Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Biblia ina vitabu sitini na sita vilivyoandikwa na waandishi arobaini, kwa muda usiopungua miaka elfu moja mia sita. (1600) kutoka kiebrania na aramaic agano la kale na kigiriki agano jipya. Katika nyakati hizo kulikuwa na ukuaji wa lugha, mabadiliko ya tafsri, rejista nk. Ukumbuke sasa hivi kuna biblia ya wakatoliki, wasabato, mashahidi wa yehova nk. Yote ni sehemu ya mkanganyo wa tafsiri za kibiblia.
 
Hi
Huko hakuna video mkuu.
Kumbe kila kundi lina Mungu wao tofauti na mwingine.

Any way achana na wahindu au budhah, hao wana miungu (wako wengi) siyo MUNGU.

Mimi nataka kujifunza GOD OF THE MOST HIGH (SUPER GOD).
Kwanini umewabagua wahindu na wabudha????
 
Chakula kikiwa kibaya analaumiwa mpishi au chakula.
Mchoro ukiwa mbaya analaumiwa mchoraji au mchoro.
Ndo hivyo bro
Uzuri wa chakula au ukamilifu based on or influenced by personal feelings, tastes, or opinions. Ni subjective... ww huli pilipili na chakula chote kimewekwa pilipili unasema mpisha kakosea kupika wakati kwake huo ndio ukamilifu?
 
Hayo mambo yana mkanganyiko mkubwa sana.


Ila in short the God displayed in religious books (bible & quran) sio Mungu mwenyewe au nguvu iliyoumba ulimwengu mzima.

Maana vitabu vinasema mungu anajua hatima ya kila mtu hata kabla hajaumbwa kama ni wa kwenda mbinguni au jehanamu na bado anakuumba na kukuleta duniani hivyo hivyo.

Ni hivi, hakuna jema wala baya machoni pa mungu wa kweli sinche they are from within na anatupenda sana tu.
 
Hivyo vitabu mnavyosoma wajanja wenu akina Paulo wamevichakachua Kwa makusudi Ili kukupotezeni msifuate dini ya Mungu ila mfuate dini yao

Hi yapa the same story Mungu alimuhadithia nabii Musa baadae akaja kumuhadithia mtume Muhammad kuhusu wale malaika walioenda Kwa nabii Ibrahim kumbashiria mtoto Isihaka

Mwanzo 18:2
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
Mwanzo 18:3
akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Mwanzo 18:4
Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
Mwanzo 18:5
Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
Mwanzo 18:6
Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
Mwanzo 18:7
Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.
Mwanzo 18:8
Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Mwanzo 18:9
Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
Mwanzo 18:10
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.



Quran 51:24
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?

25
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.

26
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.

27
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?

28
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.

29
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!

30
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.


Bibilia inasema wale wageni Ibrahim alipowaandalia chakula walikula

Quran inasema walipoandaliwa chakula hawajakula na hapo ndipo Ibrahim alipojua kuwa wale ni malaika

Ukweli ni kwamba Malaika hawali chakula so hiyo story katika bibilia imechakachuliwa
 
Nani anaabudu ng'ombe...nitajie hii dini.
 
Uzuri wa chakula au ukamilifu based on or influenced by personal feelings, tastes, or opinions. Ni subjective... ww huli pilipili na chakula chote kimewekwa pilipili unasema mpisha kakosea kupika wakati kwake huo ndio ukamilifu?
Hivi umeelewa nachomaanisha. Chakula kikiwa kibaya au kina makosa analaumiwa mpishi au chakula.
 
Na ujumbe wa huyo Mungu mmoja huujui, hujui yupoje. Hujui anataka Nini, hujui atafanyaje, so usimpe sifa na sheria ambazo watu wa kale walimbunia.
 
Mkuu naona uko vizuri, hasa upande wa dini yako (uislam).

Na kweli unavyosema, mimi huwa nasoma maandiko mengi na mengine hata siyo biblia wala Qur'an lakini ni yahusuyo tu imani.

Sasa nikuulize tena kitu kimoja, nitatumia mbinu gani kupima kuwa hiki kitabu ni cha kweli na hiki siyo (mfano kati ya Qur'an na biblia) na ukizingatia vyote vinamzingatia Mungu muumbaji ?

Na je, unaweza kunambia kati ya Biblia na Qur'an ni kipi kilianza kuwepo ?
 
Nijaribu kukujibu. Kabla sijafanya hivyo nitoe angalizo kwamba maswali juu ya Mungu hayana empirical answers, isipokuwa logical answers. Ukilazimisha logical iwe empirical na kinyume chake basi ni vyema ukaacha kuamini uwapo wa Mungu na nguvu zake.

Swali lako juu ya shetani na nguvu zake: Uwapo wa shetani ndio unaodhihirisha uwapo wa Mungu, bila usiku mchana haupo, bila kulia kushoto hakutakuwapo. Bila adhabu zawadi haina maana. Kadhalika Mungu aliumba hao malaika, na moja akasaliti Mungu akamfanya awe adhabu ya milele itakayotofautisha walio wake na wasio wake. Ni kwa nguvu zake Mungu alimfanya Lucifer awe shetani, yaani nguvu kinzani. Na mara nyingi Mungu ameonyesha ushindi dhidi ya shetani. Ungeuliza pia kwanini Mungu anayesamehe kila Jambo hakumsamehe shetani, jibu ni hilo hapo juu: lazima kuwe na usiku ili tuujue mchana. Lazima kuwe na wovu tuujuwe wema. The two are separable but interdependent.

Swali kwamba Mungu alimpa Adam msaidizi dhahifu hadi akashawishiwa na nyoka kula tunda katazwa.

Ndugu, kwani aliyekuambia kwamba Adamu hakuwa dhahifu Nani? Unadhani Adamu alisamehewa dhambi kwasababu alipewa tu lile tunda? Wote walikuwa dhahifu na Mungu alijuwa hilo ndio maana akawaonya wasile tunda walilokatazwa. Yaani binadamu wote ni dhaifu tangu kuumbwa, kumbuka Mungu hakuumba binadamu kama malaika. Hata Yesu aliyeshuka kwa baba akavaa ubinadamu naye alikuwa dhahifu na akakili udhahifu wake mbele ya mitume wake.
 

Nafikiri kuna baadhi ya biblia za lugha zingine zina vitabu zaidi ya 66, kuna biblia zina vitabu hadi zaidi ya sabini na kitu na zingine zaidi ya themanini na kitu, vp kuhusu hilo ?

Na je, kama biblia original iliandikwa katika lugha za kiebrania,kigiriki na aramaic, ina maana kufasiri kuja kwenye lugha zingine za dunia ndiyo kunaweza kuwa kulipotosha maana halisi labda ?
 
Mbona sijakuelewa, sio kweli kwamba kila kitu kizuri lazma kiwe na kibaya. Mfano wizi una adhabu lakini hamna zawadi ya kuishi bila kuiba. Hizi adhabu na zawadi zimeletwa na dini ili kufosi watu kuamini vitu visivyoaminika.
 
Hivi umeelewa nachomaanisha. Chakula kikiwa kibaya au kina makosa analaumiwa mpishi au chakula.
Hujaelewa nini? Maana ili useme kina makosa lazima uwe na reference for comparison hapa hatuna reference ya Mungu kumuumba binadamu timilifu au sio timilifu ili utuambie Mungu kakosea tupe reference ya utimilifu!
 
Hi

Huko hakuna video mkuu.

Kwanini umewabagua wahindu na wabudha????
Wale wanaabudu miungu na masanamu siyo Mungu.

Ni miungu yao iko mingi, mfano hindu mpaka ng'ombe anaabudiwa, una kuna Mungu mke sijui na wana majina tofauti tofauti sana hao miungu wao.

Sasa mimi wale binafsi nawaona hawako upande wa SUPER GOD muumbaji amabe ni mmoja tu.
 
Uzuri wa chakula au ukamilifu based on or influenced by personal feelings, tastes, or opinions. Ni subjective... ww huli pilipili na chakula chote kimewekwa pilipili unasema mpisha kakosea kupika wakati kwake huo ndio ukamilifu?
Mfano wako mzuri
 
Hapo kujua hatima ya kila mtu kabla hajamuumba ndipo kunakoniumizaga kichwa pia 🤔🤔🤔
 
Mbona sijakuelewa, sio kweli kwamba kila kitu kizuri lazma kiwe na kibaya. Mfano wizi una adhabu lakini hamna zawadi ya kuishi bila kuiba. Hizi adhabu na zawadi zimeletwa na dini ili kufosi watu kuamini vitu visivyoaminika.
Hakuna zawadi ya kuishi bila kuiba? Amri ya usiibe ina maana gani kama usipoiba hakuna adhabu. By the way sijasema kila kitu lazima kiwe na zawadi na adhabu. Jibu kufuatana na kinachoongelewa, tafadhali. Tusianze mada juu ya mada.
 
Wewe umejuaje SUPER GOD ni mmoja????? USHAWAHI KUMUONA AU UMEKARIRISHWA????Na una tofauti gani kiimani na hao wabudha na wahindu??????? KIPI KINSCHOKUFANYA UJIHESABIE HAKI NA KUWAHUKUMU WAO????
 
Duuh...mkanganyiko ni mwingi aisee.

Lakini kabla sijakubali kuwa Biblia imechakachuliwa naomba nikuulize kitu.

Nnavyojua mimi kupitia haya haya maandishi ya kidini ni kwamba:Roho (mfano malaika au chochote cha kiroho) kinaweza kufanya chochote cha kimwili ikiwa tu na chenyewe kimejibadilisha na kuwa kwenye form ya mwili muda huo, sasa kama wale malaika waliomwendea Ibrahimu walishajibadilisha na kwenda pale kimwili, unadhani walikuwa wanaweza kushindwa kula kweli kwenye hiyo hali ya kimwili waliyo kuwa nayo kwa muda huo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…