Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Kaswida sio dhambi, huu muziki wa vinanda, gitaa n.k ndio haramu

N.B mimi sio muislam ila nina rafiki ustaadh huwa ananipa mawaidha
Umeshawahi kumuuliza ni kwanini keyboard na gitaa vimeharamishwa peke yake?
 
Hivi atapata msamaha kwa Allah kweli?au anajidanganya? Alishamkosea Mungu huyu na watu wengine ,watu wamevunja ndoa zao kwa ajili ya taarabu yake .Sasa Mungu atampa msamaha je wale aliewakosea?
Huo utaratibu wa kusamehe ala hana.
 
1471034584581.jpg
 
Kuna kipindi alisema atagombea jimbo huko Zanzibar em mtu anaejua alikua chama gani atupe taarifa sababu alisema atatangaza nia ila sikumsikia tena.

Pia nampongeza kuacha mziki wa taarab ni mziki wa wambea na wapika majungu sionagi kama una la maana zaidi ya kuimba upuuzi.
 
Hahaaa comments zinatgemeaa aliendika post n wa ibilisi AMA lah
 
Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.


NB: ukitaka kujua ibliis huwa hapendi kuona watu wakiwa kwenye njia sahihi subiri comments hapa chini za ibilisi waliobaki ambao jambo hili limewakera na litawakera sana
dah ndo basi tena tushamkosa mwamba na tutarajie kukosa ladha ya kundi la jahazi maana ye ndo kiongozi ,na likifa jahazi ndo mwisho wa taarabu kwa kuwa itakosa ladha kwa kiasi kikubwa hayo makundi mengine yapoyapo tu, daah mzee rudi bana
 
Back
Top Bottom