Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 28,259
- 41,416
Umewahi kwenda ukapaona pazito?Acha atubu akhera pazito mkuu..kaona mbali sana huyu jamaa..Allah atupe mwisho mwema sote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umewahi kwenda ukapaona pazito?Acha atubu akhera pazito mkuu..kaona mbali sana huyu jamaa..Allah atupe mwisho mwema sote.
Umeshawahi kumuuliza ni kwanini keyboard na gitaa vimeharamishwa peke yake?Kaswida sio dhambi, huu muziki wa vinanda, gitaa n.k ndio haramu
N.B mimi sio muislam ila nina rafiki ustaadh huwa ananipa mawaidha
Huo utaratibu wa kusamehe ala hana.Hivi atapata msamaha kwa Allah kweli?au anajidanganya? Alishamkosea Mungu huyu na watu wengine ,watu wamevunja ndoa zao kwa ajili ya taarabu yake .Sasa Mungu atampa msamaha je wale aliewakosea?
Wale wanamuziki waliokufa morogoro walisema alihusikaga kama kweli Mungu amsamehe
Yap mkuu hizo tuhuma zilimuhusufivestars modern taarab
teh teh teh ataanza kulia tena aise duuuuMtamuongezea kilio mkuu.
Atasamehewa bhaaaaanaHuo utaratibu wa kusamehe ala hana.
Wale majambazi wakishaungama waliowaua katika matukio wanakuwa wamefufuka
Hujui[emoji15]Mziki ni dhambi?
kudadekiii itakuwa MagomeniKwani alimwacha mungu wapi
WeenomaaaaaasanaaaaNa wasiwasi na majibu aliyopata ANGAZA [emoji848]
dah ndo basi tena tushamkosa mwamba na tutarajie kukosa ladha ya kundi la jahazi maana ye ndo kiongozi ,na likifa jahazi ndo mwisho wa taarabu kwa kuwa itakosa ladha kwa kiasi kikubwa hayo makundi mengine yapoyapo tu, daah mzee rudi banaAliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.
Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)
Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).
Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.
Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)
Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.
Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
NB: ukitaka kujua ibliis huwa hapendi kuona watu wakiwa kwenye njia sahihi subiri comments hapa chini za ibilisi waliobaki ambao jambo hili limewakera na litawakera sana