Mzunguko wa hewa huwa sio mzuri ndani ya Bus zenye viyoyozi (AC), bora kufungua vioo tu

Ndege zina mfumo maalum wa kuchakata hewa na kuingiza oxygen ndani ya ndege na pia kutoa hewa chafu ndani ya ndege, unaitwa Environmental Control System(ECS)
Elezea huo mfumo wa ndege, usiishie to kusema ECS.

Kimsingi mfumo wa ndege na bus hauna tofauti kubwa, japo upo more advanced kuliko wa mabasi. Ndege hazitoi fresh air kutoka angani kwa sababu ya hewa kuwa too thin, kimsing 30,000ft kuna oxygen ndogo sana hivyo ndege hata ikitumia mfumo wa kuingiza oxygen kutoka nje itakuwa kazi bure tu.

Rather, inatumia hewa inayotokana na engine compressors kuchakata hadi kupata oxygen, inafanya recycling ya hewa inayotoka kwa abiria ili kupata hewa mpya.

Likewise kwa bus, mfumo ni huo huo ila unahusisha hewa ya nje+hewa inayokuwa recircled kutoka kwa abiria. Changamoto ya mabasi kubwa ni kuwa, compression ya hewa ni ndogo as compared to airplanes hivyo abiria hapati 100% ya oxygen anayoihitaji na hivyo uchovu, kichwa kuuma nk lazima itokee.
 
Sasa AC ya kazini ina tofauti gani na kwenye gari na kwenye bus na kwenye ndege.

AC masaa yote kumbe mshika remote umeweka 29, yaani hapo ni kama umezima tu, ila ili usionekane mkuda umewasha kizushi.
Tumeshaongea kwenye hoja huko mbele mkuu. Nyumba esp magorofa kuna vents na space za kuingiza hewa ndani unakuta oxygen ya kuchakatwa na AC ipo ya kutosha.
 
Naunga hoja mkono.
 
Ni kweli kabisa.mimi Huwa nakosa amani kabisa kukiwa kumefungwa vioo.Ukute na watu siyo wastaarabu mwingine anunue chips na samaki anakula humohumo.Mimi Huwa nikikosa kiti Cha kwenye dirisha Huwa sisafiri.Bora watengeneza mabasi ya masafa marefu wabuni mfumo mwingine wa kuingiza hewa kama yalivyo mabasi ya mwendokasi ambayo unaweza kufungua madirisha ya juu na hewa inapita vizuri kabisa
 

Umegusia hoja muhimu sana mkuu. Mabasi mengi yenye Air Conditioner (AC) mara nyingi hayategemei upepo wa nje moja kwa moja. AC huchukua hewa ya ndani ya bus, kuipoza na kuirudisha tena (recirculation).

Kwa hiyo kama mfumo haujawekwa “fresh air intake” vizuri, hewa ile ile ndiyo inazungushwa. Hii husababisha ndani ya muda mfupi oxygen kupungua taratibu na carbon dioxide kuongezeka kwa sababu ya watu kupumua kwa pamoja. Ndiyo maana abiria wengi huanza kuhisi kuchoka, kizunguzungu au hewa kuwa nzito.

Matatizo yanayotokea kwenye hayo mabasi ni:

1. Oksijeni kupungua kitu kinachosababisha mwili unachoka haraka, na usingizi mzito.

2. Carbon dioxide kuongezeka na kusababisha mtu kuanza huhisi kichwa kuuma, kushindwa kufikiria vizuri.

3. Magonjwa ya kuambukiza kwa sababu hewa inazunguka humo humo, mtu mmoja mwenye mafua au kikohozi anaweza kuwaambukiza wengine kwa urahisi.

Mfumo wa AC unatakiwa uwe na kipengele cha kuingiza fresh air kutoka nje, siyo recirculation pekee. Mabasi mapya yenye viwango vya kimataifa huchanganya fresh air angalau 10–20% kila mzunguko.

Safari ndefu zenye watu wengi (abiria 40–60) zinahitaji uingizaji wa hewa safi mara kwa mara. Hii ndiyo sababu ukiwa kwenye ndege, kuna mfumo maalumu wa kuchanganya hewa mpya ya nje na ile iliyopo ndani.

Ikiwa AC haileti fresh air, basi ni bora vioo vifunguliwe mara kwa mara ili kuwe na mzunguko wa hewa wa asili.

Kuhusu bus zenye vyoo ndani. Vyoo ndani ya bus vinaweza kuwa “udhia” zaidi kuliko maendeleo kama havijasimamiwa kitaalamu. Kwa sababu, harufu na bacteria huweza kuchanganyika na hewa ya ndani, hasa kama ventilation si nzuri. Usafi mara nyingi huwa changamoto kwenye safari ndefu. Kwa hiyo, kama hakuna mfumo mzuri wa hewa, basi kweli abiria wanaweza kuhisi hali mbaya zaidi.
 
Haya maelezo nimempa kutoka kichwani kwangu. Ila haelewi na hataki kuelewa.
 
Daah yaani uchafu wa Yutong ufanansihe na bus moja linalogharimu zaidi ya 1B aisee hayo mayutong ajali kidogo tu utasikia watu kadhaa wamekufa gari halina hata Kinga yeyote kwa abiria wake..
Wazambia walikua nyuma kwenye Usafiri wa abiria ila Bus wanazotumia sasa hivi sisi ndio tupo nyuma tena...
 
Ikiwa hali ya nje ni Jua kali la mchana inasaidia, nje ya hapo sioni sababu ya kutumika AC kwa mida ya jioni na usiku au masiku ya hali ya hewa ya wastani.
 
Wewe Kuomitang acha kufananisha Irizar na makopo ya kubebea watu hayo Yutong.
Yutong na BYD zinanunuliwa zaidi sana hapo Ulaya kuliko Irizar
Higer ndio basi pendwa zaidi Zambia
 
Yutong na BYD zinanunuliwa zaidi sana hapo Ulaya kuliko Irizar

Higer ndio basi pendwa zaidi Zambia
Zambia wanatumia bus zenye bodi ya Brasil na Spain jamaa zetu wapo na Shalom au Likili Bus na yule mzee wa Jordan wote wapo na bus za bei kwa sababu kwao kodi ni ndogo Wazambia wana Bus double decker inakuja SA na ndani seat za ngozi ina zaidi ya Mika kumi Jordan huyo..
 

Maskini ni walalamishi muda wote. Hujawahi panda ndege wewe
 
Ndege zina mfumo maalumu wa kuchakata, kuingiza oxygen na kutoa hewa chafu nje unaoitwa Environmental Control System(ECS).
Kaka nakuheshimu ila huu naona ni utetezi tu 😄
 
Higer na brands nyingine za Kichina kama Zhong zinanunuliwa zaidi Zambia
 
Ndege zina mfumo maalumu wa kuchakata, kuingiza oxygen na kutoa hewa chafu nje unaoitwa Environmental Control System(ECS).
nimemshangaa anafananisha pipa la angani na mabasi mabondo ya mchina
 
Upo sahihi mkuu, mfumo wa Air conditioning unataka usafi sana. Mabasi mengi Tanzania fundi anafanya daily check up ya Engine na sehemu nyingine. Kwenye basi za masafa inatakiwa kila Siku Ac cabin filter iwe inakaguliwa na kupulizwa uchafu, pia Ac ufanyaji kazi wake inachukua hewa iliyopo karibu na basi na bado mabasi mengine unakuta lina AC ndani usafi kwenye stand carrier, floor si mzuri. Basi inatoa moshi safari nzima ile hewa ya ukaa jua mtaivuta asilimia fulani, njia za vumbi,stand za vumbi

Pia kwa nchi zilizoendelea basi inayotoa moshi haikidhi kuwa road worthiness na kuna tozo kwa kila carbon gari inayotoa kwa mwaka
 
Hakuna kitu kizuri kama hewa ya Mungu.

Najitahidi kuavoid mabasi kwa kadri niwezavyo, ila ndio hivyo kuna muda inabidi tu.

Binafsi nikiingia tu nikakaa kwenye bus hiyo harufu ni kama nimeikariri hata kabla AC hazijawashwa Kichwa changu kinakuwa kizito balaaa, kifua kinaanza kujaa na tumbo linaanza kuvuta 😅

Bahati mbaya hata kwenye ndege zetu hizi siku hizi kuna kiharufu kimenikaa kinanichanganya 🥹
 
Mabasi yana mifumo tofauti ya AC.
Mabasi mengi tunayotumia Tanzania kwa sasa mfumo wake ni belt driven pulley kutoka kwenye engine ya Gari.

Mifumo ya Ac kwenye mabasi ipo aina 3.
1.Belt driven pulled
Huu ni mfumo wa Ac uliozoeleka na wengi unatumika kwenye gari ndogo na kubwa. Ambapo AC Compressor inatumia pulled kutoka kwenye engine.

Hii mapungufu ni pale gari kukosa nguvu, belt kulika, dereva kuzima kuhofia gari itaongeza ulaji mafuta.

2.Auxially engine for AC
Kuna basi mfumo wake wa Ac hautumii engine inayotumika kuendesha gari. Hizi zinakuwa na engine nyingine ndogo ambayo hutumika kwa ajili ya kuendeshea AC tu. Hizi AC zina ufanisi mkubwa sana na gari hizi zinatumika kwenye baridi kali na joto.

Mitsubishi fuso zile basi za engine nyuma zina auxiliry engine kwa ajili ya Ac zinafungwa nyuma pembeni engine ya 4m40, Isuzu wao waliweka 4jb, Scania basi zao wao wanatumia Dc9. Kipindi Dar watu wanaziagiza sana Fuso na Isuzu za engine nyuma baadhi ya magenta na mafundi walikuwa wanazichomoa auxiliary engine wanauza wamiliki wengi walikuwa hawajui kama gari inakuja na engine ndogo ya ziada kwa ajili ya AC


3.High Voltage AC
Hii ni kwenye basi za kisasa za umeme
 
Una uhakika gani anakuwa amesahau ku switch on na sio kwamba haipo kabisa au hajawasha kwa makusudi kwa sababu zake binafsi au kubana matumizi ya bus?
mkuu kama AC ipo on na unaona hewa nzito the thing ni kwamba kunafanyika circulation ya hewa ambayo ipo ndani ya bus tuu hamna hewa inavutwa kutoka nje na ndio maana nikakuambia lazima dereva hajaswitch from internal circulation to external circulation na hii inaweza kua kasahau au hajui mfumo wa ac unafanyaje kazi yeye akiingia ndani ya bus anawasha tuu AC basi anaendelea na safari. Ila hamna manufacturer ambaye anaweza kutengeneza bus halafu akaweka mode moja tuu NO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…