Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Itakua mzee aliona hata msipokuja kwani yeye anaona,? Anasikia? Mtajijua wenyewe...hahahahah
 
Ndugu hayajakukuta
Nimeshawahi kufiwa.
Nilichotaka kusema ni kwamba sio lazima watu wajae msibani. Ndugu pekee wanaweza kuzika mtu wao bila msaada wa watu wengine. Kama uwezo mdogo wanao.
Kwani gharama za msiba hasa ni zipi tuanzie hapo. Ni kwamba tu tuna mazoea mabaya kutegemea watu waje msibani
 
Nakumbuka msiba mmoja zile siku Tatu za maombolezo naingia zangu pori kuchota maji nikawakuta wameinamishana wakanyaduana🥶Yan sku ya pili ya pili can imagine that 🤔
 
Mleta mada namfananisha na wapumbavu fulani wanasemaga usiposhiriki jumuiya, kanisani na kutoa zaka hatuji kukuzika 🤣🤣🤣

Yani wanajiona wajanja sana kumbe kumbe wangejua ninavyowadharau wasingeamini
Usipozikwa na sheikh ama mchungaji ety watu wanasema umezikwa kama mZoga, mara umekufa dhambi so kama haujaombewa mchungaji huendi mbinguni, ama huyo pumzika kwa amani
 
Kwani wameomba Fedha za msiba?
 
Sasa mkuu mandala hapo huwa nawazaga sana Mie siend kwenye misiba, siend sherehe yoyote kwenye imani yangu sehemu ya ibada daftari la mahudhurio sipo, sitembeleagi ndugu wala kuwasiliana nao🤔

S ndo kwangu watahudhuria mtu NNE😅
Mara nyingi jinsi ulivyoishi na Watu ndivyo utakavyozikwa ,Kama mtu wa watu msiba wako watu wajaaa kama kauzu ndio kama hivyo..

Kwa Siku Hz msiba ni Gharama,wasipokuja watu ni sawa sawa tu ki bajeti
 
Misiba kama hiyo naipenda sana.

Ni kama misiba ya wazungu majuu.

Familia mnaumaliza msiba fasta bila usumbufu na gharama za kulisha watu
Itoshe kusema kuwa Sasa kama inawezeka inahitajika Sasa funeral homes ziwepo Tanzania.
Haiwezekani tufike mahali watu wajione wajanja sababu wamesusia msiba.
Mtu unaenda funeral home unalipia kama kawaida mtu wako anazikwa, nyie familia na marafiki wachache mnahudhuria TU.
Wanazengo huwa hawaelewi kama mtu upon busy na maybe shughuli za watu. Saa ingine unanyimwa ruhusa au una mambo muhimu sana ya kufanya huwezi kuacha.
Ndio maana Yesu alisema acheni wafu wazike wafu wao.
Kama ni ndugu Yako umeshindwa kufika Kuna kuhani msiba. Lakini ndugu Huwa hawaelewi kabisa kabisa.
 
Ukifa umekufa tu,hata ungezikwa na maelfu ya watu haibadili uhalisia,kwanza naomba namba ya mjane nimpe pole(ng'ombe hazeeki maini)
 
Hiyo tabia ni hatari sana ya kutokuuzulia misiba na kutokula chakula Cha msiban
 
Misiba kama hiyo naipenda sana.

Ni kama misiba ya wazungu majuu.

Familia mnaumaliza msiba fasta bila usumbufu na gharama za kulisha watu
Temea chini nuksi hiyo isikuvae.

Kama una makandokando ya kutohudhuria misiba ya kwenye nzengo unayoishi, jitahidi ndugu nenda, siku hiyo ua shughuli zako.

Jamii inayokuzunguka ndiyo wanaokupima nyendo na tabia zako.

Hapa siyo Ulaya utasema kuna vikundi vya mazishi na wafariji wa kukodi.

Ukiona jamii inakutenga siku ya msiba wako, cha kufanya kuwa mpole, usilete ujuaji ama ngebe zako kabisa.

Hapo huwa imelengwa faini ya kujikosha na kurejeshwa kundini.

Kwa hiyo faini itakayoamriwa ndugu watakuchangia na ikishatolewa, watu wataendelea kushirikiana na wewe kama kawaida.

Mi niliona hayo kwa ndugu yangu, ilibidi wanandugu tuchangishane kununua huyo ng'ombe aliotozwa na nzengo katikati ya msiba, watu wamegoma kuzika mpaka ng'ombe alipotoka ndiyohali ya hewa ikarejea kawaida.

Mambo ya kijamii ni marahisi pia ni magumu sana usiombee yakukute mr.
 
nyie jitoeni akili tu,huu ni utamaduni wetu na usipoufata uta adhibiwa tu! This isn’t Europe mate.
Sasa hapo kaadhibiwa vipi? Maana familia na ndugu zake wameshiriki kikamilifu kumzika.

Hii ngozi nyeusi ina roho mbaya kupita race nyingine zote. Always kutafutiana sababu akukomoe.

Mwingine anakuambia umenipita hujasalimia halafu nakuta umepata ajali sikusaidia. WTF?!!

Huko makanisani ni misikitini ndio mnavyofundishwa hivyo?
 
Ni kama kukomoana. Kwa mfano mimi sipendi nyama ya mchuzi hata mama yangu alikua akipika atantengea tangu ya kukaanga pembeni. Lakini misibani wanapenda sana kupika ya mchuzi nikisema asante niko vizuri naonekana nina majivuno.

Nafikiri Moja ya kazi ngumu ni kuwa Mwafrika.
 
Hana hasara walio na hasara ni wale wanaoishi.
Hapo ni wkamba hawana fedha, ingekuwa msiba kuna wapishi, vinywaji raia wangekuja tu.
Mila za wapi huko kwenu?
Hawaji, hata ungekuwa tajiri na mang'ombe yamechinjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…