Mzungu huyu atakuwa ameamua tuachane au yuko busy?

Mzungu huyu atakuwa ameamua tuachane au yuko busy?

Ulivyojibu umejibu sahihi kabisa. Niliamua kuongezea tu observation yangu kuwa wanawake wengi huwa wanajioverrate. By the way mwanamke mzuri wa kuvutia kila mtu atamuona ni mzuri tu. Haya mambo ya kusema uzuri upo machoni mwa mtu ni porojo tu.

Ni kweli na sioni haja kuji overrate sababu jamii ndio inakuona kuliko unavyojiona wewe...km ni mzuri universal utaonekana tu.
 
Ni mda gàni umepita tangu hayupo online?
 
Fikiria unachomwa na jua hadi unasikia harufu ya nyama choma, halafu unaona watu wana drive tu ndinga kali kali barabarani halafu watoto wadogo. Hadi unajiuliza kama binadamu wote ni sawa[emoji23][emoji23].
Fursa ikitokea ni kuchangamkia tu, kisa cha kuzeeka mapema ni nini? Yaani binti wa miaka 25 anakuwa kama mama wa miaka 40 na wakati ana namna ya kurahisisha maisha[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah watu mna maneno sio poa!
 
Unamuhitaji huyo jamaa zaidi ya sana. Siku tatu tu umekuwa na hofu kiasi hicho. Bora hata ingekuwa mwezi,.kweli mapenzi upofu.
Kama ni siku tatu tangu walipochat mara ya mwisho ni sawa kwa binti kuwa worried, ukisha develop feelings hata nusu siku inatosha kufanya uwaze nini kimempata mwenzangu, worse enough ni mahusiano ya mbali....sucks like hell!!
 
Kama ni siku tatu tangu walipochat mara ya mwisho ni sawa kwa binti kuwa worried, ukisha develop feelings hata nusu siku inatosha kufanya uwaze nini kimempata mwenzangu, worse enough ni mahusiano ya mbali....sucks like hell!!

Better you understand me, long distance relationship inahitaji utulivu sana wa nafsi niko worried kwa vingi tu mimi siku niliyopata ajali ilikua ni lisaa tu baada ya kuchat nae na kumwambia am going out nikapata hiyo ajali hivyo ht ningekufa angebaki anajiuliza tu asipate majibu..na si kawaida yake so kibinadamu lzm nipate sintofahamu nyingi.
 
Habari za leo wanajamvi!

Nimeona nilete hili jambo kwenu labda nitapata msaada wa mawazo na ushauri wenu ili nielewenini nifanye.

Mimi ni binti wa mid 20's km unavyojua kila mtu hua na malengo yake katika maisha basi na ana machaguo yake katika maisha km ambavyo mtu anapendelea mwanamke mwenye shape nzuri, au macho mazuri au sura nzuri, vivyo hivyo baadhi ya mabinti hupenda wanaume warefu mara wenye hela basi mimi ni binti nnaependa kudate na ngozi nyeupe (wazungu) ila si vile vibabu vya kizungu[emoji23].

Well, km ijulikanavyo huwez kupata kitu km hukifanyii efforts so nilikiunga na dating sites kadhaa katika one of the dating site nikakutana na kijana mmoja wa umri wa miaka 31 kutoka nchini Norway, huyu hakua kijana pekee niliewah kukutana nae ila wengi hawakuonyesha userious so na mm sikutaka kuwa entertain till nilivyoanza kuchat na kijana huyu, mwanzo alionyesha ukawaida km wengine so ckumtilia maanani sana ila ndani ya muda mfupi tu wa kuchat km week1 alionyesha km ana ka userious flan km kujibu txt ontime, kutoomba nudes (picha za utupu), kutaka kunijua kiundani na kufikia maamuzi ya kuomba if I can be his girlfriend of which I accepeted..alipanga aje nchini mwishon wa mwez huu na alishakata flight ya tarehe hizo za mwishon na hii ni only after 2 weeks of knowing each other, well niliona km things are going too fast ila sikuichukulia in negative way sababu mapenzi hayanaga formula.

Week 2 baada ya kua tunachat nae every day nilipata minor accident iliyonipelekea kuvunjika vidole vyangu vitatu vya mguu nikafungwa P.O.P (hogo) nikamtaarifu kua nimeumia na kumtumia picha swali la kwanza ni aliniuliza "Do you have western union?" Nikamjibu sina akaniuliza unaweza kutumia njia gani kupokea heka kutoka abroad nikamwambia ngoja niulize maana kiukweli nilikua sijui ndio one of my friend akaniambia nitumie "Worldremit" baada ya kumtumia hiyo app alishangaa maana hakuwahi kuitumia before ila aliidownload na akawa ananitumia screenshot kila hatua ili aweze kufill details zangu...baada ya dakika km mbili simu yangu ilisoma nimepokea laki7 za kitanzania kutoka kwake nilimshukuru kwa kweli ukizingatia sikumuomba ile hela na wala sikua na wazo hilo..aliniambia zitanisaidia kwa transport fees baada ya kujua sina personal car.

Tukawa tunaendelea kuchat by the time alikua na likizo za sikukuu za Christmas and new year so muda mwingi alikua online, he seems like he is an introvert masna kwenye video call hua ni km aina ya mtu anaeishiwa maongez though ni mchatiji mzuri, aliniuliza nacope vp hali ya kuwa nyumban mda wote wakat niko na ile P.O.P nikamjib kawaida tu sina jinsi inabid nitulie akaniuliza km nchini kwetu tuna Netflix nikamjibu ndio ila sikua na account akanitumia details za his personal account means user name yake na password yake na na akaniambia " do not freak out there is another girl using my account but thats my sister" so tulikua tunatumia hiyo accout mimi, yeye na huyo user mwingine ambae sikufatilia sana kumjua as long as alishaniambia ni dada yake..akanitumia kias kingine nijiunge na unlimited internet ili nisiwe bored.

Tuliendelea kuchat mpk alipomaliza likizo ya kaz na alivyoanza kazi, well mawasiliano yalipungua sio chatting za muda wote ila nilielewa sababu ya ubusy, ila lazima atatuma txt mara tu baada ya kutoka kazini mtachat au kuongea kidogo ndio atalala.

Juzi ndio ulikua mwisho wa mimi kuchati nae na our last conversation..aliniambia anatoka mara moja kutembea sababu amekaa ndan muda mrefu and he asked me how was my leg? Nilimjibu ila text ile haijafunguliwa mpk leo

Txt inadelever ila in grey tick which means haijafunguliwa, his last seen inaonyesha muda ule ule ambao tulichat mara ya mwisho so ni km hajaingia online tena, ila txt zinafika hofu yangu ni kua ya Mungu ni mengi amepata tatizo labda au? Maana siwez kujump kwenye bad conlclusion maybe amepata tatizo ila txt zinadeliver sena hazijafunguliwa tu na hajaingia online...ameamua kuquit mahusiano au? But hatujapishana kwa lolote au ni mimk ndie nina overthink?

His netflix account still works to me here, sijatuma txt nyingi sababu sion point ya kutuma txt wakati za mwanzo hazijajibiwa na hayuko online...je kwa wengine ishawahi watokea kitu km hii? Ina uwezekano akawa yuko busy sana? Isije nikasubiri meli wakati niko airport..Ndio masna nikaja hapa sababu ya ushauri wenu na mitazsmo yenu inaweza nisaidia.

I have developed some feelings for him honest speaking ila ni vyema nikajua niko position gani kwa sasa ili nisipoteze muda na hisia kwa mtu ambae labda si km nimfikiriavyo au nijaribu kumpigia kwa simu ya kawaida?

What do u think I should do guys? Au nisubiri tu nione itakuaje?
Pole bi dada!!! Kwanza jifunze kua mkweli na muwazi na wakati mwengine unapo andika Banfiko la kuomba Ushauri liwe fupi na kujitocheleza. Mengine uwe mwangalifu. Mitandao inamambo mengi ya kupotesha. Jifunze kua mvumilivu na mustaarabu. Utafanyikiwa...
 
Pole bi dada!!! Kwanza jifunze kua mkweli na muwazi na wakati mwengine unapo andika Banfiko la kuomba Ushauri liwe fupi na kujitocheleza. Mengine uwe mwangalifu. Mitandao inamambo mengi ya kupotesha. Jifunze kua mvumilivu na mustaarabu. Utafanyikiwa...

Asante mkuu kwa ushauri wako ntaufanyia kazi[emoji120]
 
Cha kwanza nilichokiona tu kwako una tatizo la njaa kwenye mahusiano sio rahisi kwa mtu wa kawaida kukwambia hilo ila most girls wanaowinda wazungu huwa ni sababu ya njaa tu na si kingine. Cha pili tuliza mshono.

Huyo jamaa atakutafuta tu usioneshe kuwa demanding sana huwa mambo yanaendaga smooth tu!
Taratibu mwenzio hajazoea maneno makali makali [emoji23]
 
Back
Top Bottom