Naanza kuamini Bundi kulia usiku Mahali palipo na mgonjwa ni ishara mbaya

Vinavyoishi ulimwengu wa roho ili vifanyekazi ulimwengu wa mwili moja kwa moja vinahitaji mwili! Mizimu, na mambo ya kichawi yako ulimwengu wa roho, vinapotaka kutia msisitizo kufanya kile walichotumwa kukifanya wakiwa katika ulimwengu wa roho, basi huchukua miili ya viumbe tunavyovijua ambavyo watu wengi huwa tuna utata na hivyo viumbe kama nyoka, bundi, paka, popo, n.k, na kuja katika ulimwengu wa mwili. Mara nyingi ukiona unasongwa na hivi viumbe, usichukulie poa! Kama ni Mt Mungu (mwombaji) basi jua ni ishara ya mapambano katika ulimwengu wa roho hivyo omba
 
vitu viwili au zaidi vikitokea kwa pamoja, au kufuatana kwa namna isiyo ya kawaida, watu mtahusianisha na uchawi, kama hapo bundi kulia kufuatana na mtoto, au kuna yale matukio unakuta flani kafariki leo na ndugu yake kafariki siku chache baada, mtasema nguvu za giza, ila sio kweli ni ushirikiano wa matukio(coincidence)

na pia kuna kitu kinaitwa 'placebo effect' kwamba ukiaminishwa kitu sana basi akili yako itatafuta njia ya kukileta hicho kitu kwenye uhalisia, kama hapo kwa vile wabongo tuna nadharia potofu ya kuamini wanyama kama bundi, paka, popo na kunguru wanahusiana na uchawi, basi kitendo cha wewe kumsikia bundi wakati mtoto anaumwa ukaunganisha matukio.

Akili ya mwanadamu ina nguvu sana.
 
Inasemwa bundi ana uwezo mkubwa wa kusikia au ku sense mzoga au seli zilizo kufa...

So unaweza ukawa hai lakini bundi aka weza ku sense harufu ya hizo seli zilizo kufa katika mwili wa binadamu........

Fisi pia anauwezo mkubwa wa kunusa na machale ya kujua wapi Kuna mzoga wa kwenda kula....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…