Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Hapana Sumaye kaonewa .Kamati kuu ya chadema ilimwona anafaa na ndie alikuwa mgombea pekee.Kulikuwa na sababu gani ya kuitisha kura Tena?
Hahaha aliyemuonea nani tena?!
Kamati kuu walimpitisha kama mgombea wa nafasi ya uwenyekiti kanda ya pwani, yeye alidhani aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kanda ya pwani.

Baada ya kupitishwa kugombea ukiwa na wenzako mliopitishwa mnajieleza mbele ya wajumbe kisha mnapigiwa kura.

Kwa bahati akawa mgombea pekee, akadhani kuna kupita bila kupingwa, aliisha sahau kuna kupigiwa kura. Kura zilipopigwa akapata nyingi za HAPANA za ndiyo chache, akawa kashindwa.

Unajua alipoteuliwa kuwa waziri mkuu Mata mbili alipigwa kura za ndiyo nyingi akashinda mara mbili.

Sasa kapata nyingi za HAPANA, uonevu uko wapi?! Alipaswa arudi tena kushindana mara ya pili, mara hii huwezi jua labda angempata mshindani na wangeshindana na angeshinda,lakini kuweka mpira kwanani kakimbia.

Kaonewa vipi, na aliujua mchakato wote wa CHADEMA au alitaka ateuliwe tu?.
 
Nitaifufua hii comment after 2020 election. Chadema wameshindwa kujipanga kuwa contain hao wanaowaona wanataka kumpindua Mbowe, unfortunately wana nguvu ya either "kugawana mbao" au ku opt kwenda ACT.

Zitto mpaka sasa is playing smart kuliko Mbowe! Good enough hata Lissu ataiacha Chadema kwasababu zile zile alipoitema NCCR! NCCR ilipo ndio inapoelekea Chadema!

Mkuu naomba nikuulize swali dogo tu? Tangu lini umekuwa msemaji wa Tundu Lissu?
 
Hapo ndio aamini kwamba hakuna mwanasiasa anayekupenda hata mmoja kila mtu yupo kwenye chama kwa maslahi yake lakini sisi wananchi ni wagumu kuelewa
 
Ramark, Wenye akili tu ndiyo wanaweza kuelewa lkn mambumbumbu yataendelea kuburuzwa kwasbb imepumbazika...wote mnaomtetea Mbowe hamna akili timamu

Unaonyesha kujawa na jazba,hii pekee ni kipimo tosha cha uwezo wako mdogo wa kujenga hoja!
 
Nimefuatilia kwa makini sana hoja za Mzee Sumaye. Ninachoweza kusema Sumaye ni mzee kwa umri lakini kisiasa ni mtoto sana.
 
Hahaha Roma mkatoriki alitabiri haya
Sumaye chadema wamambeba mwisho wamempiga chini aamini
"Wanakubeba na autaamini siku wakikupiga chini".
Hapa umeenda OP babu kunasibisha kipande hicho na tukio la Sumaye
 
Laana ya Mzee slaa haiwezi kumwacha Mwenyekiti salama.
Dr. Slaa aliondoka na Dhima na Dira ya Chama.

Kwa waliobaki hawajui hata wanaelekea wapi wala wanataka nini.

Kilichobaki ni kuunganisha kabila la mwenye chama,na walio baki huko ni bendera fuata upepo.
Historia inaonyesha kabila hilo linajitambua Sana na limekua likijitenga kutafuta namna ya kujitawala,

enzi za kupigania uhuru, kabila hilo Lili omba Uhuru wa eneo lake pekee, Kwa bahati akatokea Mwalimu julias akaomba Uhuru wa nchi nzima, wenye Uhuru wetu wakaona Mwalimu alikua na mantiki zaidi, tukapata Uhuru wa nchi nzima.

Wakati wa utawala wa Mwalimu kabila Hilo liliendesha mapinduzi mara mbili jeshini na wakabainika na kushughulikiwa barabara.

Maneno ya prof Safari ni ya msingi Sana sema ni wachache wataelewa, laiti yangeeleweka, basi Mwenyekitiangeachia nafasi hiyo.na kumuomba Dr.slaa,Zito, na wazee hawa sumaye na lowasa bila kumsahau lisu wakusaidie kukifanye kiwe chama cha kitaifa

bila hivo nakuhakikishia Kwa kuunga mkono maneno ya Mzee Safari kua kamwe hamuwezi toboa kwani historia haidanganyi.
 
Wewe akili zako zinakuambia CCM inaendelea kutawala kwa vile Mbowe ni mwenyekiti?
Kama akili inakutuma hivyo, basi nenda Muhimbili kafanyiwe scan pengine ubongo umehamia utumbo mpana na hapo kwenye fuvu kuna furushi toka utumbo mpana
Siyo hivyo! Tunasema itatawala milele sababu tunaotegemea wawe mbadala hawatofautiani na ccm.

Fikiri nje ya box
 
Wewe akili zako zinakuambia CCM inaendelea kutawala kwa vile Mbowe ni mwenyekiti?
Kama akili inakutuma hivyo, basi nenda Muhimbili kafanyiwe scan pengine ubongo umehamia utumbo mpana na hapo kwenye fuvu kuna furushi toka utumbo mpana
Na mazuzu kama nyie ndio mnafanya Mbowe aendelee kujitafunia tu ruzuku bila kipingamizi!

Huo umugabe na umuseven wake ndio unafanya hapo chadema wote muendelee kuonekana ni wahuni na sio taasisi inayojiandaa kuongoza nchi.
 
Ulafi wa madaraka
Alitegesha ndoana
Kusema kweli aende tu hakuna alilolifanya kwa upinzani alijitegesha tu
Upinzani mjifunze sasa hawa walikuwa makapi mliwapokea bila kutambua nia yao.
Sumaye huna tofauti na mmasai
Leeni wajukuuu msisumbue watu bana
Huyo Mbowe wenu anawapoteza sana
 
Ila alichofanyiwa CHADEMA hakikuwa sahihi, pamoja na madhaifu yake kama alikuwa hatakiwi aenge elezwa tuu na si kudhalilishwa namna ile, ni kweli CDM tuna hasira kweli kweli na 'dola' lakini haikuwa sahihi kumbwagia hasira zetu Sumaye.
demokrasia ilishika hatamu
 
Alianza Chacha wangwe yakamkuta, alikuja Arfi yakamkuta, akaja zitto yakamkuta... Na sumaye Naye yamemkuta . Pale CHADEMA cheza na yoyote yule Ila sio mbowe. Mbowe CHADEMA sio chama Cha siasa tu Ila pia Ni biashara tena ya kifamilia. Tuseme ukweli hata Kama unakera
 
Back
Top Bottom