Mzee Mwinyi alituachia PPF Tower, Mkapa katujengea National stadium, Kikwete kaacha Mwendokasi na UDOM, sasa twende na Rais Magufuli

Mzee Mwinyi alituachia PPF Tower, Mkapa katujengea National stadium, Kikwete kaacha Mwendokasi na UDOM, sasa twende na Rais Magufuli

Magufuli amekuja kufanya mambo mengi sana, Watanzania tutamkumbuka huyu Baba kwa uchapakazi na upendo wake kwa Nchi
Kama asipokuteua hata kuwa Mtendaji Kata utakuwa wa kwanza kumsahau na kumtukana matusi ya nguoni akiwa bado yuko madarakani. Wengi tutamkumbuka kwa matumizi mabaya ya kodi zetu katika miradi isiyokamilika kama vile SGR ikiwa bado iko Kibaha, JNPP ikiwa bonde la jangwa, Rwandair ikisafirisha minofu ya samaki, Chato International Airport ikiwa ni malisho ya swala toka Burigi National Park nk. Labda wakulima wa huko kwa kupungua ajali za mikokoteni ya punda kwa msaada wa taa za barabarani.
 
Una haki uiamini CCM Kwa sababu hatuna wapinzani tuna wapingaji
Miaka mitano ijayo ya Magufuli nchi yetu itapiga hatua kubwa sana maana hii mitano ya awali pamoja na ugeni wake kathubutu kufanya Mengi makubwa cha ajabu kwa pesa zetu za ndani. Mitano ijayo atakuwa mzoefu na anajua nani wa kufanya nae kazi tutegemee makubwa kwenye baraza lake la Mawaziri lijalo litakuwa ni moto wa kuotea mbali sidhani kama kutakuwa na Waziri asieendana na kasi yake natabiri makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jk hakuacha hivyo umetaja. Na asingeweza hata angepewa awamu nyingine. Ukitaka ujue kuwa hakuwa na Plan hasa ya fly over, lile daraja la mwendo kasi asingejenga. Coz limeleta shida kidogo kwenye ujenzi wa fly over pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba JK hakuacha mradi wa Ubungo na Tazara interchange? au JKN terminal III? kwa taarifa yako tu, the initial plan ya TAZARA ilikuwa more complex and attractive klk hii ya Sasa na bajeti ilikuwa tayari.

Daraja limeleta shida gani?
 
Katuletea siasa za ajabu ajabu za chuki ambazo hazijawahi kuwepo nchini kwetu, watu regardless itikadi zao walikuwa wanapendana, kampeni ni burudani tupu, kushindana kwa hoja majukwaani - sasa hivi watu wanawindana kwa mapanga na mashoka - hii si Tanzania tuliyoijua, hatuitaki.
 
Magufuli amekuja kufanya mambo mengi sana, Watanzania tutamkumbuka huyu Baba kwa uchapakazi na upendo wake kwa Nchi
Sema amekuja awamu ambayo miradi mingi ilikuwa imefikia hatua ya utekelezaji. Hakuwa na option, ilibidi itekelezwe tu.

Miradi yote unayoiona ni mipango ya muda mrefu hakuna jipya aliloibua
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
]Sema amekuja awamu ambayo miradi mingi ilikuwa imefikia hatua ya utekelezaji. Hakuwa na option, ilibidi itekelezwe tu.

Miradi yote unayoiona ni mipango ya muda mrefu hakuna jipya aliloibua
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
Unachokifanya hapa ni sawa na kuishukuru ATM kwa kukupa hela zako
 
Kafanya mengi sana ila kwenye ajira tyuu kabugi!nilisomeshwa kwa mkopo wa vikundi leo sina ajira ..nashindwa kulipa den nimeuza mpaka uwanja wa urithi ..anasema tujiajiri ikiwa yeye kaomba ajira kwa wanannchi!

Mkumbusheni ajira ..bwana
Asisingizie korona wakati bongo hatuna tena!
 
Hujui kitu bwana nenda zako. Kwanza nani kakuambia daraja la kigamboni ni la serikali.

Daraja la kigamboni na chuo cha udom ni vya nssf. Ukipita pale kigamboni wanaichaji hela ni wafanyakazi wa nssf.
usinifanye Nicheke aisee udom na Daraja ni vya nani?
 
KWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,,kama umeminya hivi,,ila #Kuunga mikoa yote nchi nzima kwa Rami, # JAKAYA KIKWETE Heart Instute, # Maslahi BORA kwa wafanyakazi,
 
1. Stiegler's gorge HP
2. SGR
3. Uundwaji wa meli lake victoria, tanganyika na nyasa.
4. Ununuzi wa ndege na upanuzi wa viwanja vya ndege na vya kisasa kabisa.
5. Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa( fly overs, madaraja ya busisi across lake victoria na tanazanite bridge. Pia barabara nane ubungo - chalinze, ujenzi na upanuzi wa barabara za kisasa unaoruhusu magari kupishana hata matatu hivyo kupunguza ajali.)
6. Usambazaji wa umeme kuanzia kwenye tarafa, kata hadi vijiji.
7. Vituo vya afya bwerere. Tena vya kisasa na huduma ya oparesheni ili kupunguza vifo vya uzazi.
8. Miradi ya maji na usambazaji wa maji maeneo mengi.
9. Uboreshaji wa vyuo na sekondari zilizichoka.
10. Wanafunzi kukaa chini imebaki historia.
11. Ufufuaji na usimamizi wa mazao na kumnufaisha mkulima( pamba, mkonge, chikichiki, korosho, ufuta.) Pamoja na uondoaji wa tozo.
12. Usimamizi wa mapato ya serikali uliowezesha serikali kuwa na akaunti moja badala ya 2000.
13. Usimamizi mzuri wa vita ya corona. Hapa kila mtanzania alijua tumeisha. Jamaa alitia ujasiri wa hali ya juu sana.
14. Upigaji na upigwaji kwenye ardhi umepungua kwa asilimia 90.
Mengi sana unaweza kuandika vitabu.
Mavi-Jana ya Tanzania ni mapunguani, yanafikri kukenga maflyover ndio maendeleo hayo! Hebu ulizeni raia walivyo chakali kwenye mifuko! Magu kafuta ajira serikalini raia wanalia!
 
Ila jamani kuna kitu sielewi, kwanini serikali ya Tanzania ikifanya jambo la maendeleo inapongezwa kama vile imefanya hisani na sio lazima?,
Kwani hao viongozi huchaguliwa ili wafanye nini?
Je hizo pesa wanazofanyia miradi mbali mbali zinatoka mifukoni mwao au ni kodi za wananchi?

Unakuta watu wanasifia kuwekewa umeme na maji au kujengewa hospitals na shule,
Come on guys, hizo ni kazi zao ndio maana mliwachagua na sio kama wanafanya msaada, si waliomba hiyo dhamana wakatoa na ahadi, basi ni wajibu wao kutekeleza na wasipotekeleza ndio tulipaswa kuongea na ikibidi kuwaadhibu.

Wake up guys.
Dah...kweli kuna vitu huvielewi......jiulize.....sasa kwanini mtu anapo oa anapongezwa?.....au anapofanya vizuri katika masomo yake anapongezwa? au Yanga anapomfunga Simba anapongezwa?? 🤣
 
Mkuu ni nini ambacho huelewi? Una shida binafsi na JK au nini maana sielewi, kama 2000 ilipendekezwa na haijawahi kuwa nauli rasmi, unasemaje kuwa ndy abiria walikuwa wakilipa? Tangu mradi umeanza nauli rasmi ilikuwa 650 period. Sasa Kama walipropose iwe 2000, 1000, 6000 hayo yatabaki kuwa ni mapendekezo tu.
Elewa mzee nimekuambia mradi ulisimama sababu ya buku mbili. Mradi ulianza kazi baada ya majaliwa chini ya jpmkuingilia kati na kuamua nauli iwe 600.

Fuatilia vizuri taarifa za huo mradi. Inawezekana we umeanza tu kupanda mwendokasi ili hujui nini kilikuwepo kabla mradi kuanza.
 
Back
Top Bottom