Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Mwamba nyoka anayetajwa sio nyoka yaani nyoka Kama unavyojya wewe neno lilitumika NI serpent (kifasihi zaidi) na sio snake .biblia inasema nyoka alikuwa ana hekima kuliko wanyama wote aliowaumba Bwana Mungu .maana Ake n kwamba Nyoka alikuwa agent wa maarifa.amabaye alitumea na Mungu kumjaribu Adam suala la kuongea Kwa nyoka sio tatizo kiasi ujiulize hivi wanyama uwa wanaongea ? Kuna punda aliongea ndani ya biblia .



Kuoa Kwa Cain .Mwamba biblia yote unayoiona haina utaratibu wa kurecord kuzaliwa Kwa wanawake yaani inshort biblia NI mfume dume .Cain alioa dadaake ..Hawa akizaa mtoto wa kike .Biblia haisemi.


Napingana na nabii mkuu kwamba biblia NI maneno ya wanadam Kwa hoja .Kama ni kweli na yeye akaandike ya kwake .
1. Who created the serpent and for which purpose?

2. Kama mke wa Cain hakutajwa mahali popote halafu wewe unatuambia eti alimuoa dada yake, wewe umejuaje wakati hilo jambo halikuandikwa mahali popote? Huoni kwamba nawe unataka kutuletea hadithi za Abunuwasi?
 
Kuamini pia inaweza kuwa kichaka cha kupotosha na wamisionari Lengo lilikua hilo ,upotoshwe ili iwerahisi kuku manipulate 🤔
Mkuu sisi tunaomuamini Kristo hakuna linalotutikisa.

Elimu ya dini ni pana sana, wenye maslahi wapo, waongo wapo, neema ya Yesu Kristo ndio inamfunulia mtu ukweli, sisi hatuna nguvu wala akili za kuyajua haya mambo kwa usahihi wake.
 
Unaweza kuthibitisha hili au ni story za vijiweni na akina Mazinge?
Nicene council haikugusa biblia shughulisha ubongo
Mimi kawaida yangu ni kusoma mambo sio kusikiliza waliopotea mfano wa kina Mazinge , Mimi mwenyewe ninao akili na uwezo wa kufuatilia mambo kwa umakini na undani kabisa.

Wapi nimesema Nicae imehusika na kuchange Bible , nimesema Nicaea nimegusia kwenye kusuka mambo nikaweka na uhusiano wa kuhusu Kuchange kuhusiana na kubadilisha Biblia ikiwa mambo muhimu ya itikadi na mengineyo hayakuwa stable na kueleweka mpaka wakae watu washauriane na kuweka sawa basi suala la Bible litakuwa jepesi sna kufanyika
 
Huyo Mungu alikuwa wapi hadi Shetani akaweza kumdanganya Eva?

Huyo Mungu kwa nini aliruhusu shetani aingie bustanini, kumdanganya Eva?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Nimekufatilia toka mbali ila hapa umeanza kukosea ndugu yangu

Usimtukane MUNGU MWENYEZI ni mkali tukana tu hizi dini lakini siyo MUNGU atakupiga acha rafiki yangu
 
Mkuu sisi tunaomuamini Kristo hakuna linalotutikisa.

Elimu ya dini ni pana sana, wenye maslahi wapo, waongo wapo, neema ya Yesu Kristo ndio inamfunulia mtu ukweli, sisi hatuna nguvu wala akili za kuyajua haya mambo kwa usahihi wake.
Kuamini ni sawa kabisa wala hakuna tatizo ,shida inakuja pale mnapotaka kila mtu aamini vile mnavyo amini nyie , wayahudi mabudha shinto na wahindu hauwezi wakuta kwenye huo mkenge.
 
Uislam nao ulikopi tu kwenye biblia wakajazia na tamaduni zao kidogo
Haujakopi kwenye Biblia , Biblia imejaa upotoshaji mwingi na Kuna baadhi ya mambo ya ukweli .

Qur'an inakubali vitabu vilivyopita vya kale kuwa ni Haki na vimetoka kwa Allaah mfano Injili ,Zaburi na Taurati na imekiri imekuja kuthibitisha baadhi ya mambo yaliyoko humo ndio maana unakuta baadhi ya stori za kwenye bible zipo mule.

Ila vitabu vyote vya kale vimepoteza uhalisia wake vilivyobaki masalia yake yamechangnywa ukweli na Uwongo ndani yake mfano hiyo Bible , hata kwenye visa na baadhi ya matukio ya kiihistoria yanayofanana tumetofautiana na kiitikadi ndio kabisaaa..
 
Adheists na kobazi hapa wanafurahia na kushabikia kama fisi aliyepata mzoga mkubwa ale mpaka ashibe. Hii ngoma inajibiwa freshi tu, hakuna hoja hapa nabii anapotosha ukweli. Huu uzi usifutwe ili huyo wakala wa shetani ajibiwe kikamilifu
Toa sasa majibu!
 
Kwa kadiri tunavyoelekea mwisho wa nyakati, shetani atajifunua wazi kabisa, maana amechoka kujificha. Kwa hiyo watu watamfuata shetani wakijua!!!!!! Ndio maana kwenye hukumu ya mwisho, watu watajipekeka wenyewe kwenye ziwa la moto.
Shetani hayupo wala Mungu.
,hayupo, hizo njugu walioziandika walijua kabisa ipo silu watu watapata akili ,hao jamaa hawakuwa vilaza wala viazi kama kondoo.
 
Haujakopi kwenye Biblia , Biblia imejaa upotoshaji mwingi na Kuna baadhi ya mambo ya ukweli .

Qur'an inakubali vitabu vilivyopita vya kale kuwa ni Haki na vimetoka kwa Allaah mfano Injili ,Zaburi na Taurati na imekiri imekuja kuthibitisha baadhi ya mambo yaliyoko humo ndio maana unakuta baadhi ya stori za kwenye bible zipo mule.

Ila vitabu vyote vya kale vimepoteza uhalisia wake vilivyobaki masalia yake yamechangnywa ukweli na Uwongo ndani yake mfano hiyo Bible , hata kwenye visa na baadhi ya matukio ya kiihistoria yanayofanana tumetofautiana na kiitikadi ndio kabisaaa..
Quran imeboresha tu ndio maana ningetaka kuwa na dini hata ya kuzugia tu ningekuwa mwislamu
 
bakini pembeni na uislam wenu wala msikomenti huu uzi kama hamtaki kuhusishwa acheni ushabiki wakati tunajua utopolo ulioko huko kwenu. Tulieni piteni kimyakimya, hii ngoma tuachieni sisi tunyukane na hao wanaosapoti uposhaji wa geodavie
Alhamdulillah Uzi unatembea uko page ya nane sasa na wapambe hatuko nyuma tunachochea moto mnyukane Wagalatia wenyewe kwa wenyewe , ukipoa tunaiibua tena ukae trending watu waone kuwa wapo gizani wanahitajia Nuru ..
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.

View attachment 3279501
MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.

Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.
​
Kwa hiyo yeye anafanya huduma kwa kutumia kitabu gani?
Sasa nimepata sababu ni kwa nini Goodluck alichoma gari aliyompa.
Kama biblia ni maneno ya watu,na wewe unayatumia kuhubiria watu kwa jina la Mungu hapo kuna walakini mkubwa.
Ipo siku watu kama yeye watataja ni mungu gani wanayemwabudu bila kificho.


Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?

Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?

Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?

Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.

Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.

Nawasilisha.

​
 
Back
Top Bottom