Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile wala hauwezi kuthibitisha hilo .
 
Huyo ni kweli Nabii wa Uwongo ila kwenye suala hili kasema ukweli.

Nitamani humu awepo Semenya Mgerasi Maghayo The Mongolian Savage atie neno kidogo.
 
UISLAM NI LIDUDE KUUBWA,.. A well structured religion!

By the way., Jiulize kwanini watu wengi wenye itikadi ya Atheism humu JF wametokea kwenye Ukristo na sio Uislam?,
Mimi nimetokea kwenye Uislam ,ila wakristo japo wapo kwenye box ila wana uhuru mkubwa wakufikiri 🤔
 
Hadithi za uumbaji ni porojo tu.

Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Hakuna Mungu.

Hakuna Shetani.

Binadamu hawaumbwi, Binadamu wanazaliwa.

Tunazaliana wenyewe kwa wenyewe.
Sawa, binadamu wa sasa tunazaana, je binadamu wa kwanza kabisa hapa ulimwenguni alitoka wapi mkuu?
 
Biblia ni kama introduction tu kwa beginners yaani Wakristo wa level ya kwanza au chini ya ufahamu wa maandiko.
Ukitaka kuyajua zaidi unaingia kwenye level za juu za ufahamu kuhusu Biblia.
Biblia ni coded books kimebeba funguo za siri za ulimwengu kwa level ya kwanza ya ufahamu wao uishia kwenye level za kukemea mapepo au kupiga ishara za msalaba.
Vitabu vyote vingewekwa kwenye Biblia isingetosha kwa uzito ingefikia uzito wa tani moja thus mengine yanapatikana kwenye Library za Siri Vatican,Paris nk.

Vipo vitabu vinaelezea tu habari moja tofauti na Biblia imejumlisha vingi.
Mfano Pana Kitabu kinaelezea tu maisha ya Adam na hawa pekee tangu bustani hadi walipokufa,
Pana kinachoelezea tu maisha ya Yesu hadi ile miaka 18 iliyopotea ambayo huzipati kwenye Biblia
Pana vitabu vingi sana nje ya Biblia mfano kitabu cha Enock, Anunak nk
 
Adam na Hawa walizaa watoto wengine baada ya Kaini na Abel na Kaini alikuja kuoa mmoja wa dada zake, kumbuka zamani watu waliishi hadi miaka 900 sasa kama walianza kuzaa wakiwa na miaka 16 hadi wafike miaka 600 walizaa maelfu mangapi
 
Huyo sio nabii ni white magician hao huwa hawatumii Biblia kwenye madhabau zao huwa wanaweka kama gheresha tu.
Huyo sio Mkristo ni kama zumaridi bali wanatumia Ukristo kutengeneza maisha thus hawaendi ktk misingi ya Ukristo
 
Nabii yuko sahihi
Nabii yuko sahihi.
 
Nyoka ni mmoja ya wanyama walioumbwa shetani ni roho inauwezo wa kuingia kwenye kiumbe chochote alimtumia nyoka kwa sababu ni kiumbe mwerevu na mjanja kuliko viumbe vyote
 
Kutafsiri biblia kwenye lugha zingine kumeleta huu utitiri wa madhehebu. Wafasiri husimamia misimamo yao ya kiimani kwenye kutafsiri. Anayeamimi katika utatu mtakatifu atafasiri kwa mrengo huo. Anayeamini binadamu akifa handing mbinguni mpaka siku ya kiama hata ule msemo wa Yesu kwa yule mwizi pale msalabani ataweka mkato (,) baada ya neno "nakuambia", anayeamini vinginevyo ataweka mkato baada ya neno "leo". Hapo theologically tayari ni mafundisho mawili tofauti. Afadhali wenzetu waislamu wanajifunza kitabu chao kwa lugha mama. Ukristo umepoteza mwelekeo.
 
Mbona baalamu alisemeshwa na farasi alipokwenda kuwaalani waisraeli kwa amri ya mfalme wa moabu balaki?😅
Bila shaka hiyo ilikuwa katika kitabu cha Kumbukumbu la torati......hiki kitabu ni riwaya kama riwaya nyingine mkuu......katika riwaya mwandishi amepewa mamlaka ya ku impersonate viumbe visivyokuwa binadamu.
 

Mwanzo 4:17-26 BHN​

BHNSUVNenoSRUV
Kaini akalala na mkewe, naye akapata mimba, akamzaa Henoki. Kaini akajenga mji akauita kwa jina la Henoki mwanawe. Henoki akamzaa Iradi, naye Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, naye Methushaeli akamzaa Lameki. Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada na mwingine Sila. Ada alimzaa Yabali ambaye alikuwa baba yao wafugaji waishio mahemani. Ndugu yake alikuwa Yubali; huyo alikuwa baba yao wanamuziki wote wapigao zeze na filimbi. Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila sikieni sauti yangu! Sikilizeni nisemayo enyi wake za Lameki. Mimi niliua mtu kwa kunijeruhi, naam, nilimuua kijana kwa kuniumiza. Ikiwa Kaini atalipizwa mara saba, kweli Lameki atalipizwa mara sabini na saba.” Adamu akalala tena na Hawa mkewe, naye akazaa mtoto wa kiume, akamwita Sethi akisema, “Mungu amenijalia mtoto mahali pa Abeli aliyeuawa na Kaini.” Sethi naye alipata mtoto wa kiume, akamwita Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kumwomba Mwenyezi-Mungu kwa jina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…