The Coin Man
JF-Expert Member
- Jan 2, 2025
- 1,471
- 1,879
Mwamba unanichanganyia mada .hoja yako ilikuwa NI wapi wanyama wanaongea .nimekupa hiyo ya Balaam .Unataka Twende Kitheology ok sio mbaya..
Sasa Nikuulize maswli kadhaa Kuhusu Hiyo Hadithi..
Kulikuwa na Ulazima Gani Mungu kumtuma Malaika awe anajitega Njiani muda wote kila balaam akimgeuza Punda?
Maana Alimpiga punda akatoka njiani wakapita njia nyingine ila Bado kule bondeni akamweka tena yule malaika walipokuwa njia kuu akamweka tena yule malaika ili Punda amwogope asiende.. halafu baadaye Malaika anamdhihaki kwa Kumuuliza mbona Umempiga Punda mara tatu wakati Punda kupigwa yeye ndyo chanzo?
Kama Lengo Lilikuwa ni Kumstopisha balaam asiende kwanini Kumtesa Punda? Na wakati angeweza Kujitokeza tu na Kumzuia Balaam kama Alivyofanya na Ingewezekana?
Kama Balaam Alienda Na Akafanya Kile alichoamrishwa na Mungu niambie Kosa La Balaam ni Lipi kulingana na Aya Hizi kwenye Biblia Yuda 1:11 na 2 Petro 2:15,
Haya Twende Theologically Sasa
Alimbwa akiwa zeroKwahyi kumbe Adamu Alikuwa na Miaka pia..
Aliumbwa akiwa na Miaka mingapi?
Yeye anatumia ile biblia ya kale iliyofichwa
Nimekuambia Kuwa Ilikuwa Ni metaphor na wala Sio kuongea Kwa Kuongea Hili swala Nimelijibu Ila Ulipohoji Ndo nimekupa Maswali..Mwamba unanichanganyia mada .hoja yako ilikuwa NI wapi wanyama wanaongea .nimekupa hiyo ya Balaam .
So you mean it was God's plan to subject mankind into sin by sending the serpent to Eve beause He knew she was weak and that she could easily accespt the sepent's proposal? If this is the case, why do you think He did it to the creature he had created in His own will?God sent serpent to (deserve) Eve knowing Adam was weak
Hao sio wahusika wa biblia hayo ni matukio yaliyotukia duniani zama mbalimbali na Allah ndio alikuwa anatusimulia.Nimesoma quran kwahiyo kila kinachozungumziwa NI biblia tupu .wahusika takriban wote kasoro Muhammad wametoka Kwa biblia.😸😸
DNA inabadilika kulingana na Mazingira na Sababu nyingi na kupelekea kuzalisha offspring ambayo ni tofauti na ancestors.Hakuna binadamu wa kwanza duniani wa binadamu wote.
Na hili linathibitika kwa uwepo wa utofauti wa DNA🧬 kwenye kila binadamu.
Tunatofautiana vinasaba, hivyo Haiwezekani tuwe tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza.
Tunatofautiana rangi zetu, Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weupe, weusi na wekundu. Kuna wajapan, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea n.k
Wote hawa ni binadamu wenye utofauti wa rangi. Kwa hiyo haiwezekani tuwe tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza.
Kama kweli binadamu wote ulimwenguni tungekuwa tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana kwenye vinasaba na rangi zetu.
Karne kadhaa sio miongo! Ni kama waliremanufacture kitu brand newSasa kama walificha kwa Zaidi ya Miongo kadhaa baadae wakaruhusu Una Uhakika gani kama Hawakubadili baadhi ya Aya?
Palikua na viumbe kabla ya kuumbwa binadam,kuwepo na matunda sumu yasiyo na sumu,siyo kosa la Mungu ikiwa kakuelekeza tunda hili sumu hili siyoHayo maswali ukiwauliza wafia dini humu wanaanza kukulaani, ukweli ni kwamba upeo wao ni mdogo wanapelekwa km nyumbu..!!
Kusoma na kufuatilia mambo ndio hobby yangu hiyo ilichangia nyumbani kuwepo vitabu vingi vya kidini , kiihistoria na Kisiasa vingine vya Zamani ambavyo huwezi kupata madukani kirahisi , Mimi nili tokea niko primary huko darasa la 4 na kuendelea migogoro ya Middle East nilikuwa nafuatilia kwenye vitabu harakakati za Yaseer Arafat na mengineyo nilikuwa nafuatilia japo kutokana na umri nilikuwa napata kama hints tu ubongo huakuwa matured enough kunga'mua vilivyo.Kwa mtu kama Wewe tunaweza Kukaa Meza Moja Tukaongea maana Weww Una observative Analysis..
Tofauti na wale wa "imeandikwa Hivyo na Kama Huna roho huwezi elewa"
Yeah karne kadhaaKarne kadhaa sio miongo! Ni kama waliremanufacture kitu brand new
Mkuu una hoja; usikilizwe. Tusubiri wenyewe waje kutupa majawabu.Hakuna binadamu wa kwanza duniani wa binadamu wote.
Na hili linathibitika kwa uwepo wa utofauti wa DNA🧬 kwenye kila binadamu.
Tunatofautiana vinasaba, hivyo Haiwezekani tuwe tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza.
Tunatofautiana rangi zetu, Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weupe, weusi na wekundu. Kuna wajapan, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea n.k
Wote hawa ni binadamu wenye utofauti wa rangi. Kwa hiyo haiwezekani tuwe tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza.
Kama kweli binadamu wote ulimwenguni tungekuwa tumetokana na binadamu mmoja wa kwanza, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana kwenye vinasaba na rangi zetu.
Hilo andiko linapatikana wapi? Mwanzo umeisoma lakini?Palikua na viumbe kabla ya kuumbwa binadam,kuwepo na matunda sumu yasiyo na sumu,siyo kosa la Mungu ikiwa kakuelekeza tunda hili sumu hili siyo
Kufikirika na kusadikika maana yake ni kutokuwepo?Kupitia imani zenu za kufikirika na kusadikika.
Hahaha Very Impressive Mimi nahisi Ni kama Wewe Sema Mimi Nilivuka more Way further maana Baada ya Kutoka kwenye Uislmu nilikuwa Myahudi 😀😀Kusoma na kufuatilia mambo ndio hobby yangu hiyo ilichangia nyumbani kuwepo vitabu vingi vya kidini , kiihistoria na Kisiasa vingine vya Zamani ambavyo huwezi kupata madukani kirahisi , Mimi nili tokea niko primary huko darasa la 4 na kuendelea migogoro ya Middle East nilikuwa nafuatilia kwenye vitabu harakakati za Yaseer Arafat na mengineyo nilikuwa nafuatilia japo kutokana na umri nilikuwa napata kama hints tu ubongo huakuwa matured enough kunga'mua vilivyo.
Mpaka mtaani watu wazima wakaniona kama mtoto wa maajabu jinsi ninavyowapiga KO kwenye mambo mengi na kuwapa historia na uchambuzi kamili , ikawa kiu yangu kusoma tu nikikua kitu au kupata Maarifa mapya nasikia farahi moyoni , hii ikapelekea nijifosi nijue kingereza mapema ili kuchimba zaidi maana madini kwa kiswahili huyapati kiundani na vitabu vingi vya kingereza nikawa naviweka pembeni kisa lugha.
Kwa ufupi mtu kujielemisha na kufuatilia mambo ni muhimu sana ili ukijua kile unachokisimamia na ukifuate kisawasawa , Mimi niwewahi kusikiliza na kufuatilia vitabu na documentary hatari ambazo against uislamu ambavyo zinaweza kufanya ukatae uislamu kwa haraka mno jinsi spana zinavyopigwa mle lakini nilifungua na kusoma na kusikiliza kutoka na shauku ya ndani na msukumo wa kujua , kufuatilia mambo na kusikiliza hoja kinzani.
Hata katika Uislamu hakujapoa Kuna makundi mengi sana zenye itikadi tofauti tofauti kila kundi linadai wao ndio wako sahihi na wengine potofu hapo pia nilifutilia kwa umakini hizo itikadi na makundi kisha kufanya Comparative analysis mwishowe kuchagua wapi pa kusimamia.
We akili yako hata kutosheleza mahitaji yako haiwezi unaweza kuchallenge maneno ya mwenyenzi Mungu? Upumbavu wa Mungu uko juu sana kuliko huo udwanzi wako. Acheni Mungu aitwe Mungu. Huyo ni wale manaibu wa uwongo ameshaanza kujidhihirisha, hawawezi kujificha utawajua tu kwa matendo yao.Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.
View attachment 3279501
MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.
Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.
Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?
Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?
Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?
Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.
Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.
Nawasilisha.
Kama palikua na nyoka na miti maana yake vilikuwepo kabla ya Adam,na adam na mkewe kurubuniwa haimaanishi Mungu kuzidiwa akili bali udhaifu wa binadam, wangapi wanatapeliwa/danganywa hata leo!?..hilo ni umbile la binadam,free willHilo andiko linapatikana wapi? Mwanzo umeisoma lakini?
Pale kwenye uumbaji kuna siku iliyoonyesha Mungu aliumba viumbe ambao waliweza kumzidi akili yeye?
Ni viumbe gani hao?
Sasa danga km wewe una upeo ganiHayo maswali ukiwauliza wafia dini humu wanaanza kukulaani, ukweli ni kwamba upeo wao ni mdogo wanapelekwa km nyumbu..!!