto waliosomeshwa kwa gharama wakiwa bodaboda na wachoma chips.

Mzazi kugharamia masomo ya mwanao ili aje kuwa mpambaniaji wa kazi hizo na za namna hiyo au kutokuja kuwa na future yoyote mtaani inaleta huzuni kwa mtoto mwenyewe hata kwa mzazi pia.

Wanasiasa hawafanyi ujinga huu kamwe wao na kizazi chao wanaandaliana future bora watoto wao. Hakuna mwanasiasa hata mmoja ataruhusu mwanae awe boda boda au mchoma chipsi wala kutanga tanga mtaani hovyo bila future yoyote ile.

Mzazi jukumu lako lisiishie kuzaa na kupeleka mtoto shule pekee bali muandalie na future bora mtoto wako.

[IMG alt="lukesam"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/275/275627.jpg?1500562796[/IMG]

lukesam

JF-Expert Member​

  • "Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.
Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".
Tupunguze kuzaa ovyo ovyo umetaka watoto wengi kuliko uwezo wako kulea. Kwa ulicho andika hapa ulitakiwa uwe na watoto maximum wawili. Ukiwa na watoto wachache na ukawa nao karibu, ni asilimia ndogo sana watafeli maisha hapo baadae.
 
Wewe na wewe akili zako hazina akili, ulisoma Chuo uwe mchoma Chips si ungeacha kitambo uchome chips ukishindwa nini?
Mkuu,

Pengine mchoma chipsi msomi anaweza kuchoma chipsi kwa mafuta ya good cholesterol na environmentally friendly energy tukapata chipsi za kisomi ambazo ni bora kwa afya na mazingira.

Au?
 
Kuna watu wengi washachoma vyeti, hawana time na kuajiriwa tena, wamejiajiri na wanapiga pesa kuliko hata hao waajiriwa.

Na kama akili za wasomi wetu ndo hizi zinategemea kuajiriwa tu tutafika kwelii??
Akili matope km ingekua rahisi hivyo si wote wangekua hawahangaiki kwenye 10 ni 1 hivi unaona hilo gap na hio 1 nyuma kuna nguvu ya mtu fulani inampa support bila hivyo hafiki popote unanielewa sijui au bado mpaka upigwe kidole ndio uelewe?
 
Mkuu,

Pengine mchoma chipsi msomi anaweza kuchoma chipsi kwa mafuta ya good cholesterol na environmentally friendly energy tukapata chipsi za kisomi ambazo ni bora kwa afya na mazingira.

Au?
Kwa hio unataka kusemaje? Wasomi wote wawe wachoma Chips?
 
Accessibility
Muajiriwa anauelipwa hio 700K anaweza kumiliki vibanda km hivyo zaidi ya vitano ila wewe mzee mchoma chips sio rahisi kuwa Muajiriwa wa mshahara wa 700K

Reputation
Muajiriwa wa 700K muda wote msafi rahisi kuji Address kwa watu na kutambulisha always he/she is presentable na anaheshimika ila wewe mchoma chips huna yote haya.

Workdone
Muajiriwa wa 700K anaingia kazini morning na kutoka saa 8 na pia jumamosi na jumapili harndi job, ila wewe mchoma chips unafungua morning hadi saa 4 usiku na huna weekend....Pia Muajiriwa anafanya soft works most of time ana relax job ila mchoma chips uamke 11 uende sokoni kubeba gunia za viazi, mkaa nk ukate gunia la viazi, ukaange siku mzima jikoni "nataka rojorojo" "nataka kavu ikaushe" this is hell.

Risk And Security
Muajiriwa wa 700K hata uumwe mwezi mzima still you receive your pay, wewe ukiumwa siku moja tu kazi unayo, Muajiriwa ana mafao zaidi ya 60 Millioni baada ya kazi wewe huna chako nk

This life is full of uncertainty ukiwa na Ajira ya 700K kwa asilimia kadhaa financial uncertainty zitapungua kwako ila mchoma chips Mungu ajaalie kwakweli.

Financial Credit
Mfanyakazi wa 700K anaweza kopa zaifi ya 20 Million ajafanya most potential move, ila mchoma chips hata 100K mtu kukukopesha mtiti.

Ni vizuri pia kujifariji kwasababu hakuna namna na haya maisha.
Rudi shule ndg bado elimu yako haijakukomboa na haina faida kwa jamii yako! Kama wote mtaajiriwa je ni nani atakae mhudumia mwenzie,
Elimu uliyoipata shule inatakiwa ikusaidie kutatua changamoto za jamii yako ikiwa ni pamoja na suala la kutengeneza ajira kwa wengine na siyo kutegemea kuajiriwa na serekali,
 
Mimi sisemi vibaya wanaojiriwa na wala siwashushi heshima. Dunia ina watu wengi walioajiriwa. Hata mimi nimewahi kuajiriwa sehemu tofauti na industry tofauti.
Hoja yangu na yako ziko tofauti.
Kuhusu kuchafuka hii ni hoja nyepesi. Hata hapo panapochomwa chipsi ukienda mimi hunikuti.
Kama hoja ni kuwa mwenye mshahara wa laki 7 anaweza kumiliki vibanda 10 vya chipsi.....mimi nafeli wapi? Yeye ana vimiliki vipi na anafanya kazi from 8-5?
Ana free time ya kufanya ukaguzi?
Mind you, uhakika wa ajira na kipato ni serikalini tu. Private nyingi sana hazina uhakika wa kazi. Mikataba ya mwaka hadi mwakana hakuna fringe benefit ya maana. Una mkataba wa mwaka, unakopa wapi mil 20?
Kuna bank moja hapa Tanzania mfanyakazi hawezi kukopa pesa zaidi ya mkopo wa gari, salary advance ambayo maximum ni 4 times your salary au mortgage.
Sasa niambie mil 20 unakopaje hapo kwa mshahara wa laki 7?
Ngoja nikupe kidogo kuhusu mimi:-
1. Nina duka la furniture nimeshare na bro tumeweka partnership kisheria kabisa
2. Mimi binafsi nina stationery
3. Nina banda la chipsi
4. Nna share 50% kwenye kikampuni kidogo cha microfinance.
3. Hapa nafikiria kuanzisha PRINTING SERVICES business nifanye printing ya nguo, embroidery, vikombe, bahasha, vitabu, large format printing etc. Ntaisajili kama kampuni.
Lakini msingi wa vyote hivi ni ajira zangu zilizopita.
Kama unamwandaa mtoto mwandae aje apambane katika sekta zote. Unaonaje ukawa na biashara na ukamwajiri mwanao humo?
Tusifikirie tu status, kupendeza, assurance ya kipato, kazi soft soft.....n.k
Uncertainty zipo kila mahali.

Profits are sweeter than salaries.
Umenena vyema ndg, tatizo la hawa vijana wa sasa wanataka waonekane wako smart huku mfukoni hawana kitu zaidi ya kutegemea mwisho wa mwezi, huo ni ujinga yaani mtu anajiita msomi lakini anashindwa kuitumia elimu yake kutatua matatizo yanayomkabili,
Ukiwa hujawahi lala njaa hakika huwezi fahamu maumivu anayopata yule anaelala njaa!
 
Shida Iko wapi? Kampuni uza kitimoto ikikua kubwa ndio utakuwa HR

Hata bila kampuni kukua mfano umefungua sehemu ya kitimoto wewe ndie bosi umeajiri watu wawili mmoja jikoni na mwingine mhudumu skill zako za HR si unatakiwa uzitumie? Au hukuelewa ulichosoma kazi za HR anatakiwa atumie wapi?
Usiandike just kuandika jamas HR applied kwenye reputable institution tu inayoweza kuwa na demand na supply ya human resources ufungue banda la chips uajiri mchoma chips na mmenya viazi then useme HR applied
 
Back
Top Bottom