Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

Wanalipwa ndo maana kelele mingi, tunajuwa ukweli kuwa hao wapenda mabadiliko nao wana maboss ambao wako upande wa pili, hatuhangaiki tena.

Kwa ufupi upinzani ni ka genge ambako kqzi yake ni kuisaidia serikali kufanya mambo yake.

Lazima vikelele kelele viwepo.ndo nchi ibaenda.

Bure kabisa
Fikra zako nafikiri ni finyu mnooo.

Sikupingi Kuna upinzani wa Mrema na Upinzani wa Wapinzani.
Unaowafikiria wewe wanajulikana hawakuwahi na hawatowahi kulala polisi, magereza na wala kushtakiwa na serikali kinyume chake ni wapinzani. Kazi kwako.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu na adui yangu wa miaka mingi,wewe mwenyewe nilikukumbusha utubu na kuomba msamaha kwa matendo uliotenda Karagwe,Bukoba Manispaa na Vijijini mwaka 2015 ..muache Makonda awe kichwa ngumu kama wewe.
Bishweko Haha
 
Daima kumbuka hili: If you live like a dog you will die like a dog!

Tafsiri rahisi ni kwamba..ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga.

Makonda yote anayoyapitia kwa sasa hakuna la bahati mbaya!

It is very easy for the oppressor to forget. It is never easy for the victim to forget. Kuna wengi huyu kijana ali turn maisha yao upside down. kuna watu walipoteza uhai wao simply because mawazo au vitu walivyoviamini vilipingana na wenye madaraka. Kuna waliopoteza wapendwa wao, wazazi, watoto, marafiki nk.

Unfortunately, hawana pa kusemea. hawana instagram. hawana facebook. hawana twitter. Wamemwachia Mungu wao afanye maamuzi.

Kama hizo mahakama zingekuwepo na zinatoa haki, hakika Makonda asingefanya aliyoyafanya. Kwa hiyo kuwaambia victims wake waende mahakamani..ni kama kuwasimanga. maana hata wewe sidhani kama unaamini mahakama zetu zinaweza kutenda haki pale mwenye fedha au madaraka akivunja sheria. Zikitenda haki ni selectively kwa wale waliopishana kauli na watawala.

Daima naamini kwamba Mungu ni wa wote. Wenye nacho na wasio nacho. Majira huyapanga apendavyo.

wasalaam,
Masanja umeandika kila kitu. Tatizo hata inaweza isiwe mahakama... anaweza kujitokeza DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi na jamaa akaachiwa. Huyo jamaa anayejifanya Yesu hajawahi kukutana na balaa la Makonda ndo maana anajiropokea tu na kiingereza chake uchwara.
 
Atavukaje boda? Kwa passport hii hii? Si inapigwa pini Kila alitaka clearance alarm inalia?.

Ili asiendelee kuchafua watu, apelekwe segere matata
Akimbie pale boda kama alivyofanya Lema!
 
Evaluate your battles carefully, sometimes peace is more important than being right.......

Miaka ya nyuma nikiwa na mawazo machanga nilikuwa navutiwa sana na hizi siasa za gizani, hila, fitna, visasi, propaganda na kuchafuana. Lakini siku zilivyoenda nikafahamu kwamba nchi huwa haindeshwi hivyo, hasa kwenye taifa la watu ambao wanatamani kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Unaweza ukamfanyia visa Paul Makonda kinyume kabisa na utaratibu wa kisheria, lakini fahamu kwamba mpaka tulipofika hapa ishathibitika kwamba hakuna mtanzania asiyegusika. Awamu ya tano iwe somo kubwa kwa kizazi hiki na kijacho....
Umeyajua Haya badaa ya Jiwe kutwaliwa kwenda Kuzimu sio ?
 
Tunaomba amani itawale! Inawezekana kumsamehe mtu hata Kama hajaomba msamaha Ili kuandaa mazingira ya amani. Naomba Makonda asamehewe hata Kama hajaomba msamaha na Mungu atawabariki!
Basi tukawafungulie wafungwa wote
 
Hayo uliyomshauri tayari kashachelewa. Sidhani hata kama passport yake anayo sasa hivi. Ninashauri serikali iwapeleke mahakamani washenzi wote wa awamu iliyopita ili kuwe na utawala wa kisheria badala ya kuendeleza uhuni katika sura mpya. Rais Hichilema wa Zambia aliteswa mno na utawala uliopita ila anachofanya kwa sasa ni kuwapeleka mahakamani washenzi wote wa awamu iliyopita kiasi kwamba huwezi ona kabisa kama analipiza kisasi. Nitafurahi sana kama Ali Hapi atafikiwa na rungu la walamba asali.
 
Makonda haruhusiwi kuingia US, kwa sababu ya "kuwanyima watu haki ya kuishi".

Muuaji mnamshauri akimbie bila ya kufikishwa mahakamani? Siungi mkono yeye kuviziwa mafichoni, lakini ni halali kabisa kwa yeye kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma dhidi yake.

Waliopo kwenye vyombo vya dola, wanaeleza kwamba mtu huyu aliongoza kikundi cha kuwateka, kuwaua na kuwapoteza watu waliokuwa wakimkosoa marehemu na serikali yake, na kwamba kikundi hicho kiliaminika na kupewa nguvu na marehemu kuliko taasisi rasmi ya TISS. Kikundi hiki kiliwajibika moja kwa moja kwa marehemu. Kikundi hiki, kwa kauli za Siro, zaidi kilifahamika kama "Watu Wasiojulikana", japo walikuwa wanajulikana.

Huyu ni vema akamatwe mapema, ajibu tuhuma dhidi yake, awataje watu wake aliokuwa akiwatumia kuendesha uharamia. Mmoja tunaambiwa yupo mahabusu kule Kusini mwa nchi kwa kosa la kumpora fedha mfanyabiashara na kisha kumwua.

Sabaya wakati akiwapora watu fedha kwa nguvu, alikuwa akiwaambia kuwa, hii inaitwa Makonda style! Sabaya naye ni shahidi muhimu dhidi ya Makonda.

Sanane kapotezwa
Azory kapotezwa
Kanguye kapotezwa
Lisu alimanusura
Mo alitekwa na kuachiwa
Roman alitekwa na kuachiwa
GSM waliporwa mamilioni ya pesa kwa vitisho mbalimbali
Mengi aliporwa mamia ya mamilioni kwa kudanganywa
Familia ya Chacha kule Mwanza waliporwa kiwanja Capripoint
Kuna watu wengine waliporwa fedha kwa ahadi kuwa ataongea na marehemu walegezewe kodi na wawe karibu na Serikali.

Makonda atendewe haki, asiviziwe mitaani, apelekwe mahakamani kama alivyofanyiwa Sabaya, akajibu tuhuma mbalimbali, ikiwemo za mauaji. Makonda ni mwovu mkubwa, kwa kiasi kikubwa, zaidi ya Sabaya. Mwanafunzi wake wa uovu, Sabaya, yupo jela, mwalimu wake yupo huru. Hii siyo haki.

USA ukiua kwa kutumwa nao hawana Shida. Hata kwao juzi tu wamelambana risasi kwenye Basi. Hawana Shida. Itakuwa wana mahaba sana na Tanzania kwa Uzuri wa sura zetu.
 
Ushauri kwako Makonda kunusuru maisha yako na familia yako!

Hama Nchi Kwa Muda watu uliowatesa ni wengi ila kwakuwa tumeambiwa samehe 7 mara 70 tumeshasamehe ila Kwa Usalama wako zaidi hamia Kwa Mkeo ukweni Rwanda Au Nenda Ulaya Kasome hata Miaka minne utarudi Tanzania hasira za wengi zikiwa zimetulia,


Kuna Mawili
- Kuna Kupoteza maisha kutoka Kwa hao watesi

- Au Kuna kufungwa Kabisa maana wapo wenye vielelezo vyote juu yako!

Najua a safari yako ya Kwenda ufaransa ilifeli Kwa kutokana na kigezo ulichoombea asylum haitafutwi hivyo!

Kuna mtu mmekaa wote kwenye gari Masaa 4 mbezi beach alitumwa Kwa kazi maalumu kukushauri baadhi ya mambo kuhusu wewe na Jamaa wa VX na wanachama wa mambo fulani ukaonekana kuogopa ila alivyoondoka ukashupaza shingo tena!

Mifumo Duniani kote ipo hata Kama Serikali ipo.

Nakusihi tena usisahau kufuatilia hayo mambo ama by December 2023 tutakuja kusema habari nyingine Mdogo wangu ! Anza maisha upya nchi yeyote

Ukifika huko wala usihangaike nao uwawezi tena kwakuwa huna cheo!

Pia salimisha ile bastora umiliki wake haujahakikiwa


Britanicca
Kwa hiyo anatuachia Dar yetu.. oyooooo…💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽
 
Back
Top Bottom