Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Kwa hiyo turudi kule kule kwenye sayansi kuwa "In every action there is equal and opposite reaction" 🥱

Lakini mkuu kama Mungu ndiye alimfanya Lucifer kuwa shetani kwa nguvu zake mwenyewe basi kazi yake itakuwa haina maana.

Kwa sababu kwa muktadha wako wewe even now Mungu ndiye anae ku-control

Utende dhambi ama usitende,uende mbinguni ama jehanam, yaani kana kwamba sisi hatuna free will tena isipokuwa Mungu ndiye anakifsnyia wewe maamuzi kwa free will zake mwenyewe.

Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri lakini.
 
Hujaelewa nini? Maana ili useme kina makosa lazima uwe na reference for comparison hapa hatuna reference ya Mungu kumuumba binadamu timilifu au sio timilifu ili utuambie Mungu kakosea tupe reference ya utimilifu!
Vyovyote vile. Lakini hatakiwi kumuadhibu mtu kisa makosa yake mwenyewe. Unamuumba mtu na nyege afu akifanya mapenzi Ni dhambi mpaka sijui ndoa. Hizi sheria Ni za makabila ya kale sio Sheria za muumba yote
 
Hujaelewa nini? Maana ili useme kina makosa lazima uwe na reference for comparison hapa hatuna reference ya Mungu kumuumba binadamu timilifu au sio timilifu ili utuambie Mungu kakosea tupe reference ya utimilifu!
SIna reference ya kwenye Biblia lakini tufanye tu mfano wa kibinadamu.

Kama Adam angeumbwa akiwa na option ya utii pekee bila kuwekewa option ya uovu pembeni basi huyo Adam angekuwa mkamilifu/timilifu sana.

Pia angekuwa hasinzii,hachoki,hahisi njaa n.k
 
Hakuna zawadi ya kuishi bila kuiba? Amri ya usiibe ina maana gani kama usipoiba hakuna adhabu. By the way sijasema kila kitu lazima kiwe na zawadi na adhabu. Jibu kufuatana na kinachoongelewa, tafadhali. Tusianze mada juu ya mada.
Hahaha bac we mi mjinga kwa hio Kama hamna adhabu ya kuiba na kuuwa wewe utaiba na kuua. Bac we una matatizo ya kisaikolojia. Binadamu tuna nature ya huruma na ndo maana siku hizi mauaji na Vita zimepungua kuliko zamani. Na nchi za dini ndo zinaogoza ufisadi na mauaji kuliko zisizo na dini.
 
In short hizi dini zinajaribu kufanya mwanadamu aonekane kiumbe kibaya wakati Ni nature. Imagine wanyama wanaonyesha dalili za ushoga lakini Mungu hajawapa roho na hawapewi adhabu. Hii inaonyesha kwamba Sheria za dini Ni za binadamu kwa sababu hamna kitu ambacho kiumbe chochote anafanya ambacho sio natural.
 
Wewe umejuaje SUPER GOD ni mmoja????? USHAWAHI KUMUONA AU UMEKARIRISHWA????Na una tofauti gani kiimani na hao wabudha na wahindu??????? KIPI KINSCHOKUFANYA UJIHESABIE HAKI NA KUWAHUKUMU WAO????
Twende pole pole acha ku-panic.
Swali la kama nimewahi kumwona Mungu ni ni wapi na yukoje ni suala lisilo na msingi kwa sasa kwa sababu wapo wenye akili kubwa zaidi yako ambao washauliza hayo maswali na hawana majibu mpaka.

Kama unaona hapa tunajadili Mungu, basi lazima ujue kuwa tunajadili kiumbe asiyeonekana kwa kutumia milango yetu ya fahamu, na kama wewe umekuja hapa kumuuliza Mungu anaonekana kwa macho basi wewe hata hiyo Idea ya Mungu bado huna na unapaswa kutupisha.

Na kingine kuhusu nimejuaje kuwa kuna SUPER GOD MMOJA TU, nafikiri dini za kale na kubwa zote duniani kama za Kina Ibrahim,Kiebrania/kiyahudi,ukristo,uislam zote hizi zinam-preach SUPER GOD mmoja ambae ni muumbaji wa kila kitu.

Kama mungu hana alichoumba basi huyo siyo Mungu ni miungu, mfano kama hizo sanamu za kihindu na budha hizo ni miungu ama mizimu kwa lugha rahisi
 
Mkuu wahindu na wabudha wamekuepo hata kabla ya huyo ibrahim na walikua na dini zao au hujui mkuu???? Na unajuaje mungu aliumba wakati haukua nae umesimuliwa tu??????? UNATAKA KUMJUA MUNGU ILA KILA IMANI DUNIANI INA MUNGU WAKE NA NDIO MAANA TARATIBU ZA KUSALI ZIPO TOFAUTI.Mungu wa waislamu sio Mungu wa wakrsto na wayahudi na Mungu wa wahindu sio Mungu wa Wabudha.Mungu wa makabila yote ya kibantu sio Mungu wa dini za wakoloni wa kiarabu na kizungu waliovamia afrika.........!!!!!WEWE UNATAKA KUMJUA MUNGU YUPI MAANA KILA IMANI DUNIANI INASEMA MUNGU WAKE NI SUPER GOD?????
 
Mkuu kila dini duniani ina sanamu either za wanyama au maumbo kama watu,nyota,mwezi,misalaba na kadhalika au hujui????
 
Wahindi hawaabudu ng'ombe wanamiungu Yao Krishna, Shiva, wengineyo. Soma historia za dini za wenzako ndo uzijudge sio unaongea kwa hisia
Any way labda tutoe neno 'kuabudu' na badala yake nikwambie kuwa ng'ombe ni kiumbe/mnyama mtakatifu mno na anapewa heshima maalum katika imani ya kihindu.

Ndiyo maana wahindu wenye imani kali ukionekana unamchinja ng'ombe nchini India utaishia jela ama kuuwawa kabisa.

Lakini pia uitaja miungu yao hapo, sawa uko sasa na pia iko miungu mingi zaidi ya hiyo uliyoitaja wewe miwili.

But the issue is SUPER GOD ambae ni mmoja tu na sifa yake kuu ni muumbaji wa kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana ulimwenguni.

Huyo ndiye amabae tuna-focus zaidi tumjue kama yupo kweli ama tulipigwa.
 
Dini za kale kubwa duniani ni hindusim na budha na african religiou,s.Ambazo nyinyi wafuasi wa dini mpya mnaziita hizi dini upagani,kama ishara ya dharau juu ya imani zao
 
Mkuu kila dini duniani ina sanamu either za wanyama au maumbo kama watu,nyota,mwezi,misalaba na kadhalika au hujui????
Hata kama zipo lakini ni makosa kwa mujibu wa SUPER GOD, maana yeye kasema tusijifanyie sanamu ya mfano wa yeye au chochote kilicho juu mbinguni au chini duniani.
 
Mpaka siku akijitokeza ndio utapata jibu.Kwa sasa kila dini inavutia upande wake.Subiri siku ajitokeze kama yupo mkuu
 
Hata kama zipo lakini ni makosa kwa mujibu wa SUPER GOD, maana yeye kasema tusijifanyie sanamu ya mfano wa yeye au chochote kilicho juu mbinguni au chini duniani.
Waislamu wana sanamu za maumbo ya nyota na mwezi na wakrsto wana sanamu za watu na misalaba na wahindu pia wana sanamu na Wabudha pia wana sanamu.Na dini zetu za kiafrika kuna sanamu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…