Bandari sio ya mkoloni!
Mkoloni aliacha gati 2 sasa ziko 7. Mwarabu wanasema anakuja kujenga saba (japo haipo kwenye mkataba), kwa hiyo Mwarabu akijenga gati 7 na sisi tulijenga 7. Katushinda nini ?
Nyerere took over the helm akaanza kuzijenga kuanzia 1970. Bandari imejengwa phase nne, Sultani, Mjerumani, Nyerere, na Magufuli (ujenzi wa Magufuli kaja kuuzindua Rais Samia 2021).
Msikilize huyu mwamba, shuhuda, mkufunzi na mwanafunzi wa historia ya Tanzania kuhusu nani alijenga bandari:
Kwa hiyo tuliweza kupanua bandari sisi wenyewe mdogo mdogo. Kwa nini Nyerere na wasaidizi wake kina Warioba na baadae Magufuli hawakuhitaji Mwarabu kuongeza ma gati ya bandari?