Naanza kuamini Bundi kulia usiku Mahali palipo na mgonjwa ni ishara mbaya

Ok tunaomba picha za huo mfugo wako

Bwana Bima kama umesoma ni vizuri ukazingatia Hatua za kufanya utafiti ili unapotoa hoja kama hizi Watu wasikuone popoma.

Yaani bundi Alie alafu mtoto afe ndio useme bundi akilia ni ishara Mbaya.

Kwa Siku wanalia ndege WA ngapi huo mtaa?

Au Kwa vile Bundi ni ndege MLA nyama kama tai, mwewe, Kipanga, hivyo mara nyingi sio rahisi kuonekana kama walivyo wanyama na viumbe wengine predators, hivyo kitendo cha kumuona na kusikia Sauti yake unaihusianisha na mambo mabaya.

Kwa hiyo Ile ajali ya Bodaboda na mwendokasi iliyotokea assume usikie MTU akisema Alilia ndege Fulani ndio ajali Ile ikatokea, alafu MTU huyo aseme ndege Fulani akilia muda Fulani ni ishara Mbaya. Utamchukuliaje huyo mtu?
 
Kwangu kuna bundi wanaishi, kutaga na kuzaa kwenye paa langu la banda la nje ubavu na ubavu na nyumbani kwangu, nikichungulia diroishani nawaona, tena wameanza kunizowea, wakiniona iwe usiku au mchana hawanikimbii kabisa., kwa miaka sasa, nadhani wanakwenda kizazi cha sita au saba.

Nnawapenda sana na kuwalinda sana na mapaka. Ni walinzi wazuri sana wa usiku, uwanjani kwangu hakatizi panya wala mjusi wala nyoka, wanaipatapata fresh.

Namshukuru Allah kuniwekea ndege hawa kuwa ni jirani zangu wa karibu kabisa.

Ni ndege wazuri na wanapendeza sana.
 
Nilishawahi kuona bundi shuleni tena juu ya mti, yupo kwenye tawi moja refu ametulia zake tu analialia mdogo mdogo, analia na kunyamaza. Nilimuangalia pale kama dakika kumi hivi, Kila nikimtishia ananiangalia tu ila ana macho Fulani hivi makali sana, then nikampotezea nikaingia darasani kusoma Sasa kesho mwanafunzi mwenzangu alianza kuumwa ghafla kwenye chumba cha mitihani, akaanza kutapika vitu ambavyo havieleweki kama vile mapovu ya maziwa Yale yanayochemshwa, kesho jamaa yangu huyo kafariki usingizini daah at 16 yrs kafa kama utani...nikafikiria kuhusu watu wasemavyo bundi akija huja na matatizo nikafikiria mbona nilishasikia milio ya bundi wengi sana Kijijini huko Kwa bibi na Babu still nothing happen...ila bundi ni symbol maalum kwenye taasisi nyingi tu duniani Hadi hizi za dini, Kuna kitu maalumu Kwa bundi inawezekana! bundi mwenyewe nafikiri Hana ubaya, ila binadamu ndo wabaya.
 
vitu viwili au zaidi vikitokea kwa pamoja, au kufuatana kwa namna isiyo ya kawaida, watu mtahusianisha na uchawi, kama hapo bundi kulia kufuatana na mtoto, au kuna yale matukio unakuta flani kafariki leo na ndugu yake kafariki siku chache baada, mtasema nguvu za giza, ila sio kweli ni ushirikiano wa matukio(coincidence)

na pia kuna kitu kinaitwa 'placebo effect' kwamba ukiaminishwa kitu sana basi akili yako itatafuta njia ya kukileta hicho kitu kwenye uhalisia, kama hapo kwa vile wabongo tuna nadharia potofu ya kuamini wanyama kama bundi, paka, popo na kunguru wanahusiana na uchawi, basi kitendo cha wewe kumsikia bundi wakati mtoto anaumwa ukaunganisha matukio.

Akili ya mwanadamu ina nguvu sana.
Upo sahihi. Nachoamini kuishi na positive mind ni vizuri sana. Lakini umekiri kuhusu nguvu ya maneno. Iwe waliongea kweli au uwongo na kinatokea haina budi kuamini kwenye jambo hilo. Mfano ishu ya laana na mikosi ni vitu ambayo si halisi ni fikirishi lakini mzazi akikutamkia laana huji kuishi vizuri kamwe. Je hio nayo tusiamini? Au nakupa mtihani mmoja tu nenda kamtukane mama yako afu akumwagie radhi tuone nn kitakutokea
 
😂😂😂😂
Kwangu kuna bundi wanaishi, kutaga na kuzaa kwenye paa langu la banda la nje ubavu na ubavu na nyumbani kwangu, nikichungulia diroishani nawaona, tena wameanza kunizowea, wakiniona iwe usiku au mchana hawanikimbii kabisa., kwa miaka sasa, nadhani wanakwenda kizazi cha sita au saba.

Nnawapenda sana na kuwalinda sana na mapaka. Ni walinzi wazuri sana wa usiku, uwanjani kwangu hakatizi panya wala mjusi wala nyoka, wanaipatapata fresh.

Namshukuru Allah kuniwekea ndege hawa kuwa ni jirani zangu wa karibu kabisa.

Ni ndege wazuri na wanapendeza sana.
😂😂😂😂😂Hii kamba hii
 
Ni wiki 2 mfululizo maeneo nayoishi kuna jamaa alimleta mkewe kwao ambaye alitoka kujifungua mtoto wa kike. Ndani ya hizo wiki mbili katoto hako kachanga hakakua na afya nzuri usiku kalikua kanalia sana. Cha kushangaza Kanapolia au anamaliza tu bundi naye akawa analia sana hasa mida ya kuanzia saa saba usiku. Hii ni tofauti na siku za nyuma hatukua tukisikia hizo kelele za bilundi na hata baada ya mtoto kufa hatujasikia tena. Hii ni ajabu sana! Binafsi sikuwah kuamini hilo
Bundi anauwezo kujuwa mtu anakufa kabla hajafa binadam kabla hajafa hutoa harufu ya kifo japo sio rahisi kunisikia ila bundi anaisikia hiyo harufu
 
Nilishawahi kuona bundi shuleni tena juu ya mti, yupo kwenye tawi moja refu ametulia zake tu analialia mdogo mdogo, analia na kunyamaza. Nilimuangalia pale kama dakika kumi hivi, Kila nikimtishia ananiangalia tu ila ana macho Fulani hivi makali sana, then nikampotezea nikaingia darasani kusoma Sasa kesho mwanafunzi mwenzangu alianza kuumwa ghafla kwenye chumba cha mitihani, akaanza kutapika vitu ambavyo havieleweki kama vile mapovu ya maziwa Yale yanayochemshwa, kesho jamaa yangu huyo kafariki usingizini daah at 16 yrs kafa kama utani...nikafikiria kuhusu watu wasemavyo bundi akija huja na matatizo nikafikiria mbona nilishasikia milio ya bundi wengi sana Kijijini huko Kwa bibi na Babu still nothing happen...ila bundi ni symbol maalum kwenye taasisi nyingi tu duniani Hadi hizi za dini, Kuna kitu maalumu Kwa bundi inawezekana! bundi mwenyewe nafikiri Hana ubaya, ila binadamu ndo wabaya.
Mchana hua haoni halali ulimshitua asishituke
 
Ni wiki 2 mfululizo maeneo nayoishi kuna jamaa alimleta mkewe kwao ambaye alitoka kujifungua mtoto wa kike. Ndani ya hizo wiki mbili katoto hako kachanga hakakua na afya nzuri usiku kalikua kanalia sana. Cha kushangaza Kanapolia au anamaliza tu bundi naye akawa analia sana hasa mida ya kuanzia saa saba usiku. Hii ni tofauti na siku za nyuma hatukua tukisikia hizo kelele za bilundi na hata baada ya mtoto kufa hatujasikia tena. Hii ni ajabu sana! Binafsi sikuwah kuamini hilo
Binadamu, katika kufa, huwa hafi ghafra mwili mzima, anaanza kufa sehema moja moja au kidogo kidogo. Kila sehemu inayoanza kufa hutoa harufu, ambayo binadamu uwezo wa kuinusa hana. Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kunusa harufu hata iliyo ndogo sana na toka mbali. Hivyo, mtu anapoelekea kufa, bundi husikia harufu hiyo na yeye, kama ilivyo kawaida kwa ndege wengine pindi wanusapo harufu ya mzoga, huja eneo litoalo harufu kwa minajili ya kukuta mzoga. Kitendo cha bundi kusogea karibu, na mtu kuendelea kuelekea kufa, bundi huzi kusikia harufu, hali itakayomfanya aendelee kuwepo eneo hilo. Na kwa kawaida, bundi lazima alie au atoe sauti yake. Sasa binadamu wakimuona bundi, au wakisikia sauti ya bundi karibu na eneo alilopo mgonjwa, na mara baada ya muda mfupi mtu afe, huamini kuwa bundi analeta uchuro. Kumbe siyo. Ni sawa tu na nzi anapotua eneo lenye kinyesi au uchafu.
 
Upo sahihi. Nachoamini kuishi na positive mind ni vizuri sana. Lakini umekiri kuhusu nguvu ya maneno. Iwe waliongea kweli au uwongo na kinatokea haina budi kuamini kwenye jambo hilo. Mfano ishu ya laana na mikosi ni vitu ambayo si halisi ni fikirishi lakini mzazi akikutamkia laana huji kuishi vizuri kamwe. Je hio nayo tusiamini? Au nakupa mtihani mmoja tu nenda kamtukane mama yako afu akumwagie radhi tuone nn kitakutokea
umeeleza vizuri ila sijasema kuhusu nguvu ya maneno nimesema kuhusu ushirikiano wa matukio, matukio yanaweza kutokea pamoja au kufuatana, ni ngumu sana kuelezea...

labda niseme hivi, matukio mawili au zaidi yanaweza kutokea pamoja au kufuatana kama hayavunji kanunui za kisayansi, kwa mfano, mtu hawezi kupaa, hili haliwezekani lakini inaweza kutokea ajali na akanusurika abiria mmoja kwasababu flani flani ila inawezekana kwasababu ipo kwenye uhalisia....

kuhusu hayo mambo ya laana, sio ustaarabu kumtukana mzazi au kumtendea vibaya, na ukifanya hivyo ile hali ya majuto kutokana na lawama utakazopata zitakutengenezea kitu kinaitwa 'cognitive bias' yaani unaviona vitu vibaya tu vinavotokea kwenye maisha yako, na hapo utakua unasingizia kwamba ni kwasababu ya laana ya mzazi....

Naomba niishie hapa mkuu kwa leo inatosha
 
Ni wiki 2 mfululizo maeneo nayoishi kuna jamaa alimleta mkewe kwao ambaye alitoka kujifungua mtoto wa kike. Ndani ya hizo wiki mbili katoto hako kachanga hakakua na afya nzuri usiku kalikua kanalia sana. Cha kushangaza Kanapolia au anamaliza tu bundi naye akawa analia sana hasa mida ya kuanzia saa saba usiku. Hii ni tofauti na siku za nyuma hatukua tukisikia hizo kelele za bilundi na hata baada ya mtoto kufa hatujasikia tena. Hii ni ajabu sana! Binafsi sikuwah kuamini hilo

Mshamloga mtoto wa watu kwa wivu wenu.
 
Back
Top Bottom