Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Ukiamua kuelezea mazuri tu ya Iddi Amin basi naye anaweza kuwa malaika...kuna wakati nilikuwa na rafiki yangu kutoka Uganda, kila tukizungumzia siasa basi alikuwa akimsifia sana Iddi Amin..
Usemalo ni kweli kabisa, nilienda Uganda 2014, wenzetu wanamzunguzia Idd Amini very positive kuliko Militon Obotte
 
Sasa hivi CCM yake imekuwa na wenyewe,ndani yake kumejaa waheshimiwa wa wizi wa kura na fedha pamoja na waporaji wa mali za umma.Mwl.alikuwa mnyenyekevu hadi umauti ulipomkuta akiwaita wananchi wenzake NDUGU.
Ndani ya chama dola na serikalini hakuna Mzalendo kama Mwalimu J.K.Nyerere,siyo hawa nyapara wa sasa wanaotulazimisha tuhamie Urundi.Yaani wakati sisi tukiambiwa twende huko tutakuwa tunapishana na Warundi wanaokimbilia kisiwa cha Amani!Maajabu hayaishi Tanganyika.
 
Warioba kwao anakotoka wengi wasabato wakiwemo ndugu zake
Wasabato huwa hawapendi siasa kanisani

Ndio maana kasema hivyo

Kakulia mazingira ya wasabato
 
Warioba kwao anakotoka wengi wasabato wakiwemo ndugu zake
Wasabato huwa hawapendi siasa kanisani

Ndio maana kasema hivyo

Kakulia mazingira ya wasabato
Ni suala la maadili tu bila ya kuingiza usabato wala upagani. Ni suala la unyenyekevu aliyojifunza kutoka kwa Mwalimu Nyerere aliyekuwa mkatoliki halisi.
 
Kifupi warioba kakulia kwenye eneo la usabato

Mkewe Evelyn Ojjiki ni msabato hasa

Wasabato na siasa kanisani mbali kabisa nje fanya sio kanisani .Mkewe ndie kam shape kwenye hilo

Apigiwe mkewe makofi ya hongera kwa kumshikisha adabu kuwa siasa fanya nje ya kanisa sio ndani ya kanisa

Hongera mama Evelyn Ojjiki kwa kazi umefanya credit zije kwako sio kwa warioba wala Nyerere
 
Si Mandela tu; hata rais wa Vatikano Yohana Paulo alipokuja ilikuwa hivyohivyo.
Papa alikuja 1990 Septemba kama sijakosea. Alipokelewa na Mwinyi aliyekuwa ni rais wa wakati ule, nadhani Mwalimu alikutana nae ikulu.

Nakumbuka jioni ile alipofika palikuwa na misa pale Saint Joseph jioni kama saa kumi na mbili hivi. Kesho yake tukaenda kwa maandamano kusali Jangwani misa aliongoza Papa mwenyewe.
 
Unampa mtu sifa wakati hazistahili. Nyerere mwenyewe alikuwa mnyenyekevu mwenye akili timamu.

Hakulewa sifa za kijinga na alitanguliza tabia ya mijadala yenye tija. Alipenda kuusikia ushawishi wa hoja ya mtu na sio kupelekesha watu.
 
Labda wakati wanaoana miaka hiyo ndio alikuwa msabato. Yule mama mwaka 2001 nilikuwa nae katika mafungo ya karismatiki katoliki pale Mbagala kanisani na yalikuwa ni ya wiki moja.

Sidhani kama msabato anaweza kuhudhuria mafungo yale. Labda familia aliyotoka ni ya wasabato lakini baada ya kuolewa amekuwa ni mkatoliki.
 
Atakuwa alibadili dini kufuata mwanaume enzi zao katoliki alikuwa hawaruhusiwi kuoa madhehebu mengine hadi mtu awe katoliki

Yule mama msabato kwao wote wasabato
 
Alifanikiwa kumzuia mmewe asihubiri siasa kanisani lakini akashindwa kimzuia kutumia whisky na sigara?! Hizo bidhaa kwetu wasabato marufuku.
Hakuweza kabisa ila kwenye hilo la marufuku siasa kanisani aliweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…