Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Kiuhalisia ni kwamba mara nyingi watu wamekua wakisema Mungu ni roho, namimi nakubaliana na hii kauli ya kwamba ni kweli Mungu ni roho, lakini tujiulize kidogo je, Mungu ni roho kwa namna gani? Kwa maana maandiko husema ya kwamba sisi tuliumbwa kwa mfano wake.
Kwahiyo kama sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu basi sisi ni kopi yake, na kama sisi ni kopi yake basi hakuna chochote kilicho kwetu kikawa hakipo kwake ingawa yawezekana yapo yaliyo kwake yakawa hayapo kwetu kwa maana kopi haiwezi kuwa sawasawa na ile halisi kwa asilimia mia moja ingawa kopi kimuonekano haiwezi kutofautiana na halisi.
Sasa hoja hii inaenda kupingana na ile hoja ya wale ambao wanaamini ya kwamba Mungu ni roho tupu isiyo na mwili kwa maana ukiachana na hii hoja lakini pia ukisoma maandiko katika kile kitabu cha mwanzo utagundua ya kwamba Mungu si roho tu pekee bali nayeye ni roho iliyo ndani ya nyama.
Maandiko yanasema hivi "roho yangu haitashindana na mwanadamu kamwe kwani yu nyama na yeye, Kwahiyo miaka yake itakua 120".
Hilo neno la kwani yu nyama na yeye inamaana ya kwamba Mungu angeweza kushindana na mwanadamu kama tu angekua na roho tupu ila kwakua mwanadamu anao upande wa kiroho na upande wa nyama kama vile Mungu alivyo basi inakua ngumu yeye Mungu kushindana nae.
Yu nyama na yeye inamaana ya kwamba na yeye ni nyama kama mimi.
Na andiko hilo hilo ukiendelea kulitafakari zaidi utagundua ya kwamba Mungu anaweza kumuendesha binadamu katika ule upande wa kiroho pekee ila unapokuja upande wa damu na nyama Mungu anakua hana uwezo wa kumuendesha mwanadamu.
Kwahiyo hii inamaanisha kwamba mambo yote yafanyikayo ndani ya mtu kupitia upande ule wa kiroho huwa Mungu anayajua moja kwa moja ila yale ambayo hufanyika katika upande ule wa kimwili huwa Mungu hayajui.
Na hii ndio sababu iliyopelekea Mungu amuhofie mwanadamu kwa maana ni ngumu kujua ya kwamba yale ayawazayo katika upande wa kiroho ndiyo ayawazayo katika ule upande wake wa kimwili kwa maana ya ule upande wa damu na nyama.
Kwa kulithibitisha hili kwenye maandiko ya kiimani kuna historia ya bwana mmoja anaitwa Ayubu, huyu mtu alikua ni mtu bora sana mbele za Mungu kwa maana upande wake wa kiroho haukua na shida yoyote hadi kufikia kiwango cha Mungu kujivunia yeye lakini licha ya kwamba Mungu alikua anajivunia yeye ila bado hakuwa na hakika na ile KWELI iliyo ndani yake kwa maana maandiko yanasema tumuabudu Mungu kwa ROHO na KWELI Sasa huyu bwana Ayubu ni kwamba kwenye upande wa ROHO alikua vizuri mbele za Mungu ila ile KWELI ndio ilikua inampa mashaka Mungu hadi kupelekea kumpa majaribu ya kimwili ili aone je yaliyopo rohoni mwake ni sawa na yale ambayo yapo mwilini mwake?
Lakini pia ukisoma maandiko hayo hayo kuna swali Yesu aliwauliza wanafunzi wake ya kwamba je, watu wanasema mimi ni nani?
Kikawaida ni kwamba kwa namna ya kiroho Yesu alijua vile watu wasemavyo kuhusu yeye ila kwa namna ya upande ule wa damu na nyama hakuwa anajua chochote na ndio maana alitaka apate uhakika ya kwamba je yale ya rohoni mwao ni sawa na yaliyopo katika ule upande wao wa kimwili?.
Kwa maana maandiko yanasema Mungu anataka kuabudiwa kwa ROHO na KWELI, kwa maana ni rahisi sana mtu kumuabudu Mungu kwa roho ila akashindwa kwenye kweli, kwa maana kumuabudu Mungu kwa roho ni kuwa mnyenyekevu mbele zake ila kwa kweli ni kuyaskia yale yote ya rohoni na kuyafuata kwenye upande wa mwili kwa maana ya kwamba ili uwe unamuabudu Mungu kwa roho na kweli nilazima uiruhusu roho yako iuongoze mwili, uiskie ile sauti ya ndani mwako na uifuate kama ambavyo inavyokuongoza na hapo ndipo utakapoweza kumuabudu Mungu kwa roho na kweli.
Kwa maana nyingine ni kwamba Mungu anataka akuongoze si wewe ujiongoze mwenyewe kwa kufuata yale maamuzi yatokayo katika upande wako wa damu na nyama.
Ni sawa na wewe hapo ukitengeneza robot lako hautataka lijiongoze lenyewe bali utataka uliongoze na ikitokea likaanza kujiongoza basi kuna namna hautajiskia vizuri.
Kwa hiyo Mungu ni kama rubani wa chini ila wewe yaani huo upande wako wa damu na nyama ni rubani wa ndani ya ndege kwa maana ili ndege iweze kwenda na kufika salama ni lazima rubani wa ndani ya ndege amskilize rubani wa chini kwa maana rubani wa chini ndiye anaejua mifumo yote ya anga pamoja na namna inavyokwenda Kwahiyo akisema shuka chini kidogo rubani wa ndani ya ndege anatakiwa ashushe ndege chini kwa kiwango alichoambiwa akisema aelekee mashariki basi anapaswa kufanya hivyo na kadhalika, Sasa ikitokea yule rubani wa ndani ya ndege akapuuzia sauti inayotoka kwa rubani wa chini basi moja kwa moja ndege inakuwa hatarini kwa maana rubani wa ndani ya ndege hajui mifumo ya anga Kwahiyo hali ya anga ikibadilika kidogo basi ndege itayumbishwa na itaanguka.
Lakini pia mawasiliano yakipotea baina ya rubani wa anga na rubani wa chini huwa ndege inapotea kwenye lada na ikipotea kwenye lada mifumo ya anga iliyopo chini huwa haiwezi kujua wapi hiyo ndege ilipo na ndio sawa sawa na mwanadamu pindi atakapoacha kuiskiliza sauti ya rohoni mwake na kuiskiliza sauti ya kimwili huwa ni rahisi sana kuishi maisha yaliyo nje ya hatima na ukiuacha mwili uiendeshe roho yaani mwili uifunze roho namna sahihi ya kuishi basi hapa mtu anakua amepotea katika ile mitetemo ya kimungu kwa maana yoote atakayo kuwa anayafanya kwa maana ya kimwili huwa hayaonekani katika mifumo ya Kimungu.
Na ndio maana watu husema Mungu ni roho kwa maana ya kwamba uwezo wa Mungu kuyajua yote yakiyomo ndani ya mwanadamu huwa unaishia katika upande huo wa kiroho ila ukija kwenye upande wa kimwili hawezi kujua.
Mambo haya ni kama hii teknolojia ya AI, ni kwamba mtu anapotengeneza robot huwa analiwekea command ya kwamba liwe na uwezo wa kufanya moja mbili tatu, lakini ukiacha nafasi ndani ya robot na kulipa uwezo wa kuweza kuhifadhi na kujifunza mambo mengine mapya kutokana na mazingira huwa ni ngumu kwa mtu aliyelitengeneza kujua ni mambo mangapi robot hilo litakua limejifunza kutokana na mazingira ukiachana na yale ambayo yeye aliliwekea ndani yake wakati analitengeneza.
Na teknolojia hii kwa kadri inavyokua na ikija kufikia kwenye hatua ya kuweza kuyapa haya marobot uwezo wa kuamua kwa maana ya ule uwezo wa kujua mema na mabaya kama ambavyo mwanadamu alipewa huo uwezo pale bustanini na wale wana wa Mungu ambao walikuwepo pale basi hapo ndipo ugumu utakapokuwepo kwenye kuyaongoza haya marobot kwa maana yatakua na pande mbili yaani upande ule wa zile command yaani amri ambazo waliwekewa wakati yanatengenezwa lakini pia yatakua na ule upande wa kumbukumbu zao binafsi ambazo zinahifadhiwa ndani yao kutokana na mazingira waliyopo sasa wakiyafanya yale yaliyo ndani ya command itakua rahisi kujua hatua inayofuata baada ya hapo ila yakifanya yale mambo yaliyo nje ya zile command kwa maana yakifanya yale mambo ambayo yenyewe yamejifunza inakua ngumu kujua ni nini kinafuata baada ya hapo na ndio hapa ambapo watu husema kwamba linakua linabehave tofauti na vile ilivyo tarajiwa.
Kwahiyo hii teknoloji bado iko katika kiwango cha awali kabisa kwa sasa hapa duniani au ulimwenguni kwa ujumla ila kwa kadri siku zinavyokwenda itaendelea kukua na itafikia pahala dunia yote itakua inaiogopa hii teknoloji kwa maana vitu tutakavyo vizalisha vitatushinda kwenye kuviongoza kwa maana vitakua na uwezo wa kujiendesha venyewe na kuanza kuwa na maamuzi yake binafsi na hapa ndipo tutakapojua au kugundua kwamba tabu tutakazo zipata kupitia hizo robots ndizo ambazo waliyo tuumba wanazipata.
Kwakusema hayo naomba nihitimishe hili andiko langu kwa kusema hili neno la Mungu ni roho na si mwili linamaanisha kwamba uwezo wa Mungu kuyaona yaliyomo ndani ya mtu huishia kwenye ule upande wa kiroho ila ukija upande wa kimwili hana anachokijua.