Kujiweka pembeni au kujitoa ktk siasa bila kuelezea kwa kina tofauti ya imani yake ya kiitikadi na CHADEMA ni ishara tosha Mzee Fredrick Sumaye alikuwa CHADEMA bila ya kuwa mpinzani wa kisiasa wa kweli wa CCM.
Visingizio vingi sana kwa hawa wazee kama Fredrick Sumaye, Prof. Abdallah Safari na Edward Lowassa, ukweli mikiki mikiki ya kisiasa hawaiwezi. Hoja ya kuhofia usalama wake ni muflisi.
Wote tunajua kuwa Mwenyekiti wa chama kitaifa wa chama kikuu cha upinzani siyo ngoma ya lelemama, nawapongeza wana Kanda ya Pwani ya CHADEMA mlivyomfanyia vetting Mzee huyu kuwa hafai hata kuongoza kanda.
Hapa Mzee Fredrick Sumaye alikuwa anasubiria kisingizio chochote ili ajitoe katika 'siasa' ili kulinda mali zake kama mashamba n.k yaliyokabiliana na mbinyo na michezo michafu ya siasa za CCM.
Nitakuwa wa mwisho kuamini waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Fredrick Sumaye anahofia 'usalama' wa maisha yake wakati dola inatoa ulinzi kwake popote alipo masaa 24, posho, matibabu, usafiri, safari, makazi na marupurupu kuitunza familia yake pia inatolewa na serikali yoyote iliyopo madarakani kama inavyoainishwa na kutamkwa katika katiba ya nchi kuhusu wastaafu wa ngazi yake.