Mzimbabwe Maxwell Chikumbutso ameunda gari inayoendeshwa kwa nguvu za mawimbi ya radio

 
... Wazungu siku ile wali conclude kuwa Mtu Mweusi ni kiumbe cha kuheshimiwa. Waliondoka wakiwa shingo upande kwasababu hawakuambulia kitu.
... sio kwa sababu hakuna kitu hata hivyo?
... sayansi tumesoma wengi tu, na majibu mengine unajua tu kwamba hapa kanyaboya!
😅
 
Weka chanzo cha hizi stories.
 
Huyonkijana alindwe sana, mashetani wa kimagharibi watamfinya.
... hamna kitu hapo ndugu yangu! ... au umesahau mwingine aliibukaga Uganda na teknilojia ya magumashi akawaingiza mjini mpaka akina Museveni?
NDOTO NI MWANZO MZURI, ... LAKINI ZI'MAKE' SENSE KIDOGO BASII!
 
Au ni yale mambo ya kusema tutawaletea umeme usiotumia nyaya wala nguzo za Tanesco wakimaanisha solar electricity.
 
Nitaisoma habari hii kwa kiingereza kuelewa nini hasa kimefanyika.
 
Tatizo tuna Siasa nyingi sana na we never ask how na explanation ya kutosha..., ndio maana kuna yule mtu alikuja Bongo na sijui Umeme unaoendeshwa na sumaku pekee (perpetual machine) hadi waziri akakutana nae, ingawa wadau tunaoangalia mambo na kwa undani na kupitia theories za hapa na pale tukasema hapa kuna walakini...

Kwahio huyu mdau ni wa kuuliza inaendeshwa maana yake nini ? Yaani ni kama remote inayotumia hizo waves ili kuendesha hilo gari linalotumia hio Nishati ? Au ni kama kuna Nishati unaweka ili iweze kubadilishwa na hizo waves ili kupata usable energy ya kuendeshea hilo gari na hio Nishati inabadilishwa kutoka nini kuwa nini (Energy can never be created not destroyed)

Sababu implications za hilo jambo sio gari tu kama tunaweza kupata Nishati ambayo ni bora na rahisi kuliko mafuta, maji / gesi au mechanical energy ambayo tunaweza ibadilisha ikawa umeme kwanini tuishie kwenye magari pekee, si tufunge hata lile Bwawa kule Nyerere na viwanda vyote vya makaa ya mawe ili tuanza kutumia hayo mawimbi ?

Moral of the Story..., Always ask HOW... na Kuelewa lugha ya Kibiashara sababu kuendeshwa kunaweza kumaanisha vitu Vingi na siku hizi wajanja ni wengi hapo huenda kavuta pesa za angel investors na miaka kumi ijayo bado kutakuwa na prototype ambayo bado inarekebishwa maabara....
 
Waafrika tunapenda sana kulishana Matango pori, yaani mtu avumbue njia mpya ya uzalishaji umeme ambayo inakaribiana na dhana ya "free energy" afu mataita na mabepari wa dunia wakuache kizembe zembe ? Hamko serious 😂😂
 
Mimi mwenyewe tangu jana nimeanza kupata ukakasi na explanation za jamaa na cha ziada ni kwamba uvumbuzi anaoongelea ni revolutionary sana yaani nina uhakika hadi BBC wangekua huko Zimbabwe sahizi
 
Huyu jamaa mimi nina wasiwasi ni tapeli, nachojua mawimbi ya redio yanabeba nishati ndogo sana....... Hivyo iwaje kitu kinachokuwa na nishati ndogo hivi kuweza kuendesha gari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…