Mzee Kikwete: Wanaolalamikia kupanda kwa bidhaa ni unafiki mkubwa

Mzee Kikwete: Wanaolalamikia kupanda kwa bidhaa ni unafiki mkubwa

MZEE AJIHESHIMU, asitulazimishe tukamvunjia heshima. Yeye anakula na kusaza, atambue hali hiyo sio kwa wananchi wote
 
JK bwana! Aliwahi kuulizwa kwanini Tz ni masikini akajibu hajui!

Sidhani kama anaweza kuelewa hali halisi ya Mtanzania wa Hali ya chini
 
Kinamuwasha kitu gani mtawala kukosolewa? Kani yeye ndio rais kwa sasa anajitokeza kufokea wananchi wanaolalamika?

Huyu anatakiwa akae kimya kabisa asije akapandisha hasira za wananchi bure na akaathirika kwa matendo yao.

Sukuma gang katika ubora wako
 
Rais huyu tuliye naye sasa hana majibu yoyote kwa matatizo yetu. Rais huyu walifika wale viongozi wa dunia intellectuals kuongea naye,wanachagua maneno mepesi ili aelewe.
Nchi haina mwelekeo,haina nidhamu ya kazi. But that is about to change.
Hakuna Rais anaeweza kukutatulia matatizo lako binafsi.

Kwa maandiko yako tu unaonesha una matatizo binafsi lukuki.
 
Hakuna Rais anaeweza kukutatulia matatizo lako binafsi.

Kwa maandiko yako tu unaonesha una matatizo binafsi lukuki.
Faiza Foxy umewaona wale watoto undernourished ghetto? Wale watu watajiinua kwa kamba zao za viatu? Are you a true socialist?
 

Mstaafu Jakaya Kikwete ameingilia kati mjadala wa kupanda kwa gharama za maisha kunakolalamikiwa na wananchi wengi na hii ni moja ya nukuu yake kupitia clip moja hivi inayosambaa sana kwenye mitandao.

'Bei imepanda sasa mtu ndio wanatunga na nyimbo, mafuta yamepanda bei ni unafiki mkubwa kwa kweli

'..eeeh unajua wakati mwingine offcourse ndio unasema adui yako muombee njaa wale wasiombea heri Serikali wanadhani lakini wakati mwingine ni lazima wawe wakweli tu haya mazingira wangekuwa wao ndio wako kwenye uongozi wana majawabu gani ndio bei ya mafuta ingeshuka?

Bei ya mafuta imepanda Uingereza penyewe'
Kwan na huyu mzee anajua kupanda kwa vitu
 
Mzee atuache tu, Yeye aendelee kupumzika alipopumzika huku sisi tunakula msoto.

Anga lao hili, wamechimba mifereji kila mahala.
 
In Magufuli voice wasfafu wanawashwa wapi huyu hajui maisha yalivyo
 
John.....
Nakumbuka hukuwahi kukiogopa kifo.
John..
Ulikiona kifo katikati ya mapambano kulitumikia taifa lako na watu wake kama Fahari.
Hukuchoka kusema kuwa uko tayari kukikabili.
Ulitamani kuwa mtumishi wa watu ambaye hata akifa, utaenda kuwa kiranja wa malaika kutokana na matendo yako mema.
Wenye imani, tunaamini kuwa hivi sasa wewe ni kiranja wa malaika huko mbinguni.
John...
Ulipotuacha, hatupo pale tena. Tumerudi nyuma kwa maelfu ya hatua. Sisi sio tena taifa linalochomoza miongoni mwa mataifa ambayo uchumi unakua kwa kasi. Tumekuwa magoigoi. Taifa halina mwendo.
John....
Ile ndoto uliyoihubiri na kuiishi kwa vitendo, ndoto ya kulifanya na kuliona taifa hili linajitegemea na kuondokana na utumwa mamboleo, ndoto ile imefutika na hatimaye imefunikwa na jinamizi la kuondoa kujiamini kwetu. Sasa, tunaaminishwaa kuwa misaada na mikopo ndio mkombozi wa uchumi na taifa letu.
John...
Uliowaamini wote wamekugeuka. Wanakuhubiri kama shetani uliyepewa kiti cha enzi.
Wameungana WOTE toka ndani na nje ya chama chako kukuvika taji la miiba.
Usijali John. Wanajisumbua kwa maana matendo yako yalimgusa kila mtanzania na yameacha alama ambayo itabaki milele ktk taifa hili.
John..
Wanasiasa wote wameungana dhidi ya wananchi. Wanakusanyana na kupiga picha kuwa wamepatana baada ya wewe kuwafarakanisha!!
Tunajua, kuwa hawana dhamira njema kwa taifa hili wala kwa watanzania hawa. Wameungana ili wale wakiwa wametulia.
Sisi watanzania uliotupigania na kutuaminisha kuwa tuna haki ndani ya taifa hili sasa tunapuuzwa. Wameungana dhidi yetu na hatuna mtetezi[emoji27][emoji27][emoji27]
John...
Wanakushambulia sana. Lakini bado hawajatosheka. Wameanza kushambulia hata yale uliyoyajenga.
Wanazishambulia ndege huku wanazipanda.
Wanashambulia barabara na madara ambayo wanapita juu yake.
Wanashambulia hadi bwawa la kuzalisha umeme wakati mgao wa umeme ukiumiza uchumi na maisha ya watu.
John...
Ukiwa kiranja wa malaika huko mbinguni, pumzika kwa amani.
Mbegu uliyoipanda itasiginwa sana lakini kuna siku itaota.
 

Mstaafu Jakaya Kikwete ameingilia kati mjadala wa kupanda kwa gharama za maisha kunakolalamikiwa na wananchi wengi na hii ni moja ya nukuu yake kupitia clip moja hivi inayosambaa sana kwenye mitandao.

'Bei imepanda sasa mtu ndio wanatunga na nyimbo, mafuta yamepanda bei ni unafiki mkubwa kwa kweli

'..eeeh unajua wakati mwingine offcourse ndio unasema adui yako muombee njaa wale wasiombea heri Serikali wanadhani lakini wakati mwingine ni lazima wawe wakweli tu haya mazingira wangekuwa wao ndio wako kwenye uongozi wana majawabu gani ndio bei ya mafuta ingeshuka?

Bei ya mafuta imepanda Uingereza penyewe'
Huyu Mzee na ccm wenzie ni wapuuzi tu,huwezi kulinganisha maisha ya ulaya na Tanzania,hata kama bei imepanda UK na TZ,lakini,kwa Mtanzania maumivu ni makali mala 100 kuliko raia wa UK,kwa maana hata kabla bei haijapanda,asilimia kubwa ya watz wanaishi kwenye ufukara wa kutisha,
Hawa wazee na ccm yao,wameshindwa kutatua changamoto za nchi hii,kwa hiyo anataka tuikubali hii hali,serikali imenyoosha mikono,Haina Cha kufanya,kwa hiyo tuombe Dua tu!!
Kama ccm wameshindwa,waachie ngazi,wapishe wengine,lakini kuendelea kuwa Madarakani,na kusema haiwezekani kutatua shida hii,wapishe wengine watoe majawabu.
 
Back
Top Bottom