Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

sahihi kwa 100%, wanasiasa akishaitwa mheshimiwa tayari anajiona yeye ni mtu maalum sana wakati kiuhalisia ni tofauti.

kuna watu kibao huku kitaa wapo smart sana kichwani kuliko hako kakikundi kanakoongozwa na Ndugai pale Dodoma!
Tofautisha mbunge na huyo smart wako wa mtaan!
 
Hakuna lolote hapo ni kujikweza tuu, kwanza hivyo vyeo kama ubunge majority waliiba kura, wengine walipita kwa figisu bila kupigiwa kura, sasa hoja kwamba wamepewa cheo na wananchi haina mashiko. Hivi ukiitwa ndugu mbunge au ndugu mwenyekiti akili kichwani itahama au busara zitahama??
 
Iko wazi mbona: Ili uitwe Mheshimiwa ni lazima ujiheshimu kwanza, vinginevyo ukiitwa Mheshimiwa kama hustahili, unapakwa tu mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Wewe na yeye mzee Warioba nani anajua zaidi mambo ya kiutawala?

Huyo mzee ni waziri mkuu mstaafu unaleta usukununu wako hapa?
Pia amewahi kuwa mbunge na amewahi kuwa jaji, achilia mbali tume mbalimbali zilizoundwa na rais ambapo yeye aliteuliwa kuwa mwenyekiti mfano tume ya rasimu ya katiba pendekezwa
 
Warioba ndiyo kundi la Nyerere ambao walipinga but walishindwa na hilo kundi la wengi..
 
Ndiye mzee pekee mwenye busara aliyebaki kwa sasa
 
Ushahidi upo humu ni kweli Nyerere J. K. Aliitwa Ndugu, ipo video youtube chipukizi akimkaribisha kukagua gwaride alimwita ndugu.., alikuwa na utu toka damuni
 
Wewe ni mdharauliwa?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Pia amewahi kuwa mbunge na amewahi kuwa jaji, achilia mbali tume mbalimbali zilizoundwa na rais ambapo yeye aliteuliwa kuwa mwenyekiti mfano tume ya rasimu ya katiba pendekezwa
Umeonaeee?
Tanzania tuna watu wa ajabu sana kama huyu anahoji weledi wa mzee Warioba kisiasa!
 
Yaani mtu/mbunge umwajiri wewe mwananchi kupitia kura yako halafu umwite mheshimiwa? Khaa
Wivu upo wapi hapo
 
Siyo lazima aitwe mheshimiwa, ni ndugu tu inatosha
 
huyu mzee angekuwa rais wa sasa wa jamhuri ya muungano wa tanzania nchi ingekaa sawa sana.,
 
Hiyo tafsiri kapeleke kijijini kwenu! Nyerere mwenyewe alikuwa anaitwa ndugu. Tulia ndo nani!
 
Ngoja tusahihishe kidogo.
Wakati wa Nyerere akiwa rais hakuitwa Mtukufu, aliitwa Ndugu rais, au Mwalimu.
Wabunge waliitwa Ndugu mbunge.
Nadhani ni Mzee Mwinyi aliyekuja kuitwa Mtukufu.
Wabunge nao wakapitisha hoja kuwa waitwe waheshimiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…