Mzee Mwinyi alituachia PPF Tower, Mkapa katujengea National stadium, Kikwete kaacha Mwendokasi na UDOM, sasa twende na Rais Magufuli

Mzee Mwinyi alituachia PPF Tower, Mkapa katujengea National stadium, Kikwete kaacha Mwendokasi na UDOM, sasa twende na Rais Magufuli

Mavi-Jana ya Tanzania ni mapunguani, yanafikri kukenga maflyover ndio maendeleo hayo! Hebu ulizeni raia walivyo chakali kwenye mifuko! Magu kafuta ajira serikalini raia wanalia!
Lini raia walisema wana hela mfukoni? Au awamu ipi raia walisema wana hela. Enzi za jk mlisema hali ngumu hadi mkazungusha mikono, mkasema heri ya mkapa.
Kipindi cha mkapa mkasema ukata umezidi heri ya mzee ruksa. Ni lini mliishi hali?
 
Kacheki taarifa toka hapa.
aliyekwambia NSSF sio mali ya serikali ni nani?Ni nani anapanga safu ya uongozi? NSSF sio kama makampuni ya Barhesa au Mo.Lakini kwa taarifa yako tu NSSF kumiliki hostel za MAbibo(udsm) au Udom au kuwekeza kwenye Daraja la Kigamboni haifanyi kua wamiliki wa chuo au barabara/Daraja mwisho wa siku serikali ndio mlinzi mkuu kwa niaba ya umma.Kinachofanyika ni PPP.
 
Wengi wanakurupuka na kumsifia JMK kwa sababu tu wana chuki na JPM. BWM na JMK ni marais wabovu ambao hawataondoka kwenye hiyo historia hakuna asiyefahamu kwamba mashirika yetu yaliuzwa kama njugu then akaja mvumbuzi Vasco da Gama. Yale yote aliyofanya yalikuwa na gharama gani kama sio wizi wa mchana kweupe. ATCL ilikufa, Tanesco ilikufa, shule zilikuwa hoi, viwanda vyote vilikufa hata betri tu ambazo Matsushita walikuwa wanatengeneza ilikufa kifo cha mende. Watu wanasema hivi sasa kwa sababu tu wanataka kumkejeli na kupuuzia jitihada zilizofanywa na JPM kuiweka nchi katika kuwa na uchumi ulio imara, hazina wakati JPM anaingia kulikuwa kweupe leo hii 6 months import credit ipo pale. Je wakati wa JMK hizo pesa zilikuwa zinakwenda wapi? Je, wakati wa BMW hizo pesa zilikuwa zinakwenda wapi? Hayo ndio maswali ya kujiuliza.

Mtamchukia sana JPM lakini JPM ni jembe kweli kweli ambalo limenolewa na chuma cha pua. Mnaompenda sana JMK nendeni mkanywe naye chai kwa sababu mateso aliyowapa Watanzania katika kila nyanja yanajulikana hatudanganyiki.

Wafanyakazi hewa walishamiri katika utawala wake, Hospitali zetu ziligeuzwa kuwa hosteli za kuwaangalia wagonjwa bila kuwatibu, wote waliishia kwenda India kutibiwa kwa pesa za walipa kodi na kama humfahamu mtu serikalini basi utaishia kufa kama kuku. Watoto wa JMK nao walikuwa marais wadogo huko mitaani.

Kuna mengi ya kutia aibu wakati wa utawala wa BWM na JMK tunaweza kujaza hii forum lakini tuishie hapo tu kwa leo.
 
Achana na hao ..tena JPM katumia mshahara wake kabisa
Mshahara wa rais Tanzania (JMK) ulikuwa USD 15000.00 kwa mwezi JPM kapunguza hadi USD 5000.00 kwa mwezi. Sasa unaweza kuona hapo Uzalendo wa JPM. ''mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.''
 
1. Stiegler's gorge HP
2. SGR
3. Uundwaji wa meli lake victoria, tanganyika na nyasa.
4. Ununuzi wa ndege na upanuzi wa viwanja vya ndege na vya kisasa kabisa.
5. Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa( fly overs, madaraja ya busisi across lake victoria na tanazanite bridge. Pia barabara nane ubungo - chalinze, ujenzi na upanuzi wa barabara za kisasa unaoruhusu magari kupishana hata matatu hivyo kupunguza ajali.)
6. Usambazaji wa umeme kuanzia kwenye tarafa, kata hadi vijiji.
7. Vituo vya afya bwerere. Tena vya kisasa na huduma ya oparesheni ili kupunguza vifo vya uzazi.
8. Miradi ya maji na usambazaji wa maji maeneo mengi.
9. Uboreshaji wa vyuo na sekondari zilizichoka.
10. Wanafunzi kukaa chini imebaki historia.
11. Ufufuaji na usimamizi wa mazao na kumnufaisha mkulima( pamba, mkonge, chikichiki, korosho, ufuta.) Pamoja na uondoaji wa tozo.
12. Usimamizi wa mapato ya serikali uliowezesha serikali kuwa na akaunti moja badala ya 2000.
13. Usimamizi mzuri wa vita ya corona. Hapa kila mtanzania alijua tumeisha. Jamaa alitia ujasiri wa hali ya juu sana.
14. Upigaji na upigwaji kwenye ardhi umepungua kwa asilimia 90.
Mengi sana unaweza kuandika vitabu.
Ufufuaji wa usafiri wa reli Dar to Moshi

Ujenzi wa daraja ya Mwanza Sengerema

Viwanda vimetakaa nchi nzima

Wateja ofisi za serikali ss wanathaminiwa

Shirika la ndege sasa liko hai

Dodoma kuwa makao makuu

ONGEZEA KWENYE ORODHA YAKO
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.

Dah. Mkuu hivi ndivyo vigezo vyetu vya maendeleo au umeamua kutusanifu “wanyonge”? Kweli tuna hali mbaya kama ni hivi.
 
Mshahara wa rais Tanzania (JMK) ulikuwa USD 15000.00 kwa mwezi JPM kapunguza hadi USD 5000.00 kwa mwezi. Sasa unaweza kuona hapo Uzalendo wa JPM. ''mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.''
Mkuu unajua kusoma tu.....
Kwahiyo katiba imebadirishwa ili kuhusu mshahara wa Rais mkuu?
Watu awajui kua jamaa katumia pesa za mshahara wake.
 
PPF tower imejengwa kipindi gani na pesa za nani, usisahau kusema na madeni wanayotuachia pia na mali walizotupotezea kwa ubinafusishaji usio na tija

Ni bahati mbaya sana hapa TZ watu wana ujuzi wa “kuhesabu miradi” hasa ya ujenzi na manunuzi kama kigezo cha maendeleo bila kuangalia mazingira (context) yake yote na matokeo halisi (impact) kwenye uchumi wa taifa na kuboreka kwa maisha ya wananchi.

Miradi ya aina hii mara nyingi inachangamkiwa na viongozi serikalini kwa vile inawezesha ufisadi mkubwa mkubwa na ni rahisi kuwaonyesha wananchi kama “maendeleo” (yanayoonekana kwa macho) huku kukiwa na uhakika kuwa hakuna mwenye jeuri ya kuhoji “value for money”. Tena mingine hulazimishwa hata bila kuwamo kwenye vipaumbele vya taifa. Kiongozi anaamua tu na “kutoa” pesa.

Pamoja na umuhimu wake, umakini mkubwa sana unahitajika katika kuelewa, kupanga, kugharamia na kutekeleza miradi ya aina hii ili iweze kuwa kigezo sahihi cha maendeleo. Leo hii, pesa kubwa ya pensheni za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi imeyeyuka, taifa limeelemewa na madeni makubwa, serikali inahangaika kukopa hata kwenye mabenki ya kibiashara angalau kujongeza utekelezaji wa “miradi ya kimkakati”. Halafu watu wanawahi hapa JF kutambiana kisiasa kuhusu “maendeleo makubwa” yanayofanywa na viongozi “wapendwa”. That’s too simplistic. Tusione kama Watanzania wote ni vilaza.

Itakuwa vyema zaidi tukituliza papara na kuvuta subira kuona mwelekeo mzima wa hii miradi na uchumi kwa ujumla. Hakuna kitu kama “instant results” kwenye uwekezaji wa kimkakati kitaifa. Pongezi za haraka haraka hazina tija. Hii si North Korea. Km nilishangaa sana kuona mwaka wa kwanza tu ATCL mpya kuanza kazi, manazi wakajitosa JF kutambiana na kubishana kwamba shirika limepata faida/hasara! Hizi jazba za kisiasa zinapoteza umakini katika uendeshaji wa nchi.
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
Wote wamefanya mambo yao ila JPM ni mzalendo kuliko wote
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
Yaani umetazama vyote Vyenye thamani ya Rais ukaona hostel ambazo hata KAM college wanazo nzuri tu. Na ukatazama vibgine vyote ukakosa ukaona Daraja la makutano la Ungungo.

Kweli huu utawala uondoke tu. Asante Johnthebaptist kwa kuusema ukweli.
 
Mzee kwenye Mambo ya ujenzi anaendelea kufanya Mambo mengi sana tano yangu kwake
 
Miradi mingi mijubwa ya pesa nyingi ipo ktk hatua ya mwanzo kabisa labda angejikita ktk mradi mmoja mkubwa unaogusa nchi nzima au ukanda fulani ndani ya miaka hii mitano ya CCM Mpya wangeweza kuonesha kitu kilichokamilika. Tuorodheshe miradi ambayo kazi ndiyo imeanza na bado inaendelea (work-in-progress)chini ya 33% na haijulikani lini itakamilika au kuleta faida:
  1. Mtandao wa SGR reli work-in-progress progress Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika
  2. JNHPP work in progress 'Timu ya Taifa' ya Wahandisi katika mradi wa Umeme Rufiji
  3. Dreamliner 787 , bombardier work in progress Shirika ndege KLM latimiza miaka 100 toka kuanzishwa na miaka 50 ya kutua Tz,ATCL inalo la kujifunza
  4. Korosho masoko work in progress Sakata zima la Korosho
  5. Reli mkoloni ukarabati work in progress Ukarabati wa reli ya kati wafikia 76%, Benki ya Dunia yafanya ziara kuona maendeleo ya mradi
  6. Gesi ya Kusini 6% ya uwezo wa bomba ndiyo inatumika Jesca Kishoa: Gesi yote inayopatikana Mtwara inakwenda kumilikiwa na China na Bomba la Gesi lenyewe
  7. Jiwe la msingi Makao Makuu Dodoma Kwa muonekano wa nje, Ikulu ya Dar es Salaam ni nzuri kuliko Ikulu ya Dodoma
  8. Demokrasia, Uhuru wa Habari, Mtu-Huru-Mtanzania
 
Back
Top Bottom