Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Misiba kama hiyo naipenda sana.

Ni kama misiba ya wazungu majuu.

Familia mnaumaliza msiba fasta bila usumbufu na gharama za kulisha watu

Ningekuwepo ningeshiriki kikamilifu. Maana huyo mtu lazima alikuwa na kitu tofauti.
 
Waafrika tupo obsessed sana na social empathy as if ukizikwa na mamia/maelfu watafanya ufufuke.
Si ndio hapo!! Matokeo yake familia inaingia gharama kubwa bila sababu za msingi🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Ni kama kukomoana. Kwa mfano mimi sipendi nyama ya mchuzi hata mama yangu alikua akipika atantengea tangu ya kukaanga pembeni. Lakini misibani wanapenda sana kupika ya mchuzi nikisema asante niko vizuri naonekana nina majivuno.

Nafikiri Moja ya kazi ngumu ni kuwa Mwafrika.

Afrika hata uwe jambazi au mla rushwa mkubwa, ukihudhuria misiba. Wewe wanakuona ni malaika
 
Mkipataga hela mnakuwa na nyodo utakuta zamani ulipenda sana uji wa msibani.Kila NCHI,jamii zina tamaduni na taratibu zao.Ni desturi za watanzania.
Ondoa kwanza habari za mkipataga hela mnakua na nyodo na dharau na hizo tamaduni. Tuongee uhalisia angalau kwa dakika moja.

Ni halali na haki kumlazimisha mtu kula?
 
Ondoa kwanza habari za mkipataga hela mnakua na nyodo na dharau na hizo tamaduni. Tuongee uhalisia angalau kwa dakika moja.

Ni halali na haki kumlazimisha mtu kula?
Halazimishwi mtu kila,SI halali.ila desturi za kuzikana zipo na zilikuwepo. Toka zama.Zipo familia hata 30000 ya kuanzisha mchakato wa misiba hazina.Huku uswahilini kabisa uswekeni haswa haswa.
 
Akipatikana wa kumzika inatosha na hawezi kukosekana maana harufu ya binadamu si mchezo. Sijui ni haya mavyakula tunayokula.
Ila kama ndugu wanapenda watu nasikia kuna wa kukodi wanalia kweli mradi uwalipe pesa yao.
 
Temea chini nuksi hiyo isikuvae.

Kama una makandokando ya kutohudhuria misiba ya kwenye nzengo unayoishi, jitahidi ndugu nenda, siku hiyo ua shughuli zako.

Jamii inayokuzunguka ndiyo wanaokupima nyendo na tabia zako.

Hapa siyo Ulaya utasema kuna vikundi vya mazishi na wafariji wa kukodi.

Ukiona jamii inakutenga siku ya msiba wako, cha kufanya kuwa mpole, usilete ujuaji ama ngebe zako kabisa.

Hapo huwa imelengwa faini ya kujikosha na kurejeshwa kundini.

Kwa hiyo faini itakayoamriwa ndugu watakuchangia na ikishatolewa, watu wataendelea kushirikiana na wewe kama kawaida.

Mi niliona hayo kwa ndugu yangu, ilibidi wanandugu tuchangishane kununua huyo ng'ombe aliotozwa na nzengo katikati ya msiba, watu wamegoma kuzika mpaka ng'ombe alipotoka ndiyohali ya hewa ikarejea kawaida.

Mambo ya kijamii ni marahisi pia ni magumu sana usiombee yakukute mr.
Wewe ndio umesema kuliko hawa wanaosema nzengo haina msaada huenda niwatoto wadogo sana tuwasamehe tu wakikua watajua nini maana ya nzengo
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Watu wanaendekeza vitu vya shortcut,misiba and harusi you can do whatever you want,kwangu mimi mgonjwa na mtafuta maendeleo ni viumbe muhimu sana km umeshindwa msaidia wkt wa kuuguza unaenda fanya nn wkt wa kizika,msaidie mtu akiwa hai Si kwenda kula ubwabwa na Pombe siku ya msiba
 
Haya mambo ya misiba tunapokwenda ni kubaya uswazi tunaishi na watu wenye Roho mbaya usisafiri misiba miwili ikakupita utaambiwa hautokagi misibani watasahau kama ulishawahi kuchimba kaburi la mzazi wao miaka mitatu iliyopita
 
Labla hapakuwa na nyama choma ndo mana raia wakagoma, mwnyw nngegoma
 
Unakuta mtu anaenda msibani siku zote na anakaa huko kuanzia chai, lunch hadi chakula cha jioni. Hapo unamfariji vipi mfiwa, na mchango ametoa buku mbili
Umenikumbusha juzi hapo jiran kafiwa na kaka mkoani
Watu wakajaa pale kumpa pole kama ujuavyo waswahili hawaondoki mpaka.kipikwe na mchango hawajatoa dada wa watu kawalisha kwanzia chai na chakula mchana kwa gharama za chakula chake cha ndani
Unaona wanapigiana simu kuitana msosi tayari wakisha kula hao huwaoni unabaki kujiuliza sikuizi misiban watu wanakuja kwa ajili ya kula au kumfariji mfiwa
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Ndio maana kuna kampuni za kuzika, huu ujinga utaisha one day, kwamba kazima uhudhurie misiba hata kama alie kufa hamjuani
 
La maana azikwe, hakuna mwili wa binadamu unaobaki juu ya ardhi. Hata kama hakuna kiongozi wa dini, azikwe kimila.
Huyo baba labda alijaribu kuishi kizungu ila mambo yaende. Si ajabu ukienda kwake bila taarifa unakarishwa sebuleni na wanaendelea kula. Hudhuria mazishi unapopata nafasi, sio ili watu wakuone.
 
Back
Top Bottom