Mzee Makamba ahamaki alipoulizwa kuhusu mgao wa umeme nusu amlambe vibao mwandishi wa habari

Kwa haya madudu yanayoendelea nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa nchi hii kwa sasa ina rais!!!! Watanzania tuandike maumivu tuna msukule ikulu anaendeshwa na nguvu ya hawa wezi wasiojali shida za wananchi.
 
Nkumbuka

Nakumbuka hata mimi kusema humu ndani kuwa pamoja na kuwa sikuwa nakubaliana na mambo fulani ya Magufuli, nilitaka awatandike kisawasawa hawa CCM-Asilia. Angekuwa ametuondolea tatizo moja kubwa sana.
 
Amejibu vizuri kwasababu muuliza swali alikusudia ufedhuli
Ufedhuli kivipi. Huyo si mwanachama wa CCM, tena mtu muhimu katika chama. Alitakiwa atetete kama anaweza utekelezaji wa chama katika kutatua matatizo hayo.

Ila nashukuru alivyojibu ili wale ambao wamekuwa hawaelewi tukiwaambia nchi hii imeoza wajionee wenyewe.
 
Kwa haya madudu yanayoendelea nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa nchi hii kwa sasa ina rais!!!! Watanzania tuandike maumivu tuna msukule ikulu anaendeshwa na nguvu ya hawa wezi wasiojali shida za wananchi.
Ni shida
 
Hii nchi wazee wasio wanafiki amebaki Warioba na Butiku

Makamba anasumbuliwa na udini na kulinda maslahi ya mwanaye aliyeiba mthihani wa form four aje awe Rais...

Kitu ambacho hakitakaa kitokee milele na milele amina!!!
Nasikia ni joseph huyu, hiyo yusuph ni ajili ya kuwazuga tu upande ule, Halafu eti huyu nasikia ni muha?
Mbona lakini ni kama wa mlimani kule tanga?
 
Mwandishi: Mzee Makamba nchi inakabiliwa na ukosefu wa maji na umeme, lakini wewe unasema mambo yako vizuri, hayo matatizoo.....

Mzee Makamba: Kwako nyumbani hauwaki?, kuwa na shukurani.

Mwandishi: Sawa, turudi kwenye hio point...

Mzee Makamba: Nakuambia nchi ni kama nyumba yako, hii nchi ni kama nyumba, huwezi kuwa na vyote humo nyumbani, una watoto 7, wanakwenda shule, huyu kaptura imechanika, huyu bado, huna hela utasema walimu subirini leo nimnunulie huyu, nchi ni kama nyumbani we nyumbani kwako umeyamaliza yote, baba yako ameyamaliza yote, mimmi sijayamaliza, unaitaka CCM iingie leo iyamalize, ni chama gani hicho? Kama haya huelewi hutaelewa ya mtu mwingine..

Mwandishi: Sawa tutu....

Makamba: Kuanza na neno lakini si sawa sawa, lakini ni kiungo cha ubishi, kama unajenga hoja jenga nini? usianze sentensi na lakini, lakini ni kiungo cha nini cha ubishi we hukusoma? nakuuliza hukusoma?

Mwandishi: Nilisoma.

Mzee Makamba: Mpaka wapi?

Mwandishi: Mpaka chuo kikuu.

Mzee Makamba: Umekijenga na baba yako?

Mwandishi: Sawa turud....

Mzee Makamba: Nakuuliza twende kwenye hoja, umesoma wapi?

Mwandishi: Matatizo ya nchi...

Mzee Makamba: Nakuuliza Twendeee kwenye hoja, umesoma wapiii?

Mwandishi: Kama katibu mkuu mstaafu...

Mzee Makamba: Nakuuliza swali hukusoma? hukusoma?

Mwandishi: Mzee Makamba labdaaa....

Mzee Makamba: Sisi miaka hio ya 60, tumeshinda vyuo vikuu hakuna, leo hii umekwenda chuo kikuu unasema nchi ina matatizo, umekijenga na baba yako?

Mwandishi: Mzee lakini mwanao analamba mno asali...

Mzee Makamba: Hio asali ulimnunulia?....

Mwandishi: lakini mzee?

Mzee Makamba: Twende kwenye hoja, hio asali ulimnunulia au ulikua unalamba nae?

Mwandishi: Lakini mzee, CCM ipo tangia mwaka 61, mpaka leo tunalia umeme maji....

Mzee Makamba: Kijana!!! Kijana!!! nitakunasa kofi... SHeenz umefunzwa kwenu hivyo eti eehh!!!

Mwandishi: Mzee Mwamvita yupo?

Mzee Makamba: Aisee hebu nishikieni kibaragashia changu kwanza na saa nimuoneshe huyu sheitwan....

Mwandishi: Mzee mbona tunasikia mwanao alinunua mitihani na alikuwa kiazi shuleni...

Watu wa pembeni: Jamani waachanisheni watauana.... afande, afande...

UVCCM mmoja: Aisee huyu mzee ana presha, presha imepanda iteni ambulance....

Mwandishi: Jamani mie huu mzee nilimheshimu kama mzee wangu tu, sijamgusa kaanguka mwenyewe....

Afande: Aroo uko chini ya urinzi......

SSH: Hilo nalo askari mkalitizame..
 
Hii nchi ni ngumu 😂
 
Hii nchi wazee wasio wanafiki amebaki Warioba na Butiku

Makamba anasumbuliwa na udini na kulinda maslahi ya mwanaye aliyeiba mthihani wa form four aje awe Rais...

Kitu ambacho hakitakaa kitokee milele na milele amina!!!

Aamina walahi [emoji2972]
 
Kizazi cha walamba asali (wahuni watupu)na kipana ni ngumu sana kuwaondoa madarakani watu hawa wanaolindana

Kaa utulie na uwe na positive thinking utashangaa mwenyewe kwani tumeona wababe wangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…