Mzee Kikwete: Wanaolalamikia kupanda kwa bidhaa ni unafiki mkubwa

Viongozi wa Tanzania wana akili za kuona mbali tangu lini!
Wao wanachowaza ni uchaguzi na uwizi wa Mali za Umma,basi!
 
Huyo jamaa ni Pimbi kwani huyo Msoga huwa anatugawia hela za matumizi kila siku?
Kwanza ni fisadi tu na hana msaada wowote kwa wananchi wa kawaida!
 
Uingereza imetumia £400 billion cash kupunguza gharama za maisha kwa miaka miwili; hiyo imeenda kwenye nyonyo kuwaongezea kipato watu wanaopata msaada wa serikali, kila nyumba imepata £67 kusaidia kwenye bill ya gas toka mwaka jana mwezi wa 10 na itadumu kwa miezi sita na Kuna marupurupu kibao kwa wanao jua kuyapata.

Serikali iliweka zuio la ‘price freeze’ ya bei ya nishati kupanda kipindi cha baridi, huo mpango unaisha mwezi ujao lakini serikali itaendelea kuangalia subject to market price bei ya nishati kama stable serikali itaendelea kuzuia.

Upande wa biashara serikali imeruhusu kitu kinaitwa ‘super deduction’ ambayo uwekezaji ambao ‘wenye wanaita wholly and exclusively’ kwa sababu ya biashara vitu kama mashine za viwandani, ma lorry, vans, computer and softwares, fixtures and fitting, green technology yoyote unayoweka ofisini; unaruhusiwa ku claim 130% bila ya kujali kiwango cha hela ulicho wekeza.

Maana yake nini kama ulinunua mashine millioni 200 mwisho wa mwaka kwenye hesabu zako unaruhusiwa kum claim back million 260 kabla ya kodi. Kama hakuna faida umepata hasara una claim losses mpaka miaka mitatu nyuma unapewa tax rebate, kama hiyo miaka aijafidia losses zako; kilichobaki unaenda nacho mbele mpaka umalize loss zako zote.

Hapo kuna annual investment allowance ya £1,000,000 ukinunua vitu hivyo hivyo ila second na vingine. Kwa kifupi hiki kipindi wamefanya mambo mengi sana ya kusaidia watu maskini kupambana na ugumu wa maisha na biashara ili bei za bidhaa zisipande sana kuna incentive luluki sijaziongelea.

Bila ya hivyo sijui ingekuwaje kitaa, maana pamoja na ivyo maandamano na migomo kila uchao mpaka sasa hivi serikali imeanza kukubali hizo demands. Na budget inayokuja washatangaza kutakuwa na £300 billion kusaidia kwenye mambo hayo hayo ya ugumu wa maisha.

Yeye JK ata akienda U.K. anafikia kwenye nyumba aliyomnunulia binti yake, maeneo ya matajiri, ukiingia ndani ya gate nyumba bado ipo mbali; sasa ata anajua changamoto za kitaa kupanda kwa bei za maisha U.K.

Sasa Tanzania kwenye ugumu wa maisha serikali hapo hapo inatunga na tozo za kuibia watu hela zao; tozo za Mwigulu sio kodi ule ni wizi wa kuchukua hela za watu kinguvu.
 
Tanzania hii bila kutoka kwenye mikono ya lile kundi la majizi hakuna la maana litafanyika hata wanaopiga kelele saizi ni wale wezi na watu wa magumashi ila mtu wa kawaida maisha ni magumu sana!
Jiulize mfano chakula waliruhusu chakula kitoke kwa kuacha mipaka wazi! Juzi tena hao hao wakaagiza chakula kutoka nje!
Lakini ukimsikiliza Bashe anaongea asichokijua maana kalishwa asali na wafanya biashara ili aruhusu chakula kutoka nje shagarabagara!
Na mwaka huu mazao sio mazuri kazi ipo!
 
Kiukweli hii habari inafaa ihakikiwe Kikwete kasema kweli, wapi, vipi, kwa muktadha gani?

Kama kuna audio au video itapendeza zaidi.
 
Kibaya zaidi hawana huruma.

Sasa unatafuta nafasi za uongozi kwa nini wakati uguswi na shida zinazowakabili watu maskini.

Huyo mama ndio ajali kabisa, afadhali ata ya huyo JK.
 
Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa! Hivi tayari ameishajengewa nyumba na serikali au bado?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…