Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Duh Kwa hio na wake zake itakuaje sasa??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ameshakula vitu vitamu vyote hahaahahaAiseeee, basi poa kama ni kweli.
![]()
Ameenameen Mwenyezimungu amjaalie
Alikoenda ndio atapiga hela zaid atatoa kaswida na kuuza kama wanavyofanya gospel singersAjiandae kutafuta mke mwingine,
Hawa alio nao watamkimbia,
Njaa inaitaji mazoea.
Ameen yaa Rabb.Allah azidi kumuongoza katika njia iliyonyooka,,
Amiiin.
Hakuna aliyewahi kumuona ila tunasoma vitabu na kusikia na kuamini ndio maana tunatekeleza kile tulichosikia/kusoma na kuaminiHakuna kitu, huo ni unafiki au kuna hofu imemuingia maishani, nani aliwahi kumuona Mungu?
Vitabu hivi vilivyoletwa kwenye majahazi! Kwanza vina contradiction kibao!Hakuna aliyewahi kumuona ila tunasoma vitabu na kusikia na kuamini ndio maana tunatekeleza kile tulichosikia/kusoma na kuamini
Ukiona hivyo muda wa mtu hujafika,muda ukifika kama kwa Mzee utaacha yote na utaongozwa na neema tuu,ingekua tunatumia nguvu kufanya mema wanadamu woote tungekuwa watakatifu ila ni NEEMA tu ikuvuteKwakweli haya mambo yananitatiza sana na inaonekana kwa dunia ya sasa nafikiri hali ni tofauti kwa yale aliyosema yesu kwamba ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mungu hivi sasa nafikiri tatizo lipo kwetu malofa maana unaambiwa ukienda kuhijji makka au israel(inategemea na imani yako) basi unasamehewa dhambi zako,sasa leo imekuwa kama fasheni mtu anafanya mabalaa yote wizi,dhulma,ufisadi,ujambazi,ulevi,umalaya n.k halafu kesho unasikia kaokoka au anamrudia mungu anaenda kuhijji lakini vyote alivyovipata kwa njia ya halamu bado anavyo na amesamehewa,nafikiri tuache kumchezea mwenyezi mungu.
Ni mtazamo tuu ila mmoja akasema "CHAGUENI NINYI WA KUMTUMIKIA LKN MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA TUNAYEMWAMINI"kwahiyo ndugu hapa sihubiri ila mitazamo iko tofautiVitabu hivi vilivyoletwa kwenye majahazi! Kwanza vina contradiction kibao!
Atakuwa anawaza na kujutia mambo ya akina Issa Kijoti, Sheba Juma n.k! Ha ha ha ha!Hizi dini zote mbili zimeanza kupoteza umaarufu kwenye bongo za binadamu wanaowaza kwa tafakuri, hivyo basi tukio kama hili la Mzee Yusuf ni moja ya wapanga mikakati wa hizi dini.
Mzee Yusuf kama alikuwa hajawa tajili basi sasa ndio utajili huo umemfikia yeye atatumika kama alama ya mtu maarufu aliyeamuwa kumcha Mungu.
Hii dunia ina mambo mengi nyuma ya panzia ambayo ni vigumu kuyagunduwa katika jicho la kawaida.
Hakuna commentAliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.
Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)
Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).
Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.
Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)
Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.
Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
NB: ukitaka kujua ibliis huwa hapendi kuona watu wakiwa kwenye njia sahihi subiri comments hapa chini za ibilisi waliobaki ambao jambo hili limewakera na litawakera sana