"Watu hawana wasiwasi, hawana wasiwasi kwamba nitakuwa salama au itakuwa salama, nitarudi nyumbani au sitarudi nyumbani. Kuna vipindi hivyo vilikuwa na mashaka. Mazingira yale hayapo. Kuna wakati mazingira hayo yakiwepo kwa kiingereza wanasema people just take it for granted. Hata wafanyabiashara leo wakigongewa mlango hawana wasiwasi kwamba baada ya kufungua mlango kutakuwa na watu kama 10 hivi, mmoja atauliza hiki na mwingine atauliza kile. Wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa utulivu. Hili ni jambo kubwa sana. Kwenye mazingira ambayo ndani ya nchi kuna utulivu ndio mazingira yanachochea ukuaji wa uchumi, mazingira ya leo hapa hayamfanyi mtu kufikiria kuhamisha mtaji wake, shughuli zake au kutafuta nchi ya kwenda, hayo ni mambo makubwa yanayopambanua Urais wa @SuluhuSamia" Dkt. @jmkikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tumpe mama samia maua yake. Sijajua Jakaya alikua anamzungumzia nani lakini kusema za ukweli haya aliyoyasema kwa sasa yametulia sana.