Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.

Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

Vyovyote iwavyo siuoni mwenendo mzuri katika siku zijazo kwa Askofu huyu. Ni hatari sana pale unapojaribu kujikomba kwa mtu mmoja kwa kumponda mwingine bila ya kuifahamu kwa undani wanapokuwa wamekaa pamoja wawili hao wanaongea vipi na wanaaminiana kwa kiasi gani.

Kiongozi mstaafu siku zote hapungukiwi ushawishi kwa aliyepo pale Magogoni. Askofu alipaswa kupima uzito wa kauli yake ili akwepe kufananishwa na mtu aliyelaaniwa.
Walemavu wa akili ni wengi sana Tz. na hii itachukua zaidi ya karne na karne kuondokana na ujinga,umasikini,maradhi,ufisadi,unafiki,uzambiki n.k.
Ukisikiliza Wengi wa viongozi wa swisswism na wapinzani hewa waliohudhuria mkutano wao wa familia yao wenye dhambi utagundua karibu wote ni walemavu wa akili kwani wanamjadili mtu na kusahau agenda zao.
Inanisikitisha nchi yangu ya kusadikika....
 
Mleta mada Nani kakwambia CCM wanaaminiana? Hao jamaa wanachekeana surani moyoni kila MTU kivyake.
 
Hv Pengo akisemwa tayari laana inatoka? Je Pengo si alimsamehe akiwa amekalia kiti cha uasikofu? Je Magufuli akimsema vizuri Gwajima kwenye hotuba yake, Makamba atajisikiaje?
 
Gwajima aliongea ukweli wengi hawakupenda kuusikia
 
Ingawa siungi matendo yanayo fanywa na Gwajima.
Lakini nathubutu kusema.......
Amakweli nyani haoni kundule aiseeee......[emoji15]
Hivi...[emoji47]
Huyu Mzee Makamba, si aliwahi kua mwalimu..!?
Ebu ngoja niishie hapa kwanza, nikatafute makabrasha ya kumbukumbu
Unataka kutukumbusha yale ya Kigoma kumpa mimba mwanafunzi na kukimbia? Acha bwana, nayo ya zamani watu wamesahau
 
Hivi Gwajima ni mtumishi wa Mungu au mwanasiasa?
Ni aibu mtumishi wa Mungu kuwa na tabia kama ya Gwajima!
 
JK na JPM sivyo kama tunavyowazungumzia mitandaoni. JPM anaweza kuikosoa atakavyo serikali ya awamu ya nne na zile zilizopita lakini mmoja wa washauri wake wa karibu ni JK. Hivyo wanavyokaa pamoja atakayeumia anaweza kuwa ni askofu.
Umejuaje?
 
Ngoja tuyaone hiyo kesho. Bahati nzuri umeme na lami inapita mlangoni kwa Gwajima hivyo hana ombi maalum toka kwa watawala.
 
Ukifanya mema unakuwa na mategemeo ya kwenda mbinguni, unapofanya dhambi napo njia yako ni motoni. Hivyo ndivyo anapaswa kuamini kila anaeamini uwepo wa nwenyezi mungu.
 
Naamini siku ya kesho Askofu Gwajima ni lazima atamjibu Makamba hadi Makamba ataomba poo japo kimya,kama alimjibu Slaa hadi akakimbia,akamjibu Pengo naye kimya atashindwa kumjibu Makamba,kama mwenzie JK amemtaja kimafumbo kwa kumuogopa GWAJIMA,sembuse makamba,tusubiri COMEDY mpya dah ksh rahhhhhhhhhhha saaaaaaana
Kukaa kimya si ujinga, bali ni hekima ...
 
Hapakuwa na haja ya kuendelea kumhusisha Baba Kardinari na siasa za chaguzi ndani ya CCM.
Mtoa tamko labda tu kama alikosea, lakini si vyema kuibua hayo kwani Baba Kadrinali alikwisha sahau na kumwachia Bwana wetu Yesu Kristo apate kuhukumu katika haki na ikiwezekana apate kumsaheme yule aliyemkwaza kwa kunena, kutenda na vyovyote vile ambavyo haikuwa sawa.
 
Natamani Gwajima ajibu ili siku zangu za kuishi ziongezeke
 
Baada ya siku ya leo Jumamosiya sabato kumalizika na mkutano mkuu kumpitisha kikwete,kesho ni siku maalum ya Gwajima kumjibu Makamba,naamini Makamba ameingia choo cha kike na ataomba poo japo kimya kimya na waandishi wa habari msikose Kanisa la UFUFUO na Gwajima kesho,hii ni komedy mpya inayokuja

kanisa hili si limefunguwa,? au nimechanganya kumbukumbu
 
Back
Top Bottom