Kuna watu humu hawaziamini ndoto... Nikiwa nimechaguliwa kwenda Songea Boys, huko nilikuwa sipajui, niliomba tu Mungu anijalie kupajua pakoje, na kabla ya kwenda huko, ndioto ikanionesha mazingira ya huko jinsi yalivyo mwanzo hadi mwisho. Na siku nilipolipoti, ikawa vile vile nilivyoiona kwenuye ndo. Na mwezi 11 mwaka jana, niliota kuhusu kifo cha yule baba mtakatifu na mavazi yake ya mwisho atayo valishwa siku ya kuzikwa kwake- ajabu na kweli, siku ya mazishi ikawa vile vile nilivyoona kwenye ndoto. Hadi sasa, ndoto ninaziogopa sana kwa kweli. Watu wasizipuuzie kwa kweli, ni message toka huko semehu zinapotoka... changamoto ni namna tu ya kuzisoma...