Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani


..lakini wasaidizi wa Jpm wanasema alikuwa anapenda kula chakula na wasaidizi wake na kutaniana nao.

..pia wanasema Jpm alikuwa akiwahimiza wasaidizi wake kusali/kuswali. Zaidi aliwahimiza wasaidizi wake Waislamu kwenda hijja.
 
Nadhani huu uhuni wa kutumia mimbari za nyumba za Mungu kutoa matamko ya kisiasa tumeanza kuuona kwa JK,kwa Mwendazake ilizidi! Yaani akipewa Mic ilikuwa ni kufoka mpaka kukashifu Watumishi wa Mungu!
Mwezi uliopita mmoja alipewa mic huko Njombe akaanza kuhamasisha waumini kutoa zaka
 

..Na kusema uongo.

..aliwahi kusema hawezi kukutana na wapinzani kwasababu wanataka kumuua.

..Kassimu naye alikwenda msikitini na kudai Jpm ni mzima wa afya anachapa kazi kipindi ambacho alikuwa mgonjwa amelazwa.

..hakukuwa na ulazima wa Kassimu kusema uongo msikitini.

..Kitendo hicho kinaonyesha jinsi awamu ya 5 ilivyokuwa na viongozi wa hovyo-hovyo.
 
Ila wewe ni Kubwa JInga jinga hivi .Toka lini Amaan Karume akawa mdogo wa Rais wa Zamani Wa Zanzibar ? Ndugu zangu Watanzania ,hiki ndicho kizazi tulicho nacho sasa hivi ,maneno mengi lakini kichwani hamna kitu.Kizazi kilichopinda,kinachojifanya kinajua kila kitu lakini upuuzi mtupu.Ulizeni au fanyeni tafiti kabla ya kuandika siyo kukurupuka asubuhi asubuhi unaanza kuandika.
 
Nyerere alikuwa msomi wa falsafa, kamsoma John Stuart Mill Edinburgh Scotland na kumuandikia papers, anajua separation of church and state ni nini.
Ndiyo maana hakuhubiri kanisani.
Sikumbuki lini kumsikia akitoa maagizo st Peter au kanisani. Ikiwa aliongea katika maeneo ya dini ni katika hafla maalum kama sherehe. Nyerere alielewa maana ya kutenga dini na siasa

Kiongozi aliyepalilia sana hotuba katika nyumba za ibada ni mwendazake, tulisema hili wazi
Nimeshangaa majuzi VP naye akiwa kanisani akazungumza mambo ya serikali
Nadhani ni muhimu sana viongozi watambue kuwa nchi haina dini watu wake wana dini, wengine hawana dini n.k. Kutoa maagizo maeneo ya ibada si sahihi , huko waachwe washusika
Alijua namna ya kuishi na watu. Ukifuatilia hotuba zake Nyerere alionyesha kuijua nchi na watu wake. Alikuwa muungwana sana

Mzee Warioba ameongea ''kidiplomasia '' kuhusu viongozi wa siasa kuomba vipaza sauti, ni kosa
 
..lakini wasaidizi wa Jpm wanasema alikuwa anapenda kula chakula na wasaidizi wake na kutaniana nao.

..pia wanasema Jpm alikuwa akiwahimiza wasaidizi wake kusali/kuswali. Zaidi aliwahimiza wasaidizi wake Waislamu kwenda hijja.
Ni ngumu sana kuamini!! Sidhani hao wasadizi wangeweza kusema tofauti
Anaweza kuwa mkarimu kwa wasaidizi wa karibu sana aliokula nao tu!
 
..lakini wasaidizi wa Jpm wanasema alikuwa anapenda kula chakula na wasaidizi wake na kutaniana nao.

..pia wanasema Jpm alikuwa akiwahimiza wasaidizi wake kusali/kuswali. Zaidi aliwahimiza wasaidizi wake Waislamu kwenda hijja.
Kuwahimiza watu kusali/kuswali si kazi ya rais.Tena inaweza kuwa improper imposition of a president's beliefs on others.

Ndiyo hiyo habari ya separation of church and state.Nyerere alilielewa hili. Hili ndilo lile lile Jaji Warioba alilolisema. Rais hatakiwi kuhubiri dini, kutoka madhabahuni kanisani au mbele pale msikitini, au hata Ikulu.

Nyerere alikuwa na msaidizi wake mzungu yule mama Joan Wicken, nilikuwa naenda Ikulu ananipa ma apples.

Yule mama ni agnostic, hajali habari za Mungu kuwapo au kutokuwapo, anasema hilo swali halijibiki na hivyo ni la kupoteza muda.

Nyerere alijua hilo, alimjua Joan Wicken ukianza kuongea naye habari za Mungu na dini mnaweza kugombana.

Nyerere alikuwa Mkatoliki, lakini aliheshimu sana hoja za Joan Wwicken kwenye mambo ya dini. Hakumuhubiria kuswali au kuswali.

Na Nyerere alikuwa rafiki wa Joan Wicken mpaka anakufa.

Hakuwa na ujinga wa kuhubiri dini akiwa rais.

 
Rais ni taasisi hakoseai ,πŸ˜‚πŸ˜‚
Taasisi ya urais ilikosea kutoweka vioo katika corridors za Ikulu ili watu wanapokata kona za corridors za Ikulu waweze kuona upande wa pili wa kona kuna mtu anakuja ama la.
 
Mada inamhusu nyerere hao wengine wa Nini? By the way kufa kwao hakumaanishi ndo nchi itafunwe, Kuna tofauti kubwa kipnd Cha utawala wa nyerere na Karne hii ya wasomi, mi naona mzee alikuwa Bora kwa kipindi kile, kwa namna Tanzania ilivyo kwa Sasa akitokea mtawala km nyerere watu watampinga hadharani, na hicho ndo kilichotokea kwa jpm
 
Mwanasiasa anayepanda madhabahuni anakuwa karibu sana na anguko lake. Labda awe alishawahi kuwekwa wakfu.
Magufuli alipoanza kuhutubia vijimambo kila alipoenda kusali, nilimtonya rafiki yangu mmoja nikamwambia , huyu jamaa hajui anafanya nini.
Na nilijisemea tu kuwa madhabahu itamwadhibu, pale si mahali pa mizaha.

Mtu asiye na roho wa Mungu huwa haelewi kuwa madhabahu zinawekwa wakfu na ni mahali pa waliowekwa wakfu vile vile.
 
Jamani hivi kweli mnamlinganisha Nyerere na JPM?!!

Kama hamumfahamu Nyerere jitahidini kufuatilia habari zake za kweli, hotuba zake, watu waliofanya nae kazi kina Dr Salim, n.k, n.k

Nyerere mnaeambiwa vijiweni kuwa alikuwa hivyo mnapotoshwa kabisa!!!

Anachofanana na Magufuli labda ni uanaume na kuwa rais!

Tabia, upeo, akili nyingi, werevu, busara, maono n.k tofauti kabisa ni sawa na makande na Biriani!
 
Usemalo ni kweli kabisa, nilienda Uganda 2014, wenzetu wanamzunguzia Idd Amini very positive kuliko Militon Obotte
2014 unaongea na vijana wa waliozaliwa miaka ya tisini (1990s), unaulizia utawala ulioisha kabla hata hawajazaliwa!!

Wamehadithiwa tu kama unavyohadithiwa habari za Nyerere.
 
Mjinga ni wewe unayejifanya profesa wa chuo kikuu kumbe kidampa fulani tu. Lengo langu nimsema mdogo wake aliyekuwa Rais wa Zanzibar ambaye ni mtoto wa Karume mzee.

Kabla hajagombea urais aliwahi kuwa balozi wa Tanzania kule Ujerumani miaka ya nyuma, aligombea mwaka 2005 kipindi kile kulipokuwa na wagombea karibu 40 wa CCM.
 
Kila Jumapili panafanyika mageuzi ya sakramenti, yale ni mambo mazito na jicho la kibinadamu huwezi kuona kitu lakini katika hali ya kiroho panatisha pale mahali.
 
Vidole vyangu vina allergy na hewa chafu ya baadhi ya watu humu.

Ukiona hivyo karibu nitaondoka.

Nimekusawazishia usihitaji algorithms za Claude Shannon kunisoma.
Ila weye mkuu una mambo sana.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…