Mimi ni Shuhuda, mwaka 2020 Mwezi April tarehe 19 usiku, nikiwa hapa Europe- Bundi alilia sana juu ya paa langu saa nane usiku (kwa hapa Ulaya hii ni nadra sana na sijui huy Bundi alitokea wapi, hata mke wangu alishangaa na akaanza kusema angels are visiting us), nikatoka nje nikamfukuza na kurudi kulala, baada ya muda , mbweha naye akaanza kulia kama sauti ya mtu... nikasema leo kuna namna. Sijakaa sawa, paka akaanza vile vile... ile kumekucha tu, naambiwa pole sana kwa kufiwa na kaka yako. Na sio hiyo tu, huwa nikiota kwamba niko kwenye sherehe ya kula nyama, ni lazima ndugu yangu wa karibu naye akitoe, sijui huu ni uhusiano wa namna gani. Wiki jana tu nimeota habari za kula nyama na Bundi akalia usiku, asubuhi yake binamu wangu ambaye alikuwa ni bodaboda, akasagwa na bus la JWC hapo Maili Moja Kibaha. Usidharau unachoota ukiwa umelala, wakati mwingine ni messages. Na nina mambo mengi sana ambayo nimeyaona ndotoni na nikayashuhudia, mfano, niliota oia kwamba malika na mashetani yanapigana hapo mtaani wangu, kulipo kucha tu , mchana wa siku hiyo kukatokea zogo kubwa mtaani kwangu na mmoja wa marafiki wangu aliuwawa kwa kuchoma kisu na washikaji zake...
Ninacho taka kusema nini? usiwe pinga pinga kila kitu, maana ktk ulimwengu mwingine haya mambo ni ya kawaida sana na maisha yanaendelea mwili ukiwa hauna uhai kwa mujibu wa huyu bwana Dactari wa upasuaji aliyepigwa radi na akapona- hebu sikiliza ushuhuda wake hapa :
View: https://youtu.be/fCV7ayCLA1A?si=HrjsIt965idR7ab-