SIYO 'TAPELI'...
Japo 'Usanii' upo...
Hadi hapo ubunifu wake utakapokuja kuwekwa wazi, Uwezekano ni kwamba tekinolojia yake ni uvunaji rahisi wa '
Nishati kutoka kwenye Utupu'.
Kwenye uga wa sayansi na tekinolojia hutajwa kama '
Nishati Nukta Sifuri'--Zero Point Energy, ZPE.
Ulimwengu wote unafanyika kwa 'pumzi za kiumeme'; ukijua kwa mfano '
Kapasita' ina maajabu gani khasa ambavyo hata tuseme basi: Umeme wa Mkondo Nyoofu, Umeme KN, haupiti ili kutiririka katika Sakiti ya Uelektronishi na khali Umeme Mkondo Geu unapita; unakuwa umekaribia kujua 'siri' ya mbegu ya u-JUAJI-ji ya utundu wa Chikumbutsu...
View: https://www.youtube.com/watch?v=k7_PX8BqUYY
Unachohitaji kujua kwa nyongeza, ni finomena ya Umeme Mkatizo, namna fulani ya athari ya kiumeme inayoitwa '
Transient Electrical Effect'; haya uyafananishe '
Athari Kasmiri' ili uelekee kwenye jambo linafahamika kama 'Utetemeazi Sumaku-Umeme wa Kikwantumu--
Quantum EM Resonance' katika '
Nafasi iliyotupu/Utupu/Vakyumu'... Hapa unahitaji mapana ya maarifa ya 'Ufizikia usio wa Kiunafasi--Non Local Physics', mambo ya 'Fizikia Unishati Sumaku-Umeme ulio ni Skala--Scalar Electromagnetism... Unaweza 'kupindua meza kuhusu Unishati na nguvu zake' kwa kupangua 'muundo wa vipitishi umeme vilivyo 'active-Vya kiutendaji'... Kwa mfano, unafahamu koili ya kawaida inasokotwa vipi kwenye sakiti(?).. huwa kama 'Nyoka anayejizungusha mwelekeo mmoja... Lakini ukisokota waya mwelekeo mmoja halafu ukageuza mwelekeo kinyume katika sakiti hiyo hiyo, nafasi hiyo hiyo ya kiminyongoroto, basi huo ni ndiyo mwanzo wa kuotea 'Utetemeazi wa Kikwantumu kwa Unishati Umeme-sumaku'...
Kwa utundu wa kusokota nyaya--iwe kwa maumbo zaidi ya 'ubomba'--labda kusokota kama '
Pia' kwa mfano; kupitisha umeme kwenye 'Mbawa Mbili' ama 'Usindano na Bawa', kwenye ufilamenti na ubomba unaweza 'kutekenya' nguvu za Kiumeme Sumaku zilizopo pote na kokote... Na ndiyo hili linashahibiana na utetema -- pumzi za nishati ya umeme, ambayo inakidhi kutambuliwa kama 'Mawimbi Radio'... Utemema kwa makadirifu ya kihisabati ni 'frikwensi za kasi sana za Ugeu wa Umeme' na uhamonifu wake...
Hauhitaji kuwa '
Charles Steinmetz' wa 'nadharia za Umeme'--Utundu na Magutu vinaweza kukuongoza kuotea mawezekano ya ajabu ya umeme...
Nikola Tesla, alikuwa mtundu na mwenye magutu, japo kuzungumzia 'magutu' ndiyo kuelekea kwenye 'Dunia ya Mungu'...
Ndani ya Miaka 15 kutoka mwaka huu, 2025, haya mambo ya kuvuna umeme kwa sakiti maalum za ZPE yatakuwa ni jambo la kawaida... Na linakwenda kubadilisha mambo mengi sana katika maisha na ustaarabu wetu hapa Duniani... Vyombo vya uchukuzi ardhini na hewani vinakwenda kubadilika sana... Na hili, linakwenda kututaka tubadilishe yote ya 'Uchumi Mbovu' wa leo Duniani...
Sasa Mzee Trump kuja na haja ya
mradi wa 'STARGATE' ndiyo 'ingilio lenyewe' la 'Uchawi' wote wa mambo haya... Unaweza kuendesha 'Langonyota' kwa chanzo cha nishati kilicho ni ZPE ukilivaanisha hili na matumizi ya Akili Bandia... Siyo umeme wa 'Mabwawa' ama nini...