Hahaha aliyemuonea nani tena?!Hapana Sumaye kaonewa .Kamati kuu ya chadema ilimwona anafaa na ndie alikuwa mgombea pekee.Kulikuwa na sababu gani ya kuitisha kura Tena?
Kamati kuu walimpitisha kama mgombea wa nafasi ya uwenyekiti kanda ya pwani, yeye alidhani aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kanda ya pwani.
Baada ya kupitishwa kugombea ukiwa na wenzako mliopitishwa mnajieleza mbele ya wajumbe kisha mnapigiwa kura.
Kwa bahati akawa mgombea pekee, akadhani kuna kupita bila kupingwa, aliisha sahau kuna kupigiwa kura. Kura zilipopigwa akapata nyingi za HAPANA za ndiyo chache, akawa kashindwa.
Unajua alipoteuliwa kuwa waziri mkuu Mata mbili alipigwa kura za ndiyo nyingi akashinda mara mbili.
Sasa kapata nyingi za HAPANA, uonevu uko wapi?! Alipaswa arudi tena kushindana mara ya pili, mara hii huwezi jua labda angempata mshindani na wangeshindana na angeshinda,lakini kuweka mpira kwanani kakimbia.
Kaonewa vipi, na aliujua mchakato wote wa CHADEMA au alitaka ateuliwe tu?.