Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Misiba ya kibongo unafiki Sana
One time nimefiwa na mtu wangu wa karibu akaja mwanangu mmoja wa mtaani kama saa tatu hivi usiku akanivuta pembeni akaniambia ameshindwa kuhudhuria Kwa wakati alikuwa kwenye mishemishe za utafutaji nikamwambie poa baada ya hapo akatoa autport eti nimchotee msosi dah! Nilichokaa Sana ukiongeza na majonzi ya kuondokewa na mpendwa wangu kiukweli niliumia Sana lakini ndo hivo kufa kufaana
 
Mleta mada wa watu kala chocho maana sio kwa vichambo hivi...😆😆😆
 
Ndo huu ujinga naupinga mia kwa mia,
wakati unakuta mtu wa kijijini kwenu akiumwa akapangiwa hospitali tuseme muhimbili,unapigiwa simu.
anafikia kwako,unamhudumia na pengine huko mhimbili hapajui unampeleka n.k
ila ukifa ukapelekwa maiti,wanavuta midomo kwamba huwa huji kuwazika.
Hivyo hivyo, embu jiulize kulivyo mbali ukiondoka saa 12 asubuhi unafika saa 7 usiku, halafu asubuhi uende kijijini masaa karibia 3, halafu mwajiriwa utaenda misiba mingapi na kazini utakuwa unaaga mara ngapi 😐😐😐
 
Back
Top Bottom