Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Atakuwa anawaza na kujutia mambo ya akina Issa Kijoti, Sheba Juma n.k! Ha ha ha ha!
Hawa kina Kijoti kulikoni? Maana mimi kwenye taarabu sina ninalolijuwa na si mshabiki hata chembe wa muziki huu.
 
Sio kila mtu anaweza kufanya mziki, mziki ni special talent ambayo Mungu amewajaalia watu wachache sana. Sasa kama kufanya mziki ni haramu, Mungu alitoa hivi vipaji vya nini? Kwa matumizi yapi labda? Nawaza tu msinirushie mawe
 
Assalaamu 3alaykum warahmatullahi wabarakaatuh

BREAKING NEWS

Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
 
Dah, sasa tutapata jembe kama Mzee kweli? Utunzi yumo, uimbaji usiseme, vyombo ndo kabisaaaaaaaaaaaaa ukianza na kinanda!! Mungu alimtunuku sana ndugu yetu huyu ingawa hatujui yamemsibu yepi! Allah Akbar...!! God is Great..!!
 
Habari hii siiamini. Iliishawahi kuja habari kama hii kumhusu huyu huyu Mzee Yusuph kuwa kaacha taarabu. Haikuwa kweli. Leo niaminije? Muda tu ndo utakaosema.
 
Assalaamu 3alaykum warahmatullahi wabarakaatuh

BREAKING NEWS

Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

[/b]Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.[/b]

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.

Waombee wasanii wote bila kujali dini
 
Back
Top Bottom