Chikumbutsu husema tekinolojia yake inatumia usumaku-umeme wa mawimbi radio...
Maarifa halisi ya utundu wa tekinolojia yake ya uvunaji wa umeme kutoka kwenye 'utupu' ni 'siri'; japo kwa sasa inaweza kuwa hivi kwa sababu za wazi:
USALAMA WAKE BINAFSI.
Kiukweli khasa wa mambo, utundu huu wa kugema umeme kwa sakiti za usanifu maalum--sakiti maalum za kiuelektronishi ni uwezekano; ni kitu ambacho kimefanywa 'daraja siri' kwa kuwa mapelekeo yake kwa '
statusi kwou' ni yenye kutikisa khasa
mifumo ya uchumi-siasa-tawala Duniani kote.
Ikiwa jambo la Chikumbutsu litafaulu, kurasmisha tekinolojia ya Umeme kutoka kwenye Utupu, Serikali ya Zimbambwe itakuwa imejipanga na kujiandaa na 'figisu' za 'vibopa' wa 'Fedha/Misaada/Tasnia ya Viwanda/jeshi'--Kiintelijensia na Mikakati; ama hiyo nchi ya Afrika imepata 'Kibali' cha 'Wazee' wa 'Dunia ya Mungu, Vitu vya Mzungu'...
Tekinolojia za kimapinduzi zipo; lakini haitakuwa rahisi hizi kurasmishwa kwa kuwa 'zinaweza kutibua kila kitu' katika mifumo ya fedha hapa Duniani. Wazee wa 'Dunia ya Mungu, Vitu vya Mzungu' wapo tayari hata kudhamini mikutano ya kimataifa na kutoa/kuahidi 'midolali' ili mradi tu 'Jumuiya ya Kimataifa inachezeshwa Sikinde Ngoma ya Ukae'....
Tukiwa sisi ni miongoni mwa mataifa tunayopofushwa na 'Fedha/Ruzuku/Mitaji/Uwekezaji' na mapana yote ya mataraji ya Kibepari, hatuwezi 'kupindua meza' kwa kuwa Viongozi na Watendaji katika taasisi zetu primu wanapumbazwa ama kupelekwa puta na mataraji ya 'upatikanaji wa fedha' ama 'Misaada' ya namna hii ama ile...
Hili linatutaka sana sisi kupangana kimya kimya kuhusu maendeleo yetu na mustakabli wetu kijamii, maendeleo na ustawi wetu. Inashangaza kuona khabari za Chikumbutsu zinafungamana na 'Wachina' kuingia kwenye ukuzaji na uendelezaji wa tekinolojia za utengenezaji wa vyombo vya uchukuzi, ni jambo linalofaulu kuwekwa kwenye 'Kisomo' na wadau wa uono na ufikirifu mifumo...
Nchi zote zilizoendelea, wanayomashirika na wadau wenye hizi tekinolojia na suluhu; lakini wanajikausha kimikakati....
Hmmm