Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Mkuu

Nije nikuchukue usiku nikuonyeshe roho zipo wapi???
Unatishia kuniua au. In short concept ya Roho imetungwa na watu kipindi kile ambao hawakuelewa Sayansi ya ubongo. Wanasayansi wamegundua Hilo kwa kufuatilia watu wenye matatizo ya ubongo, mapacha walioungana na kadhalika. Wakagundua akili ikifa na kila fikra na uamuzi huishia hapo.
 
Sio kukuua mkuu,bali nakupeleka makazi ya hizo roho mkuu.
 
TUKUFUNZE KUHUSU MUNGU YUPI SASA??????MUNGU WA KIARABU AU MUNGU WA KIYAHUDI AU MUNGU WA KIHINDU AU MUNGU WA KICHINA AU MUNGU WA KIBANTU??????
Ndo maana nasema tuachane na hizi dini tuamini tu kila kitu kilikuwepo na Kama kiliumbwa hatumjui na hatujui sheria zake na haingilii maisha yetu. Na hizi dini Ni Binadamu katika kujaribu kuelewa vitu wasivyovielewa.
 
Tufanye Binadamu tumweke pembeni maana yeye ana mwili.

Vipi kuhusu Lucifer na wenzake walioasi, maana wao ni roho pia (hawana mwili).
Binadamu siwezi kumweka pembeni ndio nachat nae hapa anatumia akili kusoma na kuelewa anachosoma na kuandika, anatumia utashi kufanya maamuzi, ana roho ambayo imebeba uhai wake na ndio huyo ananiuliza kuhusu lucifer anahitaji kupanua maarifa yake kuhusu ufahamu.
 
Sio kukuua mkuu,bali nakupeleka makazi ya hizo roho mkuu.
Kwa Nini usiku.. record video unitumie.. skia fuatilia Sayansi. Kuna kitu kinaitwa hallucinating..Ni kuhisi, kunusa, kusikia na kuona vitu ambavyo havipo. Ndo unaskia sijui mtu kaona jini, Mara katokewa na Mariam, zote Ni akili tu inakuchezea Ila sio kila kitu unachokisense Ni Cha ukweli. Ndo maana vitu vya hivyo haviwezi kutokea kwenye camera na Kama Kuna video jua Ni edited.
 
Hi
Huko hakuna video mkuu.Kama unaogopa ucku bas twende kesho asubuhi mkuu.
 
Duuh...

Swali la Mungu alikuwa aliishi wapi kabla ya kuiumba MBINGU ambayo ni makao yake ni swali la msingi sana, na inabidi wataalamu wa haya mambo mje mjibu huku (ila kwa reference siyo kwenye fikra zenu).

Lakini mimi nikujibu hilo la heavenly bodies kugongana, probably inawezekana zamani viliwahi kugongana na hata wanasayansi wanasema hivo.

Na hata wana sayansi wa leo (modern scientists) wanatuambia kuwa miaka bilioni kadhaa ijayo hii galaxy yetu (milky way) itakuja kugongana na galaxy ya jiran (Adromeda galaxy) na bado ya mgongano huo itazaliwa galaxy mpya kwa jina lingine,lakini hakuna proof maana haijatokea bado.

Lakini pia, can you imagine kwenye galaxy yetu pekee (milky way) kuna kana kadiriwa kuwa na nyota kati ya bilion 300 mpaka bilion 500, pamoja na sayari zisizopungua bilion 100.

Sasa, hii galaxy yetu ni mojawapo ya galaxy ndogo sana, alafu fukiria idadi ya nyota zilizopo kwenye hiyo galaxy, fananisha na galaxy zingine kubwa zaidi ya yetu zitakuwa na nyota ngapi na sayari ngapi.

Alafu kumbuka galaxy zenyewe zipo nyingi sana, na kila galaxy ina ina mabilioni ya nyota na sayari.

Alafu imagine the whole observabale universe inakadiriwa kuwa na nyota siyo chini ya trilion 12.

Alafu wanasayansi wanakadiria kuwa "The number of stars in the universe is much bigger than all the grains of sand in the beaches on planet earth"

Na hivyo vyote viko kwenye motion, waweza nambia kama hivi vitu havina anayevidhibiti huoni kuwa vingekuwa vinagongana kila sekunde ?

Au hujaskia matukio ya Austronomy, wakisema kuwa "kuna jiwe kubwa la angani linakuja uelekeo wa dunia kuja kuiogonga la likiigonga dunia ndiyo maisha kwa heri" .

Lakini mara unashangaa wanatoa repoti tena kuwa hilo jiwe lililokuwa linakuja uelekeo wa dunia sasahivi limeshabadili mwelekeo siyo hatari tena kwa dunia.

We unadhani huo mwelekeo linabadilisha tu lenyewe bila mdhibiti ?

Kuna designer wa huu ulimwengu broo hata kama hatumwoni kwa macho.
 
Anaeiendeleza Kwa Serikali za Dunia Kwa tishio za sanctions ni Marekani,
Roman empire haijawahi force kuamini Imani zao na waliheshimu desturi za watu.
 
Upo sahihi sana, Kiranga unaamini kuwa Kuna designer wa Kila kitu, tukiachana na mambo ya dini?
Anyway Kuna muda ukiwaza sana lazima utakuja kwenye conclusion ya kuwa Yupo aliyedesign huu ulimwengu na kuweka sheria za kimahesabu katika ulimwengu huu na zinajiendesha zenyewe bila makosa yaani ziko programmed
 
Kwa nini unafikia conclusion hiyo?
 
Kwenye swala la uumbaji wa binadamu Mungu hakuumba binadamu aliyekamilika. Kumbuka Adam na Hawa walikuwa na mapungufu ya kutokuwa na uelewa juu ya mema na mabaya. Had hapo naweza sema walikuwa hawajakamilika
 
Kwenye swala la uumbaji wa binadamu Mungu hakuumba binadamu aliyekamilika. Kumbuka Adam na Hawa walikuwa na mapungufu ya kutokuwa na uelewa juu ya mema na mabaya. Had hapo naweza sema walikuwa hawajakamilika
Kama adam na hawa walikuwa na Mapungufu, hapo wa kulaumiwa ni nani kati ya Muumbaji na Waumbwaji 🫢
 
Exactly ukiwaza sana, huu ulimwengu uko programmed kama unavyosema 🫠
 
Anaeiendeleza Kwa Serikali za Dunia Kwa tishio za sanctions ni Marekani,
Roman empire haijawahi force kuamini Imani zao na waliheshimu desturi za watu.
Roman Empire nafikiri pia ameelezewa kwenye kitabu cha Danieli.

Kama.mnyama wa kutisha mwenye miguu ya chuma sijui, kwa mujibu wa wafasiri lakini 🫢
 
TUKUFUNZE KUHUSU MUNGU YUPI SASA??????MUNGU WA KIARABU AU MUNGU WA KIYAHUDI AU MUNGU WA KIHINDU AU MUNGU WA KICHINA AU MUNGU WA KIBANTU??????
Kumbe kila kundi lina Mungu wao tofauti na mwingine.

Any way achana na wahindu au budhah, hao wana miungu (wako wengi) siyo MUNGU.

Mimi nataka kujifunza GOD OF THE MOST HIGH (SUPER GOD).
 
Roman Empire nafikiri pia ameelezewa kwenye kitabu cha Danieli.

Kama.mnyama wa kutisha mwenye miguu ya chuma sijui, kwa mujibu wa wafasiri lakini 🫢
Yes Roman empire ilielezwa kwenye kitabu Cha Danieli.
Ila Marekani na Anguko lake Kwa tafsiri yangu binafsi, naona Ufunuo 17&18....
Marekani itaanguka na kuwa nchi ya kawaida although sijajua lini .
 
Kumbe kila kundi lina Mungu wao tofauti na mwingine.

Any way achana na wahindu au budhah, hao wana miungu (wako wengi) siyo MUNGU.

Mimi nataka kujifunza GOD OF THE MOST HIGH (SUPER GOD).
Yes Kila dini Ina Mungu wake
Waislamu wana Mungu wao.
Wakristo na Wayahudi Wana Mungu wao .
Wahindi Wana Mungu wao.
Wabahai Wana Mungu wao
Wa-Bantu Wana Miungu Yao, mfano Wahaya waliabudu Mungu asiyeonekana anaitwa Mukama ila mizimu kwao ni Malaika wema wanaosaidia matatizo madogomadogo yale makubwa wanampelekea Mukama asiyeonekana Wala kuchorwa.
Wasumeria walikuwa wanaabudu Enki na Enlil ambao inasemekana kuwa ni ma-aliens waliokuwa na uwezo wa ajabu.
Ila Designer yupo mmoja tu, shida tuliyonayo ni , Huyu ni nani? Kusudi la kutengeneza universe ilikuwa ni nini? Na pia je anajihusisha nayo au kaamua kuachana nayo?
Imagine tu system tu za mwili wako ukivotengeneza, imagine kuwa Simba, chui na wengine licha ya kwamba ni Mammalia ila hawana akili kama zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…