Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu

Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu

Ila kusema ukweli kama huyu mzee ana huruma na Watanzania, basi hiyo miaka yake 10 inamtosha sana. Akiongeza mingine isiyo na kikomo, basi tutarajie kuona baadhi ya Watanzania wakiikimbia nchi kwa kasi ya ajabu.

Huenda yale ya wahamiaji kutoka Ethiopia, yakahamia kwetu. Hii ni kutokana na serikali yake kutumia nguvu nyingi kwenye miundombinu, huku maeneo mengine yanayo gusa maisha ya watanzania moja kwa moja mfano ajira kwa vijana, mzunguko wa fedha mtaani, nk. Yakiendelea kupuuzwa.
Mimi nimeanza kuhamisha baadhi ya biashara zangu Kenya, Comoro na Ushelisheli. Akiongeza zaidi,ntahamisha na familia yote.
 
"wako mfukoni"?
Kamwe siamini kwamba mtu kama mzee Butiku "yuko mfukoni". Kutakuwepo na neno/maneno bora zaidi ya kuielezea hali ya wengi walio kama Butiku, bila ya "kuwekwa mfukoni."
Mkuu pengine Butiku alizungumza mengi zaidi ila mleta mada akaamua kuleta machache tu? Ningekuwa nimesikiliza yote aliyosema ingekuwa vizuri zaidi. All in all dalili zinaonyesha kuna-calculated move ya kuondoa ukomo wa urais au kuongeza ile muda kutoka miaka 5 kwenda 7. Magufuli amesikika mara kadhaa akisema hana huo mpango lakini ninavyomjua angekuwa hataki ungekuta huo mjadala umeshafungwa siku nyingi. Mbona corona hakuna anayethubutu kuitaja hata jina tu wakati ipo? Hata uchaguzi uliporwa naona ni maandalizi ya kubadili katiba. Kelele zinazopigwa sasa hivi ukizisikiliza kwa sikio la tatu zinaashia motive mbaya sana.
 
Hahahaaaaaaa.
Wewe unapenda aendelee au atoe nafasi kwa Watanzania wengine!?
Mimi ni mjumbe na unazijua tabia zetu wajumbe😅😅😅 taratibu zifuatwe mwisho wa siku idadi ya kura zitaamua
 
Mkate ukiuweka kwenye chai,lazima ulainike.
Wazee kama Butiku, Warioba siyo mikate tena ni 'mabumunda magumu' yanayojua nchi hii ipo na inaelekea katika hali gani..
Mkuu pengine Butiku alizungumza mengi zaidi ila mleta mada akaamua kuleta machache tu? Ningekuwa nimesikiliza yote aliyosema ingekuwa vizuri zaidi. All in all dalili zinaonyesha kuna-calculated move ya kuondoa ukomo wa urais au kuongeza ile muda kutoka miaka 5 kwenda 7. Magufuli amesikika mara kadhaa akisema hana huo mpango lakini ninavyomjua angekuwa hataki ungekuta huo mjadala umeshafungwa siku nyingi. Mbona corona hakuna anayethubutu kuitaja hata jina tu wakati ipo? Hata uchaguzi uliporwa naona ni maandalizi ya kubadili katiba. Kelele zinazopigwa sasa hivi ukizisikiliza kwa sikio la tatu zinaashia motive mbaya sana.
Kwa mtu mwenye upeo wa kati hili la kubadilisha katiba na kumuongezea muda raisi ni rahisi kuling'amua.
 
Hawa wazee wameishi mno na sasa hawana faida kwa nchi hii, ona walivyo na mawazo ya kijinga sasa huyo wakimbadilishia katiba yeye halafu afe ndio inakuwaje wanabadilisha tena katiba kurejesha mihula.?

Watanzania tuache kuonyesha tulivyo wapumbavu, hakuna mtu au binadamu bora kuliko wengine kila mmoja anaweza akafaa akipewa fursa.

Hata akina Idi Amin, Jean Bedel Bokassa, Macius Nguema, Muammar Gaddafi, Mobutu Seseseko nao walikuwa ni marais wa maisha kipindi fulani.

Tuache ku-treat binadamu wenzetu kama miungu watu. Akina Butiku wanaongea kijinga hivyo wakijua wao hawana cha kupoteza kwani hawana siku hapa duniani.
 
Watu wameshakata tamaa, afanye vyovyote atakavyo.
 
Hata hivyo ukiachana na precedent ya marais wa huko nyuma kuondoka madarakani, hakuna kitu kingine cha kumzuia.

Watanzania washapigika kikamilifu, njaa na kukata tamaa. Tayari wako KIBRA.

Wanaishi kwa matumaini tu.

Ni yeye tu aamue kubaki au kustaafu, hakuna wa kusema chochote wala kumzuia.

Kama ni katiba anaivuruga kila siku.( Angalia suala la Wabunge wa CHADEMA maarufu kama COVID-19 ).

Kwasasa ana uwezo wa KUFANYA CHOCHOTE wakati WOWOTE.
umemaliza
 
Hili jambo siku nyingi nilikuwa nahisi linakuja, marekibisho ya katiba yanakuja wa kuzuia hakuna hilo tukubali. Mzee siku hizi anatajwa kuliko chama, kwa maana amekuwa mkubwa kuliko chama. Jana kuna kauli moja ya mbunge alisema sisi sote hapa tumeingia bungeni kwa fadhila ya Magufuli tumetumia kupendwa kwake kupata kura nyingi, sio fadhila za CCM au sera nzuri ila Magufuli. Kauli watu hawakuichukulia lakini kwangu niliona ina uzito ndiko tunakoelekea. Kama hatuwezi kumzuia kuendelea basi tunaomba tu asitupeleke hivi anavyotupeleka tunaonekana wajinga nje na baya nalo ogopa kuja kutengwa na wenzetu wengi Africa na dunia kwa ujumla kwa namna tunavyo endesha siasa za nje. Katiba inarekebishwa, Miaka 7 saba na inaanza upya 2025 na tunaanza upya kwa hiyo mzee atapiga 5+7+7 hapo atakuwa almost 75 years hii inaitwa tactic 5-7-7 mashambulizi tu
 
System ya German ni nzuri ila ukiwa na watu wana akili sana katika chama na bunge ndio maana kwao unaweza kuwa kiongozi mwaka tu au hata miezi ukiharibu tu chama wanakutoa na uongozi unapoteza sio kwamba unachaguliwa wewe kwamba lazima umalize muda wako hata kama kichaa, hapana chama kinakupa uongozi hupigiwi kura wewe ni chama kama UK ukiingia tu halafu waone unawapeleka sivyo miezi tu wanakutoa. Huku kwetu ukichaguliwa imetoka mzima, kichaa watu wanaenda na mdundo tu akipiga bongo fleva watu wanacheza akienda singeli wanacheza....
 
Back
Top Bottom