Mzee Makamba ahamaki alipoulizwa kuhusu mgao wa umeme nusu amlambe vibao mwandishi wa habari

Mzee Makamba ahamaki alipoulizwa kuhusu mgao wa umeme nusu amlambe vibao mwandishi wa habari

Yaani wanatudharau saaana wanaona nchiiii ni ya kwao.yaani huyu Mzee katuboa wengi .
Nchi ni ya kwao kweli hii nchi ni ya ccm, tukilikubali hili ndio tutaweza kuelewa hayo wanayoyafanya hao ccm ila tusipokubali ndio tutaendelea kushangaa tu na kulalamika hadi mwisho. Wewe unatamkiwa kabisa kama hutaki hamia Burundi, mnaambiwa muwe na shukrani ila bado tu hamjaelewa?
 
Mzee ameonesha kiburi, jeuri, ambacho anajua watanzania ni wajinga hawawezi kusema chochote, halafu anajua CCM ni chama Dola yaani ukifika uchaguzi polisi CCM wanapiga watu na kupora uchaguzi huku wananchi hawana maji, hawana umeme ,pia usisahau huyu Mzee na kikosi chake wanalamba asali Nape, Makamba, Kikwete, Riziwani, Samia. Ni heri wazungu wangebaki kuliko hawa wazee
Mzee Makamba ni Mzee wa Waraka! hii hadi sijajuwa umuhimu wa Waraka wao kwa Taifa!!
 
Mwandishi: Mzee Makamba nchi inakabiliwa na ukosefu wa maji na umeme, lakini wewe unasema mambo yako vizuri, hayo matatizoo.....

Mzee Makamba: Kwako nyumbani hauwaki?, kuwa na shukurani.

Mwandishi: Sawa, turudi kwenye hio point...

Mzee Makamba: Nakuambia nchi ni kama nyumba yako, hii nchi ni kama nyumba, huwezi kuwa na vyote humo nyumbani, una watoto 7, wanakwenda shule, huyu kaptura imechanika, huyu bado, huna hela utasema walimu subirini leo nimnunulie huyu, nchi ni kama nyumbani we nyumbani kwako umeyamaliza yote, baba yako ameyamaliza yote, mimmi sijayamaliza, unaitaka CCM iingie leo iyamalize, ni chama gani hicho? Kama haya huelewi hutaelewa ya mtu mwingine..

Mwandishi: Sawa tutu....

Makamba: Kuanza na neno lakini si sawa sawa, lakini ni kiungo cha ubishi, kama unajenga hoja jenga nini? usianze sentensi na lakini, lakini ni kiungo cha nini cha ubishi we hukusoma? nakuuliza hukusoma?

Mwandishi: Nilisoma.

Mzee Makamba: Mpaka wapi?

Mwandishi: Mpaka chuo kikuu.

Mzee Makamba: Umekijenga na baba yako?

Mwandishi: Sawa turud....

Mzee Makamba: Nakuuliza twende kwenye hoja, umesoma wapi?

Mwandishi: Matatizo ya nchi...

Mzee Makamba: Nakuuliza Twendeee kwenye hoja, umesoma wapiii?

Mwandishi: Kama katibu mkuu mstaafu...

Mzee Makamba: Nakuuliza swali hukusoma? hukusoma?

Mwandishi: Mzee Makamba labdaaa....

Mzee Makamba: Sisi miaka hio ya 60, tumeshinda vyuo vikuu hakuna, leo hii umekwenda chuo kikuu unasema nchi ina matatizo, umekijenga na baba yako?

Mwandishi: Mzee lakini mwanao analamba mno asali...

Mzee Makamba: Hio asali ulimnunulia?....

Mwandishi: lakini mzee?

Mzee Makamba: Twende kwenye hoja, hio asali ulimnunulia au ulikua unalamba nae?

Mwandishi: Lakini mzee, CCM ipo tangia mwaka 61, mpaka leo tunalia umeme maji....

Mzee Makamba: Kijana!!! Kijana!!! nitakunasa kofi... SHeenz umefunzwa kwenu hivyo eti eehh!!!

Mwandishi: Mzee Mwamvita yupo?

Mzee Makamba: Aisee hebu nishikieni kibaragashia changu kwanza na saa nimuoneshe huyu sheitwan....

Mwandishi: Mzee mbona tunasikia mwanao alinunua mitihani na alikuwa kiazi shuleni...

Watu wa pembeni: Jamani waachanisheni watauana.... afande, afande...

UVCCM mmoja: Aisee huyu mzee ana presha, presha imepanda iteni ambulance....

Mwandishi: Jamani mie huu mzee nilimheshimu kama mzee wangu tu, sijamgusa kaanguka mwenyewe....

Afande: Aroo uko chini ya urinzi......

SSH: Hilo nalo askari mkalitizame..
View attachment 2439144

Hahaa
 
Kuna wazee na raia wengi wa aina yake ambao mara zote wanachukulia nchi yetu kama familia tu na watawala ndio baba au mama zetu. Ni fikra za hovyo sana.
 
Habari ndugu zangu? Nimeangalia video hii ya Mzee Yusufu Makamba akihojiwa na ndugu Waandishi wa Habari ila nimeshangazwa na namna anavyojibu maswali kwa ukali na kushindwa kujibu maswali muhimu nimeshindwa kumwelewa huyu mzee nahisi kuna waya umekatika kichwani. N:B Baba na Mtoto hawaeleweki tatizo.​

View attachment 2439385

Mengine ni umri
Ukizeeka akili huwa zinarudi kama ulivokuwa awali
Unaanza kutosikia vizuri kama ulivokuwa mtoto
Unaanza kutetemeka ukisimama kama ulivokuwa unaanza kukua
Unaanza kuongea kwa kubabaika kama ulivokuwa mtoto
Unaanza kutambaa kama ulivokuwa mtoto
Mwishowe unafikia hatua ya kukaa tu na kubebwa kama ulivokuwa mtoto..
 
Data imezima
 
Kwani Makamba umri wake kawazidi miaka mingapi Wakina Butuku, Warioba, Shivaji, Biden, Kikwete?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu zangu? Nimeangalia video hii ya Mzee Yusufu Makamba akihojiwa na ndugu Waandishi wa Habari ila nimeshangazwa na namna anavyojibu maswali kwa ukali na kushindwa kujibu maswali muhimu nimeshindwa kumwelewa huyu mzee nahisi kuna waya umekatika kichwani. N:B Baba na Mtoto hawaeleweki tatizo.​

View attachment 2439385

Huyu akipewa nchi atakuwa mmbaya kuliko Magufuli.
 
Unavyizidi kuwa mzee ndivyo akili inazidi kupungua.huyo makamba akili imeisha ndiyo maana anashindwa namna ya kujibu
 
Back
Top Bottom