Naanza kutilia shaka uwezo wa Rais Samia kuongoza Taifa

Uwezo wa Rais ni mdogo sana, sikuamini kama Rais ndo anajibu vile
 
JF inaongoza kwa wataalamu wa masuala ya IQ
 
Nampongeza madam president amefanya vema kuongea na BBC. Lazima tufahamu asili yetu binadamu kwamba mwanaume ni tofauti na mwanamke. Kwa hulka,silka na haiba ya mama yetu tunahitajika kumpongeza.
Kweli kabisa huyu mama tusimtwike zigo zito Kama Lile la katiba,ambalo wanaume wenyewe walilikwepa JK alipolianzisha alipogundua ni zigo la misumari akavuta muda ili aje kumrushia zigo ajaye.
Alikuja JPM mzee wa kubana matumizi alisoma mchezo mapema akaepa.

Sema tu mama alikosea aliposema wasubiri.Alitakiwa aseme tu kuwa haliwezekani kabisa kwenye utawala wake.
 
Iwapo leo ndio umeanza kutilia shaka basi kichwa chaka siwezi kukitofautisha na utendaji kazi wa computer ya 1995 yenye windows 95!
 
Ulivyoanza nilitaka kukusapoti,lakini umeharibu sana kugusa katiba mpya na kuonesha siyo agenda muhimu.
Tafakari upya

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Niliingia mtego wa kumpenda na kumheshimu mama samia suluhu mara tu alipoapishwa kuwa rais nikijua atakuwa rais bora lakini nimegundua nilikuwa wrong, niliapa kumpa kura yangu 2025 ingali mm ni mpinzani!!
Anyway mama amekosea sana kwa suala la mbowe na akitaka watanzania tulio na akili timamu turudishe upendo kwake amalize suala la mbowe kwa akili na atimize ahadi yake ya kuonana na watanzania wenzetu (vya vya upinzani)
Tujenge nchi yetu na turudishe umoja na upendo na mshikamano kama watanzania.
 
Umempa za uso vizuri sana!

Eti wanataka watukane waangaliwe tu, waandamane waangaliwe tu, wafanye ujinga wote waangaliwe tu!

hawa watu sometimes unaweza sema wana hidden agendas. Nchi gani makini Haina utaratibu mzuri wa kufanya mambo yake?
Kama hata wewe umemgeuka Lisu basi kuna shida
 
Hivi hii inatoka wapiiiii
 
Niite vyovyote vile unavyotaka lakini nope, si kila unachotaka katika maisha lazima ukipate.

Na ung'ang'anizi wenu unazidi kuwaumbua jinsi mlivyo watu wasioaminika hata kidogo.

Ni majuzi tu Magufuli alizitilia mashaka chanjo mkamwita mshamba wa Chato. Leo hii mama kaleta chanjo mmeshamgeuka kuwa ni chanjo za majaribio?

Ni majuzi tu mlimponda Magufuli kwa kutumia nguvu kubwa suala la kuhamia Dodoma. Leo hii mnamponda mama kutoichukulia serious Dodoma?

Kelele zenu kuhusu miamala, tozo, katiba mpya, bla bla... ni kelele za mtu anayetafuta umaarufu upya baada ya kupoteana. Msifikiri tumesahau kelele zenu kuhusu ufisadi baadaye mkamkumbatia mtu mliyetumia miaka kibao mkituaminisha ni fisadi.

Msitumie nguvu kubwa kupambana na adui mnayeamini ni mwingine. Adui yenu ni nyie wenyewe. Mna akili ndogo sana za kufanya siasa zenye tija.
 
Nakusikilizia ili nijue vijana wa CHADEMA wanasema nini, baada ya miezi 4 ya kumsifu na kuamini Magufuli alikuwa hovyo sana!! Lakini wajue, walipotoa sifa hizo, mwenzao alizivaa na kujiamini kwamba kumbe anafaa sana! Sasa M'kiti wao yuko ndani bila hata kelele za chama. Nasema ndani!!

Sisi wengine tunaojitambua tuliposikia elimu ya hapa na pale, baadaye Mzumbe, baadaye Open University, zikaja clip za kuonesha niya yake ya kutaka Ph.D...... aaah, basi! Ni wapi rais wetu huyu mwenye jinsia ya kike aliwahi tumia ubongo wake kwa kiwango cha juu kabisa? Wapi jamani?
 
Oooh! anajua kiingereza, oooh! huyu ni muungwana, Oooh! angalau watu wana nyuso za furaha! Yaani tuna mijitu mijinga ktk nchi hadi inatia shaka. JF yenyewe imejaa mijitu ya hovyo hovyo hadi unashangaa mitandaoni inafanya nini! Tena watu wako ktk ajira za serikali wanatamani rais mzembe!
 
Mie tu pale alipokuwa akiwahoji sijui wakandarasi au nani pale Kariakoo mwendokasi 🙂 🙂 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…