Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Sasa wewe ukitaka kuifanya Ile story iwe kweli inabidi uweke miujiza kila sehemu kwenye wanyama kuishi mule, chakula chao kuenea, mimea kukua gizani vitu vingi. Sasa Kama Ni muweza yote si angefumba na kufungua na hao watu wabaya wangekufa au angewafanya wawe wema. Ila hii story imetengenezwa na watu wasioelewa Sayansi. Nitajie miujiza unayoijua wewe ambao Ina udhibitisho wa kisayansi na kihistoria. Sio unasoma hadithi za watu afu unataja Kama point za Historia.
 
Kuhusu Dunia au other heavenly bodies in the universe kuzunguka bila kugongana, umejuaje kama hazijawahi kugongana hapo kabla??

Inawezekana hizo bodies ziligongana sana hapo mwanzo, Hadi ikafika kipindi Bodies zote Zika obey kanuni Fulani ambayo ilikuwa strong.

Pia hadithi za biblia kuhusu uumbaji, zinaibua maswali kuhusu Mahali alipokuwa amekaa Mungu akifanya huo uumbaji.

Ukisema Mungu alikuwa (mf. Mbinguni) wakati anafanya uumbaji. it means, Mbingu ilikuwepo kabla ya Mungu au mbingu ndiyo ilimtoa Mungu. Ukisema hakua sehemu yeyote, unamaanisha Mungu hayupo
 
Dini imekufungia ufahamu wewe ndo maana we huwezi elewa kwamba vimetungwa. Ukitaka uelewe jifanye hujui chochote kuhusu dini afu uifuatilie ndo utaelewa kwamba imetengenezwa na watu na haina ukweli. We unadhani kwa Nini unafundishwa dini utotoni ili iwe rahisi kuamini. Na mtu mzima anaamini dini kwa miujiza feki ya wachungaji na sio story za watoto za Biblia
 
Na hapohapo unajiuliza kama kweli Mungu anataka watu tumuelewe, kwanini atumie lugha ya mafumbo?
 
Ngoja kwanza wapi huko pamesema malaika hana utashi.

Kabla sijaendelea
Mkuu hilo ni somo lingine tena maana lina involve quotes kadha wa kadha katika Bible kutetea point ya kusema Malaika hawakuwa na Freewill

Kitu cha kutambua ni kwamba, Malaika wameongelewa tofauti kidogo kwenye hizi Imani mbili, Islamic na Christian

Katika Christian kupitia baadhi ya maandiko inaonesha kuwa Mwanzo kulikuwa na Malaika tu pasipo kuwa na Shetani, ila Shetani alikuja baada ya Malaika Gabriel kumpinga Mungu ndio akapatikana Lucifer

Kwenye Islamic inaonekana kuwa tangu mwanzo kuna Malaika na Shetani, Malaika huku ndio rahisi kaelezewa kuwa ye hana freewill ispokuwa anafanya kile ambacho anaagizwa na Mungu tu

Katika Islamic, Shetani yupo tangu mwanzo na ameumbwa akiwa na freewill hivo anaamua fanye kipi na kipi asifanye, na katika Islamic Shetani alilaaniwa baada ya kukataa kumsujudia Adam

ila kabla ya kulaaniwa bahati mbaya me sijui alikuwa na majukumu gani Duniani hadi kupelekea yeye kuumbwa na Mungu since day one

Kwakuwa unaonekana sio mvivu wa kusoma basi ningeomba ujaribu kusoma pia kuhusu issue ya freewill kwa Malaika katika Dini ya Christian maana huko ndio naona Uzi wako umebezi sana
 
Kwahiyo unadhani wewe ndio kiumbe pekee uliyeumbwa na Mungu
Mungu kaanzisha ulimwengu... Kaweka kanuni zake na mazingira yakajiendeleza. Nimezaliwa kwa wazazi. Ila hao majini Kama unayo Ni wewe tu na wenzako. Mi Sina jini, hamna ushahidi kuonyesha Kuna majini so sijui kwa Nini unaamini. Ni sawa na kuamini ma vampire, ma zombie, ma dragon, zote Ni fikra za binadamu.
 
Uko Islam Sina imani nako ila sio hoja

Kwa mjibu wa Islam shetani akua malaika bali Ni viumbe wa mwanzo kabla yetu ambapo wenzake walikaidi wakateketezwa ila yeye alichukulia baada ya kukutwa anasujudu to cut off the story baadae alileta ubishi akatupwa duniani ila mimi Sina imani na kitabu hicho kwa misingi binafsi

Kwa upande wa Bible haijaelezea vyema juu ya life staili nzima ya malaika

Zaidi ya shetani kuwa na cheo na baadae kukengeuka na kisha kutupwa duniani na wafuasi wake.

Kurasa zingine walionekan katika majukumu yao tu.

Hilo la freewill wewe umepata wapi?
 
1.Nenda kaone nguzo ya chumvi (mke wa rutu)
2.nenda kaangalie mabaki ya safina ya nuhu huko milima ya Ararat uturuki.
 
Duuh...bado naendelea kujifunza Mengi
 
1.Nenda kaone nguzo ya chumvi (mke wa rutu)
2.nenda kaangalie mabaki ya safina ya nuhu huko milima ya Ararat uturuki.
Hebu ingia Google uzisearch afu uone zipo ngapi.. hayo mabaki Wanayosema sio ya ukweli na hio nguzo Ni ndefu Kama mnazi haiwezi ikawa mtu. Hizi Ni Sayansi feki za dini. We ingia Wikipedia uone Kama hizo sehemu Ni halisi.. Ni vivutio tu vya utalii bac.
 
Radi si umeme wewe..au hujawahi ona rad
Sijaelewa radi imeingiaje hapa. Lakini pia unajua umeme wa radi na muungurumo wake unatokana na nini? Jitahidi kutafuta maarifa itakusaidia kuelewa. Umeme ni umeme tu haijalishi wa jua, wa radi wa betri au wa Kidatu.

Afu hapa hatuzungumzii uwepo wake
Hauzungumzi wewe na nani? Mimi sijazungumzia uwepo wa Mungu ambao mimi najua haujadiriki kwa kuwa yupo upende au usipende.

Nimejikita kujibu hoja za mleta uzi pengine kwa imani yake yaweza kumfaa au isimfae. Ndio maana nimejibu swali au hoja moja baada ya nyingine.
Tunazungumzia ukweli wa story za Biblia.
Stori za Biblia hapa tena zinatoka wapi? Hakika nakwambia ukiishi kwa msisimko wa stori za Biblia bila kujua wewe na Mungu ni kitu kimoja katika uhusiano wa baba na mtoto au Muumba na kiumbe umepotoka. Story za Biblia hazitakaa zikusaidie kitu zaidi ya ujuaji usio na tija. Acha zibadili tabia uuishi uwepo wa Mungu maishani mwako
 
umekaribia kuchanganyikiwa kwa kujifanya great thinker. Kafanye shughuli zitakazokuletea mkate
Na kweli huwa nikianzaga kuwaza/kujiuliza haya maswali huwa naanzaga kuhisi kama Mind yangu ina Collapse/lose cotrol/stability.

Naanzaga kuona hakuna ninachojua chochote kuhusu huu ulimwengu, kila kitu ulimwenguni naanzaga kuona ni ubatili mtupu.

Naanzaga kuona kana kwamba ulimwengu ni fake, kila kitu fake, ni kama wahuni tu wachache wamekaa wakaamua kutuletea sheria za kutuongozea ulimwengu kwa ajili ya maslahi yao wanayoyajua wenyewe.

It's like every thing in this world is an illusion
 
Ndugu achana na ujinga wa dini. Hata wewe unaweza anzisha ya kwako

Mjue Mungu wako, na bahati nzuri hauhitaji kwenda kanisani au msikitini kwenye dini zako kumpata.

Lakini pia hapa hatuongelei dini. Tunamzungumzia Mungu muumba.

Jikite kwa mada.
 
Kwa Nini kuwe na designer? Na kwa Nini awe mtu.. na ukiulizwa aliyemdesign huyo mtu.. utajibuje
By the way labda nimetumia mtu kwa sababu ya mazoea.

Labda nibadili lugha niseme kutakuwa na kiumbe ambaye ame-design huu ulimwengu bila kujali ni kiumbe wa aina gani.

Na huyo designer lazima atakuwa ana ufahamu/maarifa kutokana na ukweli kwamba ulimwengu uko fashioned sana.

Sasa huyu designer kama ataitwa Mungu au nani hapo ndiyo sijui, ila nadhani designer yupo.

Na nasema designer yupo kwa sababu kuu moja kwamba "Ulimwengu wetu huu/universe kila kitu kipo katika mpangalio/system maalum na unajongea (uko kwenye mwendo) na kila kitu kinapita katika njia yake bila kukosea au kugongana na mwenzake.

Ni hilo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…